Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu katika kujifunza Neno pamoja na Maombi.
Utangulizi: Kusoma Neno bila Kuomba, au kuomba bila Neno la kusimama nalo ni sawa na kitamba cha bendera kisicho na mlingoti, kitapelekwa huku na kule na kupotea…
Kupitia mfululizo huu na tafakari hizi tutapata mwongozo sahihi wa kuomba kwa kusimama na maandiko matakatifu ya Biblia.
Yuda 1:2 “MWONGEZEWE REHEMA na AMANI na UPENDANO”.
Mambo haya matatu ni muhimu kuwa nayo kama watu tuliokokoka
1. OMBI LA REHEMA (Tumia dk 45):
Rehema kwa tafsiri rahisi ni kibali ambacho mtu anaweza kukipokea kutoka kwa MUNGU au kwa Mtu mwenzake, ambacho kinazaa Msamaha, ufadhili, huruma, au msaada.
Kwamfano Mtu aliyerehemiwa na MUNGU, anakuwa amesamehewa makosa yake, au kupewa kibali na Baraka..
Zaburi 78:8 “Lakini Yeye, KWA KUWA ANAYO REHEMA, Husamehe uovu wala haangamizi. Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake, Wala haiwashi hasira yake yote”.
Na rehema za MUNGU ni mpya kila siku.. na zilikuwepo tangu zamani (Zab. 25:6) na zitaendelea milele..
Maombolezo 3:22 “Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu”
Kwahiyo chukua nafasi hii kuomba REHEMA za MUNGU ziongezeke juu yako, kwani utazipokea ikiwa utaomba kwa kumaanisha na kwa imani..
Kutoka 20:6 “nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”.
Waebrania 4:16 “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji”
Lakini pia tunaweza kuwa watu wa Rehema kwa wanadamu wenzetu.
Kama MUNGU anavyoturehemu tunapomwomba, ni lazima na sisi tuwe watu wa kurehemu wengine,
Mathayo 8:32 “Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; 33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?”.
Mathayo 8:32 “Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi;
33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?”.
Faida ya kuwa watu wa rehema kwa wenzetu, ni sisi pia kurehemiwa na MUNGU..
Kwahiyo chukua nafasi hii kuomba MUNGU akakuongezee Rehema ndani yako kwa wengine.
2. OMBI LA AMANI. (Tumia dk. 45)
Ipo amani ya MUNGU na amani ya ulimwengu.
Yohana 14:27 “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga”.
Maandiko yanasema pasipo upendo sisi sio kitu, katika Sehemu ya pili ya darasa letu hili la Neno na Maombi tulijifunza mwongo sahihi wa kuombea Upendo..Kwahiyo fungua link ifuatayo kupata mwongozo huo.
NENO NA MAOMBI~ Sehemu ya 2 (AMRI YA UPENDO)
Usikose sehemu ya tano (05) ya darasa letu hili la Neno na Maombi.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
NENO NA MAOMBI~ Sehemu ya 1 (MAPENZI YA MUNGU)
NENO NA MAOMBI~ Sehemu ya 3 (UTAKASO WA KINYWA)
FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU
MWONGOZO WA MAOMBI YA ASUBUHI.
2 Samweli 6:22
[22]Kisha nitakuwa hafifu zaidi, nami nitakuwa mnyonge machoni pangu mimi mwenyewe; lakini kwa wale vijakazi uliowanena, kwao nitaheshimiwa.
Pale kiongozi anapokubali kuwa dhaifu machoni pake mwenyewe ndio mwanzo wa yeye kuwa na heshima machoni pa watu wake.
Kinyume chake ni kweli pale kiongozi anapotaka kujiwekea heshima yake mwenyewe ndivyo anavyokuwa dhaifu machoni pa watu anaowaongoza.
Mke wa Daudi alidhani Daudi atadharauliwa kwa kucheza cheza na kuruka-ruka mpaka nguo kumtoka mbele za Bwana na watumishi wake. Lakini kinyume chake, kumbe ndivyo walivyompenda na kumthibitisha zaidi.
