Je mtu anaweza kuwa “roho moja na Mungu”?.. jibu ni ndio!.
1Wakorintho 6:17 “Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye”.
Sasa ni kwa namna gani mtu anakuwa roho moja na Mungu?..
Jibu: Ni kwa namna ile ile ambavyo mtu anaweza kuwa mwili mmoja na mwenzake..
Marko 10:7 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; 8 NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA; HATA WAMEKUWA SI WAWILI TENA, BALI MWILI MMOJA”.
Marko 10:7 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
8 NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA; HATA WAMEKUWA SI WAWILI TENA, BALI MWILI MMOJA”.
Kama mwanaume na mwanamke wanavyokuwa mwili mmoja baada ya ndoa, nasi tunakuwa roho moja na MUNGU baada ya kuokoka kikweli kweli.
Kwanini hatuwi mwili mmoja na MUNGU na badala yake tunakuwa Roho moja naye?..
Ni kwasababu MUNGU ni ROHO (soma Yohana 4:24), na kwakuwa nasi( wanadamu) pia tunazo roho basi tunapomgeukia MUNGU tunaunganishwa naye na kuwa roho moja naye.
Na tunapokuwa roho moja naye maana yake sisi na yeye tunafanana?.. na mfanano wa kwanza ni “usafi na utakatifu”.. Kama Mungu alivyo mtakatifu nasi tutakuwa watakatifu kama yeye.
Mambo ya Walawi 20:26 “Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi Bwana ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu”.
Ukiona bado uasherati upo ndani yako basi ni dhahiri kuwa bado haujaungwa na Bwana, ukiona wizi upo ndani yako basi ni dhahiri kuwa bado haujaungwa na Bwana kwasababu MUNGU sio mwizi..na ukiona mambo yote yaliyotajwa katika kitabu cha Wagalatia 5:19-20 bado yapo ndani yako maana yake bado haujaungwa na Bwana.
Pia aliyeungwa na Bwana atafikiri daima habari za kuwavuta watu kwa MUNGU (yaani injili), kwasababu MUNGU naye anasikitishwa na maovu na anataka watu wote watubu, kadhalika na mtu aliyeungwa naye atakuwa na maazimio hayo hayo, kila siku atafikiri jinsi ya kuwavuta watu waiamini injili aidha kwa kuhubiri (mitaani, makanisani, mashuleni, masokono, mitandaoni au mahali pengine popote), au kama hatasimama basi ataiwezesha injili kwa mali zake kwa kadiri awezavyo, akijua kwamba hata kama hatasimama kuhubiri basi kawezesha injili kwa mali zake.
Lakini kama bado ndani yako huoni kiu wala hamasa ya kuhubiri/ kushuhudia watu waokoke au kuishika injili kwa mali zako, basi ni wazi kuwa bado haujaungwa na BWANA, kwasababu Neno la MUNGU linasema kuwa yule Roho wa MUNGU pamoja na Bibi arusi (yaani mtu aliyeokoka), kwa pamoja wanasema Njoo!.. yaani njoo upokee msamaha wa dhambi kwa kutubu na kuacha njia mbaya..
Ufunuo 22:17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.
Je kwa maandiko haya, unajiona kwamba umeungwa na MUNGU, au umeungwa na vitu vingine?
Kama unajiona kwamba umeungwa na vitu vingine na si MUNGU, habari njema ni kwamba unayo nafasi ya kujitenga na muunganiko huo haramu, na kujiunganisha na MUNGU, kwa njia ya kutubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi, na kubatizwa kwa maji mengi kwa jina la BWANA YESU KRISTO na kwa ROHO MTAKATIFU, na kuanzia hapo na kuendelea utukufu wa MUNGU utakushukia.
Bwana YESU Akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
AMBATANA NA WALIO HAI ROHONI.
MISTARI YA KUOMBEA AMANI YA FAMILIA.
PONGEZI NA MAONYO YA BWANA KWA WATAKATIFU.
IMEANDIKWA NINI KATIKA TORATI? WASOMAJE?
HAPANA HATA MMOJA ATAKAYEIONJA KARAMU YANGU.
Ni maswali mengi yanaulizwa na watakatifu, mbona ninajuhudi sana, ninahudhuria vipindi vingi vya mafundisho, mifungo na maombi, semina na mikutano, na makambi makubwa ya ujazo wa Roho Mtakatifu, ninapokea nguvu, Mungu anatenda makubwa, lakini najiona moyoni bado sina ukuaji mzuri wa kiroho?
Kwanini, sababu ni nini?
Tukisoma maandiko tunaona kuna upande ambao, tunausahau kuutilia msisitizo katika kumjua Kristo, na pengine hauhubiriwi sana madhabahuni, lakini ni muhimu
Upande huo mtume Paulo aliusema katika kitabu cha Wafilipi,
Wafilipi 3:10 ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na USHIRIKA WA MATESO YAKE, nikifananishwa na kufa kwake;
Zingatia hapo, anataja mambo mawili anasema, ili nimjue yeye na uweza wa kufufuka kwake,
Lakini pia..
Na ushirika wa mateso yake.
