NINA WATU WENGI KATIKA HUU MJI.

NINA WATU WENGI KATIKA HUU MJI.

Ziara ya Paulo Korintho ilikuwa ya ukinzani sana, ambapo yamkini kama sio Mungu kumthibitishia neno lake, asingeendelea kubaki kwenye mji ule, kwasababu watu wa mji ule sio tu walipingana  naye waziwazi, bali biblia inasema pia walimtukana Mungu. Jambo ambalo lilikuwa gheni sana machoni pa watendakazi wa injili, (Matendo 18:1-6)

1 Baada ya mambo hayo, Paulo akatoka Athene akafika Korintho…
4 Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani..
5 Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo.
6 Walipopingamana naye na kumtukana Mungu, akakung’uta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu; mimi ni safi; tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa.

Lakini katika moyo wa ukinzani ule, ambao alikuwa karibu kuondoka, Bado Mungu alimtokea katika maono usiku akamwambia, baki, kuwa kuwa mimi nina watu wengi katika mji huu. Sio ‘watu tu’, bali ‘watu wengi’, idadi kubwa mno, umati wa watu.

Matendo 18:9-11

9 Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze,
10 kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; KWA MAANA MIMI NINA WATU WENGI KATIKA MJI HUU.
11 Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu.

Mara nyingi tunapokuwepo kwenye miji mikubwa, na kuona uzito na ugumu wa mioyo ya watu, na ubize wao, na kiburi chao ni rahisi kukata tamaa na kusema hapa Mungu hana watu tena.

Lakini kaa ukifahamu Mungu bado ana watu wake wengi nje ya kanisa, wanaopaswa waje ndani ya kanisa.  Katikati ya wanaomtukana yeye, wanaopingana na wewe, kwenye mikanganyiko ya kipepo ya kila namna, Mungu bado anaona watu wengi ambao anataka waokolewe.

Badili mtazamo wako kuanzia leo, injili sio macho yetu, ni macho ya Mungu, pale tunapoona hapafai, haimaanishi kuwa hapafai machoni pa Mungu.

Endelea, tena na tena, lipo kusudi kubwa la Mungu nyuma ya mahali ulipo.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply