Jina la Bwana na Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe.. karibu katika kujifunza Neno la MUNGU lililo taa na Mwanga wa nyia yetu (Zaburi 119:105).
Katika Ufunuo 4:6, Biblia inasema kwamba wale wenye uhai wanne walikuwa wamejaa macho mbele na nyuma.
Ufunuo 4:6 “Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma”.
Sasa ukiendelea kusoma habari hiyo utaona wale malaika (wenye uhai wanne) walikuwa na nyuso nne kila mmoja, ambapo upande mmoja walikuwa na uso wa mwanadamu, upande wa pili uso wa Simba, upande wa tatu uso wa ndama na upande wa nne na wa mwisho walikuwa na uso wa Tai.
Sasa kila uso ulikuwa na maana yake, na kila uso ulikuwa unaangalia upande wake (maana yake pande nne za nchi, kaskazini, kusini, mashariki na magharibi).. na kila uso ulikuwa na macho mawili, jumla macho nane, hiyo ndio maana ya neno hilo, (walikuwa na macho pande zote).
Sasa umuhimu wa yale macho ni nini?.
Umuhimu wake ni kwamba hawakuwa na haja ya kugeuka nyuma wanapotaka kubadilisha mwelekeo kwani hawakuwa na kisogo, waliona pande zote hata wewe ungekuwa na macho nyuma ya kisogo chako usingekuwa na sababu za kugeuka nyuma ungekuwa unarudi tu nyuma kwani macho yako yanaona pia nyuma, na hawa wenye uhai wane walikuwa hivo hivyo, hawakuwa na haja ya kurudi nyuma.
Lakini pia faida nyingine ya macho ya nyuma au pande zote (hususani kwetu sisi wanadamu) ni kujikinga na hatari, siku zote adui ana tabia ya kuvizia na hawezi kumvizia mtu kwa mbele bali huwa anamvizia kwa nyuma kwasababu haoni, ili tuliweke hili vizuri uweze kuelewa tutafakari pamoja habari hii ifuatayo.
Katika maeneo baadhi ya nchi za India na Bangladesh, kuna aina ya wanyama jamii ya paka wakubwa, wajulikanao kama simba-mbarara au Tiger, wanyama hawa wana nguvu zinazokaribiana na simba au hata kuwazidi kidogo, na wanaishi katika misitu..
Sasa tabia ya paka hawa ni kuvizia kwa nyuma, maana yake wakimwona mtu wanasubiri apite na akishatoa mgongo basi wanashambulia kutoka nyuma, sasa jamii ya wanavijiji wakabuni mbinu ya kukabiliana na wanyama hawa ili wasiwadhuru, na wakagundua kuwa wanapenda mgongo na wanaogopa macho, hivyo walichokifanya ni kutengeneza vinyago vyenye sura ya mtu na kutembea navyo wakiwa wamejifunga nyuma ya kisogo, na hivyo chui hao wanapowakaribia na kuona kama wanatazamwa kwa nyuma huwa hawashambulii na hivyo mtu anabaki salama.
Mbuni hii pia inatumika katika ulimwengu wa roho kuzuia mashambulizi ya kiroho, adui yetu ibilisi ni kama simba ambaye anazunguka huku na huko akitafuta mtu ammeze, hivyo ni lazima tuwe na macho ya mbele na nyuma katika roho.
Macho ni silaha kubwa sana ya kumshinda adui, hata wezi hawaibi mtu akiwa macho, bali wanasubiri wakati ambapo macho yamefumbwa na adui hawezi kufanya uharibifu wakati mtu akiwa macho, hawezi kupanda magugu katika maisha ya mtu akiwa macho (Mathayo 13:25).
Hivyo ni lazima tuwe na jicho la TAI (linaloona mbali mambo yajayo ikiwemo uzima wa milele na hukumu ya MUNGU), na jicho la Tai tunalipata kwa njia ya maombi na kusoma Neno la MUNGU.
Pia ni lazima tuwe na macho ya Simba, kama wale wenye uhai wan ne (jicho la simba ni jicho la ujasiri na nguvu) na sisi ni lazima tuwe majasiri katika imani na tuwe na nguvu za Roho Mtakatifu katika maisha yetu.
Pia ni lazima tuwe na macho ya ndama, kama wale wenye uhai wane (jicho la ndama ni jicho la unyenyekevu na linaloona mahali pabichi penye nyasi)..nasi ni lazima tuwe na unyenyekevu maishani mwetu ili turuhusu Neema ya MUNGU itende kazi, pia ni lazima tupaone mahali pabichi, yaani penye malisho ya kweli ya Neno la MUNGU lisiloghoshiwa.
Na mwisho ni lazma tuwe na jicho la Mwanadamu kama wenye uhai wanne (Jicho la mtu limejaa hekima na utambuzi).
Macho yote haya ya pande zote tukiyapata basi adui hatatushinda wala kutuvamia bali sisi ndio tutakaomshinda, hivyo usikwepe maombi ndugu wala mifungo wala kusoma NENO, mambo haya ndiyo yanayoimarisha macho yetu ya kiroho na kutufanya kuwa washindi siku zote.
Bwana YESU atusaidie.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