Watu wanatazama sana, eneo la kwanza, ambalo ni uweza wa kufufuka kwake, yaani wanatafuta nguvu za Mungu kwa juhudi kubwa, miujiza, uponyaji, baraka, unabii, ujazo wa Roho Mtakatifu, jambo ambalo ni zuri sana, na linapaswa litafutwe, lakini, bado mtu huyu kwa bahati mbaya anaweza asikamilike kama hatataka na sehemu ya pili pia ya kumjua Kristo, ambayo ni ‘ushirika wa mateso yake’.
Paulo alifanya miujiza lakini alifungwa pia kwa ajili ya hiyo, aliponya watu lakini alipigwa mawe, alifanya makubwa lakini bado alitukanwa, na kufanyiwa visa.
Ukuaji mzuri wa kiroho, hautazamii tu, kupokea nguvu za Mungu, unatazama pia Ushirika wa mateso yake.
Tunataka tumjue Kristo, lakini hatutaki kuudhiwa kwa gharama tulizoingia kwa ajili yake, Yesu alisema tutapata mara mia kweli, lakini pia tutapata na udhia (Marko 10:30).
Ndege hawezi kuruka kwa bawa moja, ni lazima yote mawili yafanye kazi, Tukimtaka Mungu kwa nguvu zake, tu lakini hatumtaki na mateso yake, bado maendeleo hayatakuwa makubwa. Haijalishwi tutajazwa Roho kiasi gani.
Ushirika wa mateso ni pamoja na kukubali kuchukiwa kwa ajili ya jina lake, kutengwa kwasababu ya misimamo yako ya kiroho, kumbuka gharama ya Danieli kupendwa ni pamoja na kukubali kutupwa kwenye tundu la simba, Yusufu kuwa mkuu ni pamoja na kuuzwa na ndugu zake kwasababu ya misimamo yake, Ayubu kuitwa mcha Mungu ni pamoja na majaribu aliyoyastahimili. Huo ndio ushirika wa mateso yake.
Usifurahie tu, kuona nguvu za Mungu, jiulize binafsi ni wapi nimeshiriki mateso ya Kristo, kwa kuzikubali gharama? Palipo na gharama na umakini wa kiroho, ushirika wa mateso ni lazima utaambatana nawe.
Tukue kiroho.
Shalom.
Ziara ya Paulo Korintho ilikuwa ya ukinzani sana, ambapo yamkini kama sio Mungu kumthibitishia neno lake, asingeendelea kubaki kwenye mji ule, kwasababu watu wa mji ule sio tu walipingana naye waziwazi, bali biblia inasema pia walimtukana Mungu. Jambo ambalo lilikuwa gheni sana machoni pa watendakazi wa injili, (Matendo 18:1-6)
1 Baada ya mambo hayo, Paulo akatoka Athene akafika Korintho… 4 Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani.. 5 Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo. 6 Walipopingamana naye na kumtukana Mungu, akakung’uta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu; mimi ni safi; tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa.
Lakini katika moyo wa ukinzani ule, ambao alikuwa karibu kuondoka, Bado Mungu alimtokea katika maono usiku akamwambia, baki, kuwa kuwa mimi nina watu wengi katika mji huu. Sio ‘watu tu’, bali ‘watu wengi’, idadi kubwa mno, umati wa watu.
Matendo 18:9-11
9 Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze, 10 kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; KWA MAANA MIMI NINA WATU WENGI KATIKA MJI HUU. 11 Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu.
Mara nyingi tunapokuwepo kwenye miji mikubwa, na kuona uzito na ugumu wa mioyo ya watu, na ubize wao, na kiburi chao ni rahisi kukata tamaa na kusema hapa Mungu hana watu tena.
Lakini kaa ukifahamu Mungu bado ana watu wake wengi nje ya kanisa, wanaopaswa waje ndani ya kanisa. Katikati ya wanaomtukana yeye, wanaopingana na wewe, kwenye mikanganyiko ya kipepo ya kila namna, Mungu bado anaona watu wengi ambao anataka waokolewe.
Badili mtazamo wako kuanzia leo, injili sio macho yetu, ni macho ya Mungu, pale tunapoona hapafai, haimaanishi kuwa hapafai machoni pa Mungu.
Endelea, tena na tena, lipo kusudi kubwa la Mungu nyuma ya mahali ulipo.
Wale wakoma wanne (4), walipofika kwenye kambi ya washami na kujiokotea utajiri kwa jinsi walivyoweza, biblia inatuonyesha baadaye dhamiri zao ziliwasuta, kwanini wanufaike wao peke yao, wakati Israeli nzima ipo kwenye janga kubwa la njaa?
Hivyo walipogundua ubinafsi wao, haraka sana bila kukawia walijirekebisha wakaenda kuwaambia wakuu wa Israeli, na baadaye watu wakaja kujikusanyia nyara kwa wingi kwa jinsi wawezavyo, na tangu huo wakati Israeli yote janga la njaa likapotea.
Watu wanne tu ambao hawakuwa wabinafsi, waliliokoa taifa zima,
2 Wafalme 7:3-11
[3]Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe? [4]Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu. [5]Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu. [6]Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi. [7]Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao. [8]Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha. [9]Ndipo wakaambiana, MAMBO HAYA TUFANYAYO SI MEMA; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme. [10]Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha. [11]Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme.