Daudi alikuwa ni kiongozi wa kiroho wa watu, sio mfalme tu wa watu, haikuwa rahisi kumtofautisha na mtu mwingine yeyote, katika bidii yake ya kumtafuta Mungu, hakukitanguliza cheo alichokuwa nacho, palipostahili kufunga sana na kuomba alifunga, palipostahili kulia alilia na kuvaa nguo za magunia, palipostahili kuimba aliimba kwa nguvu zake zote hadi nguo kumdondoka.
Alitenga mambo ya ufalme na ibada, alionyesha bidii kuwathibitishia watu kuwa yeye ni mnyonge, na mdhaifu, mbele ya macho yake mwenyewe, ndio maana mke wake akamdharau. Akasema mimi siwezi kuitwa mke wa mfalme wa namna hii, asiyejitofautisha na vijakazi wake, ambaye haeleweki kama ni mfalme au mchungaji.
Unyenyekevu aliokuwa nao, alipokuwa mchungaji wa kondoo, ndio huo huo aliendelea nao alipokuwa mchungaji wa watu. Katika namna ya kimwili alionekana dhaifu, tofauti na wafalme wengine, waliokuwa wanajivunia majeshi, Daudi alijivunua Jina la Bwana.
Halikadhalika wewe kama kiongozi wa kiroho, Je!, unaweza kuwa si kitu, kwa mambo unayoyatenda kwa Mungu wako, yanayopelekea mpaka wengine kukudharau, kwa kusema unajishusha daraja?
Bwana atusaidie.
Sauli alikuwa ni adui mkubwa sana wa Daudi, kiasi cha kumfanya maisha yake yote yawe ni mafichoni tu na ugenini kwa miaka mingi. Lakini cha ajabu ni kuwa uadui aliokuwa anauongeza kwa Daudi, uliongeza pia upendo mwingi kwa Daudi kupitia mwanawe Yonathani.
1 Samweli 19:1-2
[1]Kisha Sauli akasema na mwanawe Yonathani, tena na watumishi wake wote, kwamba wamwue Daudi. [2]Lakini huyo Yonathani, mwana wake Sauli, alikuwa akipendezwa sana na Daudi. Basi Yonathani akamwambia Daudi, akasema, Sauli, baba yangu, anatafuta kukuua; basi, nakusihi, ujiangalie sana asubuhi, ukae mahali pa siri na kujificha;
[1]Kisha Sauli akasema na mwanawe Yonathani, tena na watumishi wake wote, kwamba wamwue Daudi.
[2]Lakini huyo Yonathani, mwana wake Sauli, alikuwa akipendezwa sana na Daudi. Basi Yonathani akamwambia Daudi, akasema, Sauli, baba yangu, anatafuta kukuua; basi, nakusihi, ujiangalie sana asubuhi, ukae mahali pa siri na kujificha;
1 Samweli 20:17
[17]Naye Yonathani akamwapisha Daudi mara ya pili, kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwake; kwa maana alimpenda kama alivyoipenda roho yake mwenyewe.
Upendo ambao Daudi mwenyewe baadaye anashuhudia ulizidi upendo wa mwanamke..
2 Samweli 1:26
[26]Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu, Ulikuwa ukinipendeza sana; Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, Kupita upendo wa wanawake.
[26]Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu, Ulikuwa ukinipendeza sana;
Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, Kupita upendo wa wanawake.
Naam, Familia moja inatoa uadui uliozidi na wakati huo huo inatoa upendo usio na kifani.
Na hatimaye upendo ukazidi nguvu uadui wote..
Popote unapojikuta hupendwi, unapigwa vita, unatendewa mabaya, unaonewa wivu, bila sababu yoyote, fahamu kuwa hapo pia pana upendo mwingi sana nyuma yake uliojificha.
Kwanini pengine huuoni?
Ni kwasababu unashindana na maadui zako badala ya kuwaombea mema. Mwangalie Daudi hakudhubutu kushindana na bosi wake, ijapokuwa alijua anawindwa naye ili auawe, hata yule mtu aliyejifanya amemuua mfalme, Daudi hakufurahishwa naye, kinyume chake alimwua huyo, hata alipothibitisha kifo mfalme Daudi hakucheka bali aliomboleza na kulia.
Hatimaye Mungu akampa zawadi ya upendo kupitia mtoto wa huyo huyo adui yake, ndiye Yonathani.
Hii ndio sababu kwanini Bwana Yesu anasema wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi. Kwasababu ndani yao pia upo upendo mwingi sana usiouona.
