Kuhusu sisi

wingu la mashahidi

Wingu la Mashahidi  ni huduma yenye lengo la kusambaza  habari njema za wokovu ulioletwa na Bwana wetu Yesu Kristo, kwa njia mbalimbali

Tunaamini kuwa biblia ndio kitabu pekee kilichovuviwa na Roho Mtakatifu kwa lengo la kuwakomboa na kuwakamilisha wanadamu. Hivyo hicho ndio kitovu cha mafundisho yote yapatikanayo katika huduma hii.

Tunaamini kuwa wokovu unatoka kwa mtu mmoja tu naye ni YESU KRISTO, Na huo unapatakana kwa kumwamini, kisha kubatizwa kwa jina lake, na kisha kupokea Roho Mtakatifu sawasawa na  Matendo 2:38

Tunaamini kuwa kanisa tunaloishi ndio kanisa la mwisho, lijulikanalo kama Laodikia (Ufunuo 3:14-22). Na kwamba hili ndio kanisa tutakaloshuhudia tukio la unyakuo.

Zingatia: Wingu la Mashahidi wa Kristo Sio dhehebu la “Mashahidi wa Yehova”. bali jina hili limetoka katika kitabu cha Waebrania 12:1

 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

Hivyo mimi na wewe pia tunaweza tukawa sehemu ya wingu hilo la mashahidi wa Bwana wetu Yesu Kristo, kama walivyokuwa wale wa wakati ule. Na ndio lengo la huduma hii, kuwakaribisha watu wote waliookoka kutoka katika pande zote za ulimwengu wenye imani moja na sisi kushirikiana katika kuipeleka injili ya Bwana wetu Yesu kwa watu wote.

Tunapatikana Tegeta, karibu na kituo cha mabasi cha NYUKI.

Ratiba za Ibada:

Jumapili, ibada kuu kuanzia saa 3:00 asubuhi -6:30 Mchana

Jumatano Mafundisho ya biblia/ Maombezi: Saa 10:00 jioni – Saa 12:00 Jioni

Ijumaa mombezi/Ushauri/ Neno : Saa Saa 10:00 jioni – Saa 12:00 Jioni

Karibu sana.

Na Bwana akubariki

Kwa mawasiliano zaidi piga namba hizi : +255789001312/+255693036618

Print this post

Tutumie ujumbe au Piga

Mawasiliano

Je! utapenda kujumuika nasi? tutumie ujumbe wako

+255-789-001-312

Tunapatikana

Dare es salaam, Tegeta, - Tanzania

Barua pepe

info@wingulamashahidi.org

Utapenda kuchangia?

Mchango wako utaifanya neema ya Bwana wetu iwafikie na wengi zaidi, na hivyo pale watakapomshukuru Mungu basi ni kwa ajili yako pia, Na Mungu atakubariki