[3]Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe?
[4]Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu.
[5]Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu.
[6]Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi.
[7]Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao.
[8]Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha.
[9]Ndipo wakaambiana, MAMBO HAYA TUFANYAYO SI MEMA; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme.
[10]Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.
[11]Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme.
Hii inatoa sauti gani kwetu?
Sisi tuliookoka ni zaidi ya wanne.. Lakini kwanini injili haiwafikii wengi? Ni kwasababu haya tuyafanyayo tunaona ni vema..
Tunaona ni sawa tu tuingie rahani mwa Mungu sisi wenyewe.
Ni sawa tu tuhubiriwe peke yetu, wengine waendelee kukaa nje ya kanisa..
Ni sawa tu tujazwe Roho, wengine waendelee kukaa chini ya vifungo vya mapepo.
Hii ni sifa ya ubinafsi.
Ikiwa upo kanisa, kila siku unahubiriwa lakini wewe huwahubirii wengine ni ubinafsi,
Ikiwa unafuatilia mafundisho kama haya mitandaoni, lakini wewe hutaki kushea na wengine, ni ubinafsi.
Ikiwa umeokoka muda mrefu, halafu huna tunda la mtu yeyote kuokoka kupitia wewe, ni ubinafsi..
Kujilimbikizia mambo ya ufalme peke yako…wenzako hawakishiriki kipawa chako, Si jambo jema linalokubalika kiroho
Nenda kahubiri.
Utauliza je “tumbo” linaweza kuwa “mungu”? jibu ni Ndio, maandiko yanasema hivo..
Wafilipi 3:19 “mwisho wao ni uharibifu, MUNGU WAO NI TUMBO, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani”.
Na kama tumbo ni mungu, basi maana yake anaabudiwa na pia anatumikiwa.
Yafuatayo ni makundi mawili makuu ya watu wanaoabudu tumbo, aidha kwa kujua au kwa kutokujua.
1. Manabii wa Uongo.
Hili ndilo kundi la kwanza linaloabudu “tumbo” (kwa kujua kabisa).. Hawa wapo tayari kupotosha maandiko ili tu wapate kushibisha matumbo yao, wapo tayari kuzunguka kote kote kuwalaghai watu kiroho ili wapate fedha kutoka kwao.
Hawa biblia imewataja kwamba hawamtumikii Bwana YESU bali matumbo yao wenyewe..
Warumi 16:18 “Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, BALI MATUMBO YAO WENYEWE; NA KWA MANENO LAINI NA YA KUJIPENDEKEZA WAIDANGANYA MIOYO YA WATU WANYOFU”.
Kundi hili la watu, chochote kile kilichoandikwa kwenye biblia kwao ni fursa ya kupata pesa..wapo tayari kutumia chochote kile na kukupatanisha na biblia lengo si kujenga roho za watu bali kutoa pesa kutoka kwa watu, wanaweza kutumia picha, nguo, maji, mafuta na viungo vingine vyote ili mradi tu kuvuna mali kutoka kwa watu, ili washibishe matumbo yao.
Hawa madhabahu zao ni matumbo yao, shetani ameketi katika matumbo yao..na hawawezi kuishi bila kuyatumikia matumbo. Hawa biblia imetuonya tujihadhari nao, kwani kukuua kiroho wenyewe hawaoni shida.
2. Wakristo vuguvugu.
Hili ni kundi la pili la waabudu matumbo.. Hawa ni wale ambao hawawezi kuitawala miili yao katika eneo la kula, ni wale watu ambao maisha yao hawajawahi kufunga, au kama walifunga basi hawakumbuki ni lini kwasababu ni zamani sana walifanya hivo.
Ni wakristo wa kupenda kuombewa tu, hawawezi wenyewe kutenga muda kufunga na kuomba.. kwani wakijaribu kufanya hivyo wanaona kama wanakufa “roho inawatoka”.. Wanalisha matumbo yao mara tatu kwa siku, mwaka mzima, na wakikosa chakula kidogo tu ni watu wa kunung’unika, kulalamika na kuhisi kama wameonewa sana.
Hawa ni watu wanaoabudu tumbo pasipo kujua. Wakidhani kwamba kwasababu tumeruhusiwa kula, basi kila wakati ni lazima kula, pasipo kufahamu kwamba Bwana YESU alisema mambo mengine hayatoki (yani hayawezekani) pasipo kufunga na kusali.
Mathayo 17:21 “[Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]”
Hili ni kundi la watu linalopenda karamu za ulafu za kula kula…kukitokea hafla fulani, au pati, au sherehe au harusi huwa halikosi!.. linaweza kuchangia kila aina ya gharama ilimradi tu lisipitwe na shughuli, lengo kubwa ni chakula.
Mpendwa kama huwezi kulitawala tumbo, fahamu kuwa tumbo lako ni mungu wako hata kama hukiri hivyo!