Mathayo 5:43-44
[43]Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; [44]lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
Ikiwa ni boss wako, anakupiga vita mwombee kwa kuugua kabisa, sio kinafki mnyororo ulio nyuma yake utakupenda kwa upendo mkuu, unaorudisha kwake.
Mungu anapenda, tuitafute amani kwa bidii zote(Waebrania 12:14). Je! Unamwona adui yako kwa jicho lipi?
Shalom.
Mwanzoni nilidhani kilchowafanya mitume washindwe kumtoa yule Pepo ambaye alimvaa yule kijana, na kumtupa majini, ni uwezo wa pepo yule. Kwamba alihitaji kiwango cha juu zaidi cha kiroho ili kumshinda ambacho hicho kinakuja katika mifungo na maombi mengi kama Bwana Yesu alivyosema.
Marko 9:28-29
[28]Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa? [29]Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba.
[28]Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
[29]Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba.
Lakini uhalisia ni kwamba sio kuwa pepo lile lilikuwa na nguvu nyingi za ukinzani. Bali lilikuwa ni sawa tu na mapepo mengine ambayo walishawahi kukutana nayo huko nyuma, na huwenda hata yale yalikuwa ni yenye nguvu zaidi ya hili, lakini waliyatoa yote, na hapa wameshindwa…walijiuliza sana, mpaka wakaenda kumuuliza Yesu.
Ndipo Yesu akawaambia namna hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa kuomba.
Hapo anaposema isipokuwa kwa kuomba, hamaanishi kuwa kiwango chao cha maombi kipo chini, lakini hasaa analenga “Utegemezi” wao kwa Mungu umeshuka.
Ikumbukwe kuwa wakati mfupi nyuma, Yeye alikuwa mlimani siku tatu, uwepo mwa Mungu, usiku na mchana anamtafakari Mungu lakini ni wanafunzi tu watatu walioongozana naye, ambao ni Petro, Yohana na Yakobo. Wengine wote waliosalia hawakuwepo, wapo bize na huduma, muda wa utulivu na Mungu hawana, muda wa kudumu magotini kujinyenyekeza kwa Mungu umefinywa .
Hawakujua kuwa utegemezi wao wa jana sio sawa na wa leo, ndio hapo wakashindwa kutoa pepo.
Hivyo wakajifunza, kuwa pamoja na huduma lakini pia kuwepo uweponi mwa Bwana kimaombi ni muhimu vinginevyo tutashindwa kutatua matatizo mengi ya kihuduma.
Nasi tujue nguvu za jana, haziwezi kuwa za leo, ikiwa hatatuendeleza utegemezi wetu kwa Mungu.
Inawezekana kabisa ukaitatua hiyo changamoto leo kwa ushindi wote, lakini kesho ikakushinda, ukapona leo, lakini kesho ugonjwa ukakurudia..
Ukatoa pepo leo lakini kesho ukashindwa, angalia utegemezi wako umeyumba kiasi gani..
Kisha rudisha ile namna yako ya ukaribu na Mungu, pata muda wa utulivu mwingi, kutafakari Neno, kuomba, kufunga, kuimba na kuabudu, na kuisikia sauti ya Mungu, hiyo yote ndio inaitwa kuomba…fanya hivyo mara kwa mara..hatimaye kile kilichokuwa kionanekana kama ni changamoto kinatatulika tena.
Tatizo sio nguvu, tatizo ni kiwango cha utegemezi wako. Kwasababu nguvu tayari zipo hazijatengenezewa njia ya kutoka.
Shalom
Mtu anapookoka, vitu viwili huwa vinaanza kukua ndani yake kwa pamoja cha kwanza ni Karama, na cha pili Roho.
Lakini la kutilia maanani, ni asili ya ukuaji wao, kwasababu karama huwa inatabia ya kukua kwa haraka sana kuliko roho ya mtu.
Karama inaweza ikakua ndani ya mda mfupi sana, baada ya kuokoka, na isiwe na maandalizi mengi, Kwamfano mtu anaweza akawa amepewa karama ya unabii, karama ya uponyaji, karama ya lugha na fasiri za lugha, karama ya miujiza na vikaanza kufanya kazi kwa nguvu sana,. Sasa mahali pa kuwa makini sana ni hapo, kwasababu pale inapoonekana karama wengi hudhani ndio ishara ya ukuaji wa kiroho.
Na pengine huyu mtu anaweza kujiona amepiga hatua kubwa sana, kumbe sio. Ukuaji wa kiroho ni hatua ya taratibu sana, inayochukua safari ya muda mrefu hata miaka. Na ndivyo ambavyo Mungu amekusudia.
Haijalishi utawahi kuelewa maandiko, karama yako itatenda kazi kwa ukubwa kiasi gani, bado Mungu humtengeneza mtu taratibu, kama tu vile mwili wake unavyokuwa taratibu. Ilimchukua Musa miaka arobaini (40), kuwa mchungaji wa Israeli aliyeaminiwa na Mungu, ilimchukua Paulo miaka kumi na nne (14) mpaka awe mtume wa kiMataifa, ilimchukua Bwana Yesu miaka thelathini (30), mpaka awe mwokozi.
Sio kwamba muda wa hapo katikati walikuwa ni wazembe sana, hawamchi Mungu, ndio maana muda ukapita mrefu hakionekani chochote kilichofanyika hapana, bali matengenezo ya mwanadamu yafanywayo na Mungu huwa yanaenda kwa hatua nyingi ambazo humchukua muda, ijapokuwa sisi tutayataka yawe kufumba na kufumbua, lakini kwa Mungu sivyo.
Je! Ni madarasa yapi ambayo mtu anapitia hapo katikati?
Nyakati za ukimya wa Mungu: Hapa Mungu anamwandaa mtu katika ukimya wake, si rahisi kusikia chochote, kuona chochote, kama ilivyokuwa mwanzo, lakini haimaanishi kuwa Mungu hayupo na mtu huyo, bali anajengewa ndani yake saburi na Imani. Usiishi tena kwa hisia au misisimko bali kwa Imani katika ahadi za Mungu. Jambo hili linaweza kumchukua mamiezi hata miaka.
Nyakati za mafunzo: Hapa Mungu anamweka chini ya waalimu, kumfundisha, ni wakati wa kulishwa Neno, na kupokea maarifa mengi, na uzoefu wa kiroho, kwa waliomtangulia. Kama Kristo alivyokaa chini ya waalimu akiwasilikiliza, akiwatazama, na kuwauliza maswali (Luka 2:46). Vivyo hivyo huyu naye ni lazima tu atapitishwa chini ya watu kumfundisha, na akikwepa darasa hili, hatoona maendeleo yoyote ndani yake.
Nyakati hizi, huambatana na kusikiliza mahubiri, kusoma vitabu, kuwauliza maswali, kuhudhuria semina na vipindi vingi vya mafundisho.
Nyakati za utulivu na kutengwa: Hizi ni nyakati ambazo Mungu atakutenga mbali na ulimwengu, au kukupunguzia mahangaiko, ili upate muda mwingi wa kuomba na kufunga na kujisomea Neno peke yako. Nyakati hizi wengine hata watafute kazi vipi hawapati, ukiona hivyo tumia muda huo kumkaribia Bwana, kwasababu Mungu anakufundisha kujenga mahusiano yako binafsi na yeye. Ili uielewe sauti ya Mungu.
Nyakati za Kunyenyekezwa: Hapa Mungu atakuacha uwe kwenye uhitaji/ utegemezi fulani, atamwagiza kunguru (ndege mchafu), akuhudumie kama ilivyokuwa kwa Eliya, sio kwamba ameshindwa kukuletea mtu mwema, au kukupa tu yeye mwenyewe, hapana, anaweza mtumia yule usiyempenda, usiyemtarajia kukuhudumia eneo fulani, lengo akufundishe unyenyekevu wake, na upendo usio na sharti. Ikiwa mtu atakwepa darasa hili, anaukwepa unyenyekevu wa Mungu.
Nyakati za Majaribio: Ibrahimu alipitishwa kwenye majaribio, lengo sio kuangamizwa, bali kuhakikiwa imani yake, , ijapokuwa Ibrahimu alishinda katika mengi ikiwemo kumtoa mwanawe sadaka, lakini alishindwa kwa kusikiliza sauti ya mkewe Sara akazaa na kijakazi wake. Ni kuonyesha kuwa lile utakaloshindwa lisiwe sababu ya wewe kudhani kuwa Mungu amekutupa, lengo, jirekebishe, jifunze kutokana na makosa, ili uwe mkamilifu. Ibrahimu aliposhindwa kwa Sara Mungu alimwambia uwe mkamilifu mbele zangu (Mwanzo 17:1). Kipindi hichi ni kufanywa mkamilifu.