Roho Mtakatifu aliwahi kunifundisha jambo kuhusu tumbo…
“Wakati fulani nilikuwa katika mfungo, na siku niliyopanga kumaliza, Roho mtakatifu aliniambia niongeze siku nyingine moja mbele, wakati nawaza hilo kama vile najiuliza uliza, kutokana na uchovu wa mwili, akaniambia toka nje tembea na nitapata nguvu, nikatii na kutoka nje na kutembea na nilipokuwa natembea mwili ulianza kupata nguvu, na nikasikia tafakari nyingi za kimaandiko zikipita ndani yangu, wakati naendelea na matembezi nilifika mtaa mwingine ambapo kuna nyumba kubwa sana ya kifahari na nje ya nyumba hiyo hapo getini, kuna kibao kidogo kimeandikwa maneno haya “bwana tumbo estate, niliposoma kibao hiko ambacho labda kilikuwa kinamtambulisha mmiliki wa nyumba hiyo, nilielewa pale pale ni nini Roho Mtakatifu alichokuwa ananiambia, kwamba “tumbo” la mtu ni bwana, kwa kifupi ni mungu” na kila anayelitumikia litampoteza kabisa, na kumfanya akose uzima wa milele”.
Na ndio maana siku za mwisho tumbo litatoweshwa..
1Wakoritho 16:13 “Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili”.
Kama mkristo uliyeokoka hakuna sifa yoyote unayopata kwa kula sana, wala chakula hakikusogezi karibu na MUNGU..
1Wakorintho 8:8 “Lakini chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu”.
Kama mkristo ni lazima ujifunze kulitawala tumbo, na si tumbo likuendeshe wewe, ni aibu kwa mkristo kumaliza mwezi haujafunga..hata hivyo kila wiki ni lazima uwe na angalau siku moja ya kufunga, tabia ya mkristo kusema kufunga ni mpaka uongozwe hatuipati katika maandiko, kama vile tunavyoikosa kanuni ya kula mara tatu kwa siku.
Ni kweli ni halali kula, hata mara tano kwa siku lakini si tabia inayofaa..
1Wakorintho 6:12 “Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote. 13 Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili”.
1Wakorintho 6:12 “Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.
13 Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili”.
Je umeokoka?.. Una uhakika Bwana YESU akirudi leo utakwenda naye?.. Kama bado haujaokoka fahamu kuwa muda umeenda kuliko unavyodhani muda wowote parapanda ya mwisho inalia, na wote walio nje ya Kristo watahukumiwa.
UVUKISHE MIPAKA UPENDO WAKO.
JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?
Kwa namna gani mauti ya wacha Mungu ina thamani machoni pake? (Zaburi 116:15).
JE! UMEFIKIA VIGEZO VYA KUWA BABA ROHONI?
Ni kwanini mifugo ya Yakobo iliongezeka kwa wingi kiasi kile?
Jina la BWANA YESU libarikiwe, karibu tujifunze Biblia, Neno la MUNGU wetu, lililo taa na mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).
Katika Biblia tunasoma jinsi MUNGU alivyomtukuza Mtumishi wake Musa, na hata kufikia wakati kusema akiwapo nabii mwingine yoyote atasema naye kwa ndoto na maono lakini Musa atasema naye mdomo kwa mdomo.
Hesabu 12:6 “Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, Bwana, nitajifunua kwake katika maono, NITASEMA NAYE KATIKA NDOTO. 7 Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; 8 KWAKE NITANENA MDOMO KWA MDOMO, MAANA, WAZIWAZI WALA SI KWA MAFUMBO; NA UMBO LA BWANA YEYE ATALIONA. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?”
Hesabu 12:6 “Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, Bwana, nitajifunua kwake katika maono, NITASEMA NAYE KATIKA NDOTO.
7 Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;
8 KWAKE NITANENA MDOMO KWA MDOMO, MAANA, WAZIWAZI WALA SI KWA MAFUMBO; NA UMBO LA BWANA YEYE ATALIONA. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?”
Sasa kitendo hiko cha Mungu kumtukuza Musa kuliko watumishi wake wengine, iliwafanya wana wa Israeli waamini kuwa hakutatokea tena mtumishi mwingine au nabii mwingine atakayekubalika na MUNGU kwa kiwango cha MUSA.
Na hata Musa alipokufa, na kijiti cha kuwaongoza wana wa Israeli kukabidhiwa mtumishi wa MUNGU Yoshua hakuna aliyemwamini wala kumheshimu Yoshua kwa kiwango ambacho Musa alichokuwa anaaminiwa na kuheshimiwa.
Na hilo MUNGU aliliona na kumwambia Yoshua maneno yafuatayo..
Yoshua 3:7 “BWANA AKAMWAMBIA YOSHUA, HIVI LEO NITAANZA KUKUTUKUZA MBELE YA ISRAELI WOTE, WAPATE KUJUA YA KUWA MIMI NITAKUWA PAMOJA NA WEWE, KAMA NILIVYOKUWA PAMOJA NA MUSA. 8 Nawe uwaamuru hao makuhani walichukuao sanduku la agano, ukawaambie, Mtakapofika ukingo wa maji ya Yordani, simameni katika Yordani”
Yoshua 3:7 “BWANA AKAMWAMBIA YOSHUA, HIVI LEO NITAANZA KUKUTUKUZA MBELE YA ISRAELI WOTE, WAPATE KUJUA YA KUWA MIMI NITAKUWA PAMOJA NA WEWE, KAMA NILIVYOKUWA PAMOJA NA MUSA.