Nyakati za huduma: Hapa Bwana atakujaribu kwa lililo dogo, atakuweka katika utumishi wake, uwahudumie wengine, hapa anapima uaminifu wako. Je! Utatenda kwa uaminifu? Ndicho alichokifanya kwa mitume wake (Mathayo 10), alipowatuma wawili wawili, kabla ya huduma kamili kuja juu yao siku ya pentekoste.
Wito kamili: Hapa Mungu amekuhakiki na kukuthibitisha, kuwa chombo chake kiteule. Ndipo anapokutumia jinsi apendavyo, yawe kwa makubwa au madogo, Hapa ni rahisi kuona mema mengi sana ya Mungu, katika maeneo mbalimbali ya rohoni.
La kufahamu tu, hatua hizi zinaweza kuingiliana, yaani ukapitishwa tatu, au nne, kwa wakati mmoja, na huweza jirudia rudia, mzunguko ukawa huo huo kwa kipindi kirefu.
Lakini mwisho wa mnyororo huo , utaona mwisho wa madarasa hayo Umefundishwa;
Saburi, Imani, maarifa, Kiasi Uaminifu, ukamilifu (utauwa), upendo
Ambavyo vinaenda sambamba kabisa na lile Mtume Petro aliloliandika kwa uweza wa Roho katika..
( 2Petro 1:5-11)
5 Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, 6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, 7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo. 8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo. 9 Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani. 10 Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. 11 Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Hivyo ikiwa umemwamini kweli Kristo, na kumfuata, basi fahamu kuwa lengo kubwa na Mungu ni wewe ufikie ukuaji bora wa kiroho, jitahidi kutembea kikamilifu kwenye madarasa yake ambayo huchukua muda, lakini mwisho wake ni TAJI LA UZIMA lisilonyauka, kwa kufuzu madarasa ya Mungu.
Mungu akubariki.
Usingizi, unapopita kiasi, hutuletea hasara, na umaskini, biblia imeliweka wazi hilo (Mithali 6:9-11), na sio usingizi tu, bali mambo yote yanayoonekana mazuri kama vile chakula, tendo la ndoa kwa wanandoa, yakikosa kiasi huleta uharibifu, Lakini usingizi kama usingizi, sio jambo baya, endapo tutaliona kiroho.
Mungu alipomleta Mwanamke duniani, alitumia njia ya usingizi, kama kanuni ya kumtoa kwa mwanamume, ingewezekana kabisa Mungu kumchukua Adamu kwenye maono kama alivyomchukua Yohana kule Patmo, kisha amuumbe Hawa kwa njia hiyo, au angemwacha macho, ashuhudie kazi yote ya upasuaji inavyofanyika, lakini hilo hakulichagua bali alitumia usingizi.
Robo ya maisha yako, unakuwa usingizini, hivyo huo muda, sio kwamba hakuna chochote kinachoendelea, au muda wako unapotea kama wengi wanavyodhani.
Watafiti wa kisayansi wanasema mtu anapokea taarifa katika ubongo, anapokuwa macho, lakini pale anapolala, taarifa zile ndipo zinapokusanywa, na kuhifadhiwa. Sasa huo ni utafiti wao, ambao tunajua kwa sehemu una uhalisia, lakini sisi wa rohoni tunaona zaidi ya mwilini.
Usipojua kuuandaa usingizi wako vema, basi unaweza kuzuia kazi za Mungu kutimilika vizuri tulalapo, kama tu vile tunavyoweza kuzuia kazi za Mungu anazotenda ndani yetu wakati wa mchana, tusipofuata kanuni zake.
Ukiona mara nyingi usingizi wako unavurugika, hulali, wakati mwingi unataabika usiku, unaota tu ndoto mbaya kila siku, magonjwa ya usiku yasiyokoma, fahamu kuwa pia hali yako ya kiroho inadhoofika.
Ni nini Mungu hufanya usiku?
Ili mojawapo ya huduma hizi, au zote, zitimie ndani yetu, basi jifunze kufanya yafuatayo.