8 Nawe uwaamuru hao makuhani walichukuao sanduku la agano, ukawaambie, Mtakapofika ukingo wa maji ya Yordani, simameni katika Yordani”
Sasa mbeleni tunaona ni nini kilitokea baada ya MUNGU kumwambia Yoshua maneno hayo, ni kwamba Maji ya mto Yordani yalitimamishwa yasitiririke kwa muda ili kuruhusu majeshi ya Israeli kuvuka, mfano ule ule tu wa jinsi Musa alivyopasua bahari ya Shamu kwa uweza wa MUNGU kuruhusu majeshi ya Israeli kuvuka.
Yoshua 3:14 “Hata ikawa, hao watu walipotoka katika hema zao, ili kuvuka Yordani, makuhani waliolichukua sanduku la agano wakatangulia mbele ya watu, 15 basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno), 16 ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko”.
Yoshua 3:14 “Hata ikawa, hao watu walipotoka katika hema zao, ili kuvuka Yordani, makuhani waliolichukua sanduku la agano wakatangulia mbele ya watu,
15 basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno),
16 ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko”.
Sasa ninachotaka tujifunze si jinsi MUNGU alivyokausha Yordani kwa mkono wa YOSHUA, bali ninachotaka tukione na kujifunza ni unyenyekevu wa Yoshua baada ya MUNGU kumwambia kuwa “anaenda kumtukuza katika Israeli, na kuwafanya watu wote wajue kuwa yupo na yeye kama alivyokuwa na Musa”.
Hebu turejee tena tuweze kutembea vizuri
Yoshua 3:7 “BWANA AKAMWAMBIA YOSHUA, HIVI LEO NITAANZA KUKUTUKUZA MBELE YA ISRAELI WOTE, WAPATE KUJUA YA KUWA MIMI NITAKUWA PAMOJA NA WEWE, KAMA NILIVYOKUWA PAMOJA NA MUSA”.
Sasa tungetemea kwamba kuanzia huo wakati Yoshua awaambie wana wa Israeli wote kuwa …“ yeye ndie kiongozi aliyechaguliwa na MUNGU hivyo wamsikilize na kumtii”.. lakini Yoshua hakufanya hivyo, kinyume chake tunaona alienda kuwaambia kuwa “MUNGU yupo na wao wote, na si yeye peke yake”..
Yoshua 3:9 “BASI YOSHUA AKAWAAMBIA WANA WA ISRAELI, NJONI HUKU, MKAYASIKIE MANENO YA BWANA, MUNGU WENU. 10 YOSHUA AKASEMA, KWA JAMBO HILI MTAJUA YA KUWA MUNGU ALIYE HAI YU KATI YENU, NA YA KUWA HATAKOSA KUWATOA MBELE YENU MKANAANI, NA MHITI, NA MHIVI, NA MPERIZI, NA MGIRGASHI, NA MWAMORI, NA MYEBUSI”.
Yoshua 3:9 “BASI YOSHUA AKAWAAMBIA WANA WA ISRAELI, NJONI HUKU, MKAYASIKIE MANENO YA BWANA, MUNGU WENU.
10 YOSHUA AKASEMA, KWA JAMBO HILI MTAJUA YA KUWA MUNGU ALIYE HAI YU KATI YENU, NA YA KUWA HATAKOSA KUWATOA MBELE YENU MKANAANI, NA MHITI, NA MHIVI, NA MPERIZI, NA MGIRGASHI, NA MWAMORI, NA MYEBUSI”.
Huu ni unyenyekevu mkubwa sana, ambao tunapaswa kuuiga, na hii ndio sababu ya MUNGU kumtumia Yoshua kwa uhodari mkuu hata kufanya ishara kubwa ambazo Musa hakuzifanya kama “kusimamisha jua”..kwasababu ni mtu aliye mnyenyekevu na mwenye kumrudishia MUNGU utukufu siku zote, si mtu wa majivuno au kujitukuza.
Nasi hatuna budi kujifunza unyenyekevu wa Yoshua, kwani maandiko yanasema kuwa Mungu huwapinga wenye kiburi lakini huwapa wanyenyekevu neema (1Petro 5:5).
Huenda kuna hatua Mungu kakuvusha, huna sababu ya kujivunia mbele za watu, badala yake mtukuze MUNGU na usubiri Mungu audhihirishe utukufu wake kwako, au labda kuna Baraka Mungu kakuahidia isiwe sababu ya wewe kujitukuza mbele ya watu, au kujionesha kuwa weweni bora kuliko wengine, bali siku zote jifunze unyenyekevu.
Bwana atusaidie, tuwe mfano wa mtumishi wake Yoshua.
MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.
JAWA NA UPENDO UNAOTAFUTA.
Unyenyekevu ni nini?
KIJAKAZI ALIYEJUA UPONYAJI ULIPO.
Nuru ya UpendobibliayetuEdit Profile
Wana wa Israeli walitoka kweli Misri, na Mungu akawaahidia kuwa mbele yao wamewekewa nchi njema ibubujikayo maziwa na asali, nchi yenye raha, na ya kustarehe (Kutoka 3:8). Na kweli wakaifikia hiyo nchi, waliyoahidiwa lakini biblia inasema hawakuipata ile raha aliyoikusudia Mungu.
Waebrania 4:8-10
8 Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye. 9 Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. 10 Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake.
Walidhani, wingi wa utajiri walioukuta, na ardhi yenye rutuba, na chakula kingi walichokutana nacho huko ndiyo raha yenyewe, lakini kumbe sio. Mungu alikuwa amewawekea Raha yake maalumu, ambayo wao walikuwa hawaithamini.
Raha yenyewe ilikuwa ni YESU KRISTO.
Mathayo 11:28
28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Mathayo 12:8
Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.
Tangu wakiwa jangwani, Yesu alianza kujidhihirisha kwao kwa njia ya maumbo, na ishara, lakini walimkataa, mfano ule mwamba waliounywea alikuwa ni Kristo (1Kor 10: 4:3), yule nyoka wa shaba aliyeinuliwa (Yohana 3:14-17) alikuwa ni Kristo, ile Mana alikuwa ni Kristo (Yohana 6:48-58), Jinsi ile hema ya kukutania ilivyokuwa imepangiliwa, makabila yote kuzunguka hema, huchora umbo la msalaba, ilikuwa ni msalaba wa Kristo.
Hivyo Kristo alikuwa tayari ni raha yao, Hivyo hata walipokuwa wanaingia katika nchi ya Ahadi wamengemwona kwa maumbile mengi yaliyo bora kuliko yale, akiwaponya kimiujiza, akiwapa raha nafsini mwao, kwa kuwatiririshia maji ya uzima mioyoni mwao, maziwa na asali yangeyaona halisi kabisa nafsini mwao, starehe wangeifikia, mpaka atakapotokea mwenyewe halisi katika mwili, ili kuubadilisha mfumo wa ulimwengu mzima kuwa milki ya Mungu.
Lakini baada ya kufika kwenye ile nchi walimpinga, sana, hata alipowatuma manabii wake bado hawakuwasikiliza, hatimaye, wakabakia tu Kaanani lakini sio rahani. Jambo hilo liliendelea kwa maelfu ya miaka, mpaka yeye mwenyewe Kristo alipochukua mwili na kuja katikati yetu,
Na tunaona wote waliompokea, waliingizwa kwenye Raha hii halisi, ambayo kwanza inaanza kwa kuwekwa huru mbali na utumwa wa dhambi, Lakini pia kujazwa Roho Mtakatifu, ndani yake ili kuruhusu badiliko kubwa kutokea ili kumfanya mtu aone kumpata Mungu ni raha zaidi ya fahari na mali zote za dunia.
Raha hii inaendelea ndani ya waamini, mpaka leo, na hadi Atakaporudi mara ya pili kuitimiza kwa ukamilifu wote wa macho kwa kutuingiza kwenye ile Mbingu mpya na nchi mpya, aliyotuandalia.
Hivyo kwasasa tumekabidhiwa jukumu la kuitunza, kwasababu tusipodumu ndani ya Kristo haijalishi tumeingia Kaanani kwa kubarikiwa mwilini, kiasi gani, pengine kiafya, ki-makazi au vinginevyo, haitufaidii kitu, bado tupo matesoni na utumwani. Ni wajibu wetu kuhakikisha nyakati zote tunadumu ndani ya Kristo, ili tukifikishwe kwenye kilele cha raha hiyo atakaporudi.
Waebrania4:1-11
Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa. 2 Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia. 3 Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha ile; kama vile alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu: 4 Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote; 5 na hapa napo, Hawataingia rahani mwangu. 6 Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao, 7 aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu. 8 Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye. 9 Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. 10 Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. 11 Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.
Hama Kaanani, zama rahani mwa Kristo.
Kitu pekee ambacho tumepewa na MUNGU kinachofanana kwa viumbe vyote ni “muda”.. Tunaweza tofautiana rangi, kimo, ukubwa, umri, utajiri, heshima, umaarufu, cheo, mamlaka n.k lakini hatuwezi kutofautiana muda.
Hata “Mchana” una muda sawa na “usiku” mgawanyo wa masaa 12, Bwana MUNGU hajaupendelea mchana kwa kuupa masaa mengi kuliko usiku, bali utaona usiku na mchana muda ni ule ule.
Mchana unaweza kuwa umependelewa kwa mambo mengi kuliko usiku.. lakini kwenye suala la muda, haujapendelewa, maana yake mambo yanayopaswa kufanyika mchana kwenye nuru na utukufu, yasipofanyika kwa masaa 12, basi giza litaingia na kutawala kwa masaa yale yale 12, ndio maana Bwana YESU alisema maneno hivi..
Yohana 11: 9 “Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu. 10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake”.
Yohana 11: 9 “Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.
10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake”.
Na yeye mwenyewe Bwana YESU alitumia muda vizuri sana na pia alitufundisha kuutumia muda vizuri..
Yohana 9:4 “Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka, maadamu ni mchana; usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.”
Umeona?.. muda ni kitu cha kuzingatia sana kwetu sote….hata ibilisi anazingatia sana muda, hafanyi mchezo na muda kabisa… kwani anajua, ukiisha huo hawezi tena kuuongeza..