Siku zote omba, kabla ya kulala, Kwa kufuata mpangilio huu.
Sema, Bwana Yesu, yote uliyonifundisha kutwa nzima ninaomba usiku wa leo, yazamishe kwenye vyumba vya ndani vya moyo wangu, nisiyasahau.
Bwana Yesu lile agizo kuu, ulilosema nami kutwa nzima, au siku zangu za nyuma, lithibitishe tena kwa kupitia njozi zangu.
Bwana Yesu nijuze yote kuhusiana na mambo ya kesho na yale yanayokuja mbeleni kupitia njozi zangu.
Bwana ninakwenda kinyume ni mashambulizi yote ya usiku yatokayo kwa yule mwovu, ndoto za kipepo, magonjwa, na madhaifu ninavifuta kwa jina la Yesu Kristo. Amen
Sikuzote ona usiku wako, ni sehemu ya huduma. Jipe muda wa kupumzika, huku umeuandaa kwa maombi mazuri.
WhatsApp
Je mtu anaweza kuwa “roho moja na Mungu”?.. jibu ni ndio!.
1Wakorintho 6:17 “Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye”.
Sasa ni kwa namna gani mtu anakuwa roho moja na Mungu?..
Jibu: Ni kwa namna ile ile ambavyo mtu anaweza kuwa mwili mmoja na mwenzake..
Marko 10:7 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; 8 NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA; HATA WAMEKUWA SI WAWILI TENA, BALI MWILI MMOJA”.
Marko 10:7 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
8 NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA; HATA WAMEKUWA SI WAWILI TENA, BALI MWILI MMOJA”.
Kama mwanaume na mwanamke wanavyokuwa mwili mmoja baada ya ndoa, nasi tunakuwa roho moja na MUNGU baada ya kuokoka kikweli kweli.
Kwanini hatuwi mwili mmoja na MUNGU na badala yake tunakuwa Roho moja naye?..
Ni kwasababu MUNGU ni ROHO (soma Yohana 4:24), na kwakuwa nasi (wanadamu) pia tunazo roho basi tunapomgeukia MUNGU tunaunganishwa naye na kuwa roho moja naye.
Na tunapokuwa roho moja naye maana yake sisi na yeye tunafanana?.. na mfanano wa kwanza ni “usafi na utakatifu”.. Kama Mungu alivyo mtakatifu nasi tutakuwa watakatifu kama yeye.
Mambo ya Walawi 20:26 “Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi Bwana ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu”.
Ukiona bado uasherati upo ndani yako basi ni dhahiri kuwa bado haujaungwa na Bwana, ukiona wizi upo ndani yako basi ni dhahiri kuwa bado haujaungwa na Bwana kwasababu MUNGU sio mwizi..na ukiona mambo yote yaliyotajwa katika kitabu cha Wagalatia 5:19-20 bado yapo ndani yako maana yake bado haujaungwa na Bwana.
Pia aliyeungwa na Bwana atafikiri daima habari za kuwavuta watu kwa MUNGU (yaani injili), kwasababu MUNGU naye anasikitishwa na maovu na anataka watu wote watubu, kadhalika na mtu aliyeungwa naye atakuwa na maazimio hayo hayo, kila siku atafikiri jinsi ya kuwavuta watu waiamini injili aidha kwa kuhubiri (mitaani, makanisani, mashuleni, masokoni, mitandaoni au mahali pengine popote), au kama hatasimama basi ataiwezesha injili kwa mali zake kwa kadiri awezavyo, akijua kwamba hata kama hatasimama kuhubiri basi kawezesha injili kwa mali zake.
Lakini kama bado ndani yako huoni kiu wala hamasa ya kuhubiri / kushuhudia watu waokoke au kuishika injili kwa mali zako, basi ni wazi kuwa bado haujaungwa na BWANA, kwasababu Neno la MUNGU linasema kuwa yule Roho wa MUNGU pamoja na Bibi arusi (yaani mtu aliyeokoka), kwa pamoja wanasema Njoo!.. yaani njoo upokee msamaha wa dhambi kwa kutubu na kuacha njia mbaya..
Ufunuo 22:17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.
Je kwa maandiko haya, unajiona kwamba umeungwa na MUNGU, au umeungwa na vitu vingine?