Ufunuo 12:12 “ Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, AKIJUA YA KUWA ANA WAKATI MCHACHE TU”.
Hivyo na sisi ni lazima tujifunze kutumia muda vizuri..
SASA TUNAUTUMIAJE MUDA VIZURI?.. tusome maandiko yafuatayo..
Waefeso 5:15 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 MKIUKOMBOA WAKATI kwa maana zamani hizi ni za uovu 17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, BALI MFAHAMU NI NINI YALIYO MAPENZI YA BWANA.”
Waefeso 5:15 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 MKIUKOMBOA WAKATI kwa maana zamani hizi ni za uovu
17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, BALI MFAHAMU NI NINI YALIYO MAPENZI YA BWANA.”
Kulingana na maandiko hayo ni dhahiri kuwa tunaukomboa muda “KWA KUYAFAHAMU NA KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU”.
Mtu asiyeyafanya mapenzi ya MUNGU ni mtu anayetumia muda vibaya, na mapenzi ya MUNGU ni yale yaliyotajwa katika..
1Wathesalonike 4:2 “Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu. 3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; 4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; 5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.
1Wathesalonike 4:2 “Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.
3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;
5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.
Kwa urefu juu ya somo la “namna ya kuyajua mapenzi ya MUNGU na kuyafanya” basi wasiliana nasi kwa namba zilizopo mwisho wa ujumbe huu.
Je umeokoka?.. kama bado fahamu kuwa muda unakimbia kuliko kawaida, unavyozidi kukawia ndivyo mlango unavyozidi kuwa mwembamba zaidi, fanya uamuzi wa busara leo kumpokea BWANA YESU na atakusaidia kushinda dhambi.
Bwana akubariki
JIWEKE TAYARI KUYAFANYA MAPENZI YA MUNGU.
YAFAHAMU NA YATENDE MAPENZI YA MUNGU.
JE UNAYAFANYA MAPENZI YA MUNGU?
NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?
ATAWAFANYIA WAMCHAO MATAKWA YAO.
WhatsApp
Mungu anapotaka kumwinua mtu, si kila wakati atampa machaguzi fulani, au atamwagiza kiupendo, bali wakati mwingine atamshurutisha katika jambo ambalo halitaki kabisa, au hajawahi kulifanya, na hapa ndipo wengi hukimbia,
Simoni mkirene, alikuwa ni mkulima tu, akiendelea katika kazi zake za kilimo, lakini ghafla, alikamatwa na kutikwa msalaba ambao si wake,
Ni wazi kabisa hilo jambo halikumpendeza moyoni, na alionyesha ukinzani, ndio maana biblia inasema wakamshurutisha, lakini baadaye ilimbidi akubali tu, Bila kujua kuwa ndio heshima yake, ukuu wake, baraka zake zilipo.
Marko 15:21 Wakamshurutisha mtu aliyekuwa akipita, akitoka mashamba, Simoni Mkirene, baba yao Iskanda na Rufo, ili auchukue msalaba wake.
Shuruti maana yake ni kulazimishwa, kufanya matakwa magumu ya mtu mwingine.
Hakuna mtu anayependa shuruti, kulazimishwa kutenda, mambo ambayo hujajiandaa nayo, huna mapenzi nayo, huna nguvu nayo. Lakini fahamu kuwa kwa Mungu shuruti ni sehemu ya kukuzwa kwako kiroho,
Wakati mwingine Mungu anapoweka shuruti kwa wazazi wako, viongozi wako, wachungaji wako, Maadamu ni jema, tii tu hata kama hujisikii, ukishurutishwa kufunga na kuomba, usiseme mimi sijisikii wakati huu, fungeni nyie, ukishurutishwa kutoa huduma fulani, usiseme mimi sijajiandaa, bado ni mchanga kiroho, ukishurutishwa kuhudhuria darasa fulani usiwe na udhuru mwingi, ukasema nina ratiba zangu. Tii tu hata kama utaathirika kwenye mambo mengine, kwasababu Mungu huwatumia wao bila kujua, kukuinua kiroho na kihuduma.
Kama Simoni mkirene angegoma kabisa, leo hii tungemjulia wapi, lakini mpaka sasa vizazi vyote vinamjua na kumwona heri kwa kutenda tu hiyo huduma ambayo haikuwa machaguzi yake.
Watumishi wengi makanisani, wanaokuwa kihuduma ukichunguza kwa ukaribu utaona ni wale ambao wanapopewa majukumu yaliyo nje ya mipango yao, au zaidi ya uwezo na nafasi zao, huyapokea na kuyasimamia kikamilifu bila udhuru, bila kiburi.
Kubali shuruti za Bwana.
Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, ASIJIWEKE TAYARI, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. 48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi”.
Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, ASIJIWEKE TAYARI, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi”.
Hebu tulichambue kidogo neno hili kwa undani, neno baada ya Neno na kuna jambo tutajifunza..
maandiko yanasema “Mtumwa aliyejua mapenzi ya bwana wake”.. Kumbe! Kuna watumwa wanaoyajua mapenzi ya Bwana zao na kuna ambao hawayajui mapenzi ya Bwana zao…
Sasa mapenzi hayo ni yapi?.. Bila shaka si mengine zaidi ya yale tunayoyasoma katika kitabu cha
1Wathesalonike 4:2 “Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu. 3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, KUTAKASWA KWENU, MWEPUKANE NA UASHERATI; 4 KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE KATIKA UTAKATIFU NA HESHIMA; 5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.