Kama unajiona kwamba umeungwa na vitu vingine na si MUNGU, habari njema ni kwamba unayo nafasi ya kujitenga na muunganiko huo haramu, na kujiunganisha na MUNGU, kwa njia ya kutubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi, na kubatizwa kwa maji mengi kwa jina la BWANA YESU KRISTO na kwa ROHO MTAKATIFU, na kuanzia hapo na kuendelea utukufu wa MUNGU utakushukia.
Bwana YESU Akubariki.
AMBATANA NA WALIO HAI ROHONI.
MISTARI YA KUOMBEA AMANI YA FAMILIA.
PONGEZI NA MAONYO YA BWANA KWA WATAKATIFU.
IMEANDIKWA NINI KATIKA TORATI? WASOMAJE?
HAPANA HATA MMOJA ATAKAYEIONJA KARAMU YANGU.
Ni maswali mengi yanaulizwa na watakatifu, mbona ninajuhudi sana, ninahudhuria vipindi vingi vya mafundisho, mifungo na maombi, semina na mikutano, na makambi makubwa ya ujazo wa Roho Mtakatifu, ninapokea nguvu, Mungu anatenda makubwa, lakini najiona moyoni bado sina ukuaji mzuri wa kiroho?
Kwanini, sababu ni nini?
Tukisoma maandiko tunaona kuna upande ambao, tunausahau kuutilia msisitizo katika kumjua Kristo, na pengine hauhubiriwi sana madhabahuni, lakini ni muhimu
Upande huo mtume Paulo aliusema katika kitabu cha Wafilipi,
Wafilipi 3:10 ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na USHIRIKA WA MATESO YAKE, nikifananishwa na kufa kwake;
Zingatia hapo, anataja mambo mawili anasema, ili nimjue yeye na uweza wa kufufuka kwake,
Lakini pia..
Na ushirika wa mateso yake.
Watu wanatazama sana, eneo la kwanza, ambalo ni uweza wa kufufuka kwake, yaani wanatafuta nguvu za Mungu kwa juhudi kubwa, miujiza, uponyaji, baraka, unabii, ujazo wa Roho Mtakatifu, jambo ambalo ni zuri sana, na linapaswa litafutwe, lakini, bado mtu huyu kwa bahati mbaya anaweza asikamilike kama hatataka na sehemu ya pili pia ya kumjua Kristo, ambayo ni ‘ushirika wa mateso yake’.
Paulo alifanya miujiza lakini alifungwa pia kwa ajili ya hiyo, aliponya watu lakini alipigwa mawe, alifanya makubwa lakini bado alitukanwa, na kufanyiwa visa.
Ukuaji mzuri wa kiroho, hautazamii tu, kupokea nguvu za Mungu, unatazama pia Ushirika wa mateso yake.
Tunataka tumjue Kristo, lakini hatutaki kuudhiwa kwa gharama tulizoingia kwa ajili yake, Yesu alisema tutapata mara mia kweli, lakini pia tutapata na udhia (Marko 10:30).
Ndege hawezi kuruka kwa bawa moja, ni lazima yote mawili yafanye kazi, Tukimtaka Mungu kwa nguvu zake, tu lakini hatumtaki na mateso yake, bado maendeleo hayatakuwa makubwa. Haijalishwi tutajazwa Roho kiasi gani.
Ushirika wa mateso ni pamoja na kukubali kuchukiwa kwa ajili ya jina lake, kutengwa kwasababu ya misimamo yako ya kiroho, kumbuka gharama ya Danieli kupendwa ni pamoja na kukubali kutupwa kwenye tundu la simba, Yusufu kuwa mkuu ni pamoja na kuuzwa na ndugu zake kwasababu ya misimamo yake, Ayubu kuitwa mcha Mungu ni pamoja na majaribu aliyoyastahimili. Huo ndio ushirika wa mateso yake.
Usifurahie tu, kuona nguvu za Mungu, jiulize binafsi ni wapi nimeshiriki mateso ya Kristo, kwa kuzikubali gharama? Palipo na gharama na umakini wa kiroho, ushirika wa mateso ni lazima utaambatana nawe.
Tukue kiroho.
Ziara ya Paulo Korintho ilikuwa ya ukinzani sana, ambapo yamkini kama sio Mungu kumthibitishia neno lake, asingeendelea kubaki kwenye mji ule, kwasababu watu wa mji ule sio tu walipingana naye waziwazi, bali biblia inasema pia walimtukana Mungu. Jambo ambalo lilikuwa gheni sana machoni pa watendakazi wa injili, (Matendo 18:1-6)
1 Baada ya mambo hayo, Paulo akatoka Athene akafika Korintho… 4 Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani.. 5 Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo. 6 Walipopingamana naye na kumtukana Mungu, akakung’uta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu; mimi ni safi; tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa.
Lakini katika moyo wa ukinzani ule, ambao alikuwa karibu kuondoka, Bado Mungu alimtokea katika maono usiku akamwambia, baki, kwa kuwa mimi nina watu wengi katika mji huu. Sio ‘watu tu’, bali ‘watu wengi’, idadi kubwa mno, umati wa watu.
Matendo 18:9-11
9 Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze, 10 kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; KWA MAANA MIMI NINA WATU WENGI KATIKA MJI HUU. 11 Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu.
Mara nyingi tunapokuwepo kwenye miji mikubwa, na kuona uzito na ugumu wa mioyo ya watu, na ubize wao, na kiburi chao ni rahisi kukata tamaa na kusema hapa Mungu hana watu tena.
Lakini kaa ukifahamu Mungu bado ana watu wake wengi nje ya kanisa, wanaopaswa waje ndani ya kanisa. Katikati ya wanaomtukana yeye, wanaopingana na wewe, kwenye mikanganyiko ya kipepo ya kila namna, Mungu bado anaona watu wengi ambao anataka waokolewe.
Badili mtazamo wako kuanzia leo, injili sio macho yetu, ni macho ya Mungu, pale tunapoona hapafai, haimaanishi kuwa hapafai machoni pa Mungu.
Endelea, tena na tena, lipo kusudi kubwa la Mungu nyuma ya mahali ulipo.
Wale wakoma wanne (4), walipofika kwenye kambi ya washami na kujiokotea utajiri kwa jinsi walivyoweza, biblia inatuonyesha baadaye dhamiri zao ziliwasuta, kwanini wanufaike wao peke yao, wakati Israeli nzima ipo kwenye janga kubwa la njaa?
Hivyo walipogundua ubinafsi wao, haraka sana bila kukawia walijirekebisha wakaenda kuwaambia wakuu wa Israeli, na baadaye watu wakaja kujikusanyia nyara kwa wingi kwa jinsi wawezavyo, na tangu huo wakati Israeli yote janga la njaa likapotea.
Watu wanne tu ambao hawakuwa wabinafsi, waliliokoa taifa zima,
2 Wafalme 7:3-11
[3]Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe? [4]Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu. [5]Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu. [6]Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi. [7]Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao. [8]Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha. [9]Ndipo wakaambiana, MAMBO HAYA TUFANYAYO SI MEMA; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme. [10]Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha. [11]Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme.
[3]Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe?
[4]Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu.
[5]Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu.
[6]Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi.
[7]Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao.
[8]Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha.
[9]Ndipo wakaambiana, MAMBO HAYA TUFANYAYO SI MEMA; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme.
[10]Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.
[11]Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme.
Hii inatoa sauti gani kwetu?
Sisi tuliookoka ni zaidi ya wanne.. Lakini kwanini injili haiwafikii wengi? Ni kwasababu haya tuyafanyayo tunaona ni vema..
Tunaona ni sawa tu tuingie rahani mwa Mungu sisi wenyewe.
Ni sawa tu tuhubiriwe peke yetu, wengine waendelee kukaa nje ya kanisa..
Ni sawa tu tujazwe Roho, wengine waendelee kukaa chini ya vifungo vya mapepo.
Hii ni sifa ya ubinafsi.
Ikiwa upo kanisa, kila siku unahubiriwa lakini wewe huwahubirii wengine ni ubinafsi,
Ikiwa unafuatilia mafundisho kama haya mitandaoni, lakini wewe hutaki kushea na wengine, ni ubinafsi.
Ikiwa umeokoka muda mrefu, halafu huna tunda la mtu yeyote kuokoka kupitia wewe, ni ubinafsi..
Kujilimbikizia mambo ya ufalme peke yako…wenzako hawakishiriki kipawa chako, Si jambo jema linalokubalika kiroho
Nenda kahubiri.