3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, KUTAKASWA KWENU, MWEPUKANE NA UASHERATI;
4 KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE KATIKA UTAKATIFU NA HESHIMA;
Mapenzi ya MUNGU kulingana na maandiko hayo ni TUTAKASWE, Kwa kuepukana na uasherati na tamaa mbaya.
Sasa kama hayo ndio mapenzi ya MUNGU, (yaani UTAKASO)..hebu tuendee na maandiko yale ya Luka 12:47 tuone nini Roho Mtakatifu anataka kutufundisha.
Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, ASIJIWEKE TAYARI, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana”..
Umeona tena hapa! Kumbe kuyajua mapenzi ya MUNGU na KUTOJIWEKA TAYARI KUYAFANYA ni KOSA KUBWA!
Wengi tunadhani kosa ni “kutoyafanya tu”!…Lakini Biblia inatufundisha kuwa kosa linaanza kwa “kutojiweka tayari”.. Sasa nini maana ya kutojiweka tayari.
Tuanze na “kujiweka tayari” maana yake nini?.. kujiweka tayari ni kitendo cha kuwa tayari kiakili, kifahamu, kimkakati, na kiutendaji…. Mara nyingi “kujiweka tayari” kunatangulia kabla ya kitendo chenyewe, na kinyume chake kutojiweka tayari ni ile hali ya “kukataa, kudharau, kupuuzia, kuchukulia jambo juu juu, kusema huu sio wakati, kwa ufupi kutojishughulisha zaidi na kuyajua mapenzi ya MUNGU”.
Sasa Roho Mtakatifu anajua katika hali za kwanza kabisa za kuokoka si rahisi mwamini, awe mkamilifu katika kuyafanya mapenzi yake, Lakini anachokiangalia na kukithamini sana katika hatua za awali ni angalau mtu “kujiweka tayari”.
Maana yake mtu awe tayari kusikiliza maneno ya MUNGU na kuongozwa na Roho Mtakatifu, ili Roho Mtakatifu achukue nafasi ya kumtengeneza zaidi, pia awe ajiweke tayari kufanywa mpya na Roho Mtakatifu kwa kuendelea kumtii Roho Mtakatifu.
Lakini jambo la kuhuzunisha utakuta mtu analisikia Neno ambayo moyoni anajua kabisa ni kweli ya MUNGU, lakini hana utayari wowote moyoni wa kulitii… Utakuta mtu ndani Roho Mtakatifu anamfunulia kabisa njia sahihi ya kwenda lakini rohoni hana utii wala utayari bali anaendelea kufanya mambo yake, jambo lenye madhara makubwa kwani Biblia inasema mtu huyu “atapigwa sana”
Na ni wapi atakapopigwa?.. si pengine zaidi ya kwenye ziwa lile liwakalo moto katika siku ya mwisho..
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye AFANYAYE MAPENZI YA BABA YANGU ALIYE MBINGUNI”.
Sasa ili tuzidi kuona uzito wa jambo hili, tuendelee mbele kidogo na kitabu kile cha Luka, tuone adhabu ya wale ambao hawajajua mapenzi ya MUNGU, lakini wametenda yastahiliyo mapigo, jinsi watakavyoadhibiwa ili itupe kutafakari kwamba “kama wasiyoyajua watapigwa vipi kwa wale walioyajua mapenzi ya MUNGU na hawajajiweka tayari kuyafanya nini kitawapata”.
Umeisikia injili mara ngapi?.. Umefundishwa mara ngapi njia ya kweli na hautaki hata kujiweka tayari?.. je siku ile utasalimikaje kwa maneno yaliyo dhahiri kama haya?. Je utasema sikusikia?..na ili hali hata kujiweka tayari kusikia hukutaka?.. je kuna kusalimika unadhani?… Jibu lipo wazi kuwa hakuna kusalimika, suluhisho ni moja tu, kuanza kujiweka tayari kuyafanya mapenzi yake kabla ya mwisho kufika.
Na kama bado haujaokoka, umechelewa sana, upo nyuma sana, upo mbali sanaa.. leo fanya geuko la maisha kwa kumwamini mwokozi YESU, na kuzingatia kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha, Kwa msaada zaidi juu ya safari ya wokovu, kwa neema tuliyopewa tutakupa mwongozo wa hatua za kufanya, unachopaswa kufanya ni kuwasiliana nasi kupitia namba tajwa hapo chini.
Bwana YESU akubariki sana.
JE! UPO KATIKA MAJI YA UTULIVU?
KWA KUWA FURAHA YA BWANA NI NGUVU ZENU.
CHOCHOTE UMFANYIACHO KRISTO KINA THAMANI.
Maana ya Mithali 29:21 “Amtunduiaye mtumwa wake tangu utoto, Mwisho wake atakuwa ni mwanawe”
Desturi ya maziko kibiblia ilikuwaje?.