Category Archive Uncategorized @sw-tz

ASIYEMPENDA BWANA NA AWE AMELAANIWA.

Je unajua “Kumpenda Mungu sio Ombi bali ni Amri”?..Tofauti na inavyodhaniwa leo kuwa kumpenda Mungu ni jambo ambalo  ni “Ombi”.. Kwamba tunaombwa kumpenda Mungu.. Lakini Biblia haitufundishi hivyo.

Biblia inatufundisha kuwa kumpenda Mungu ni Amri, (maana yake tunaagizwa kumpenda Bwana Mungu wetu kwa roho zetu zote) na pasipo kufanya hivyo ni makosa..

Mathayo 22:35 “Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;

36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?

37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.

38 HII NDIYO AMRI ILIYO KUU, TENA NI YA KWANZA”

Ni madhara gani yanayoweza kumpata Mtu, anapoivunja hii amri na kumpenda miungu mingine?

Madhara yapo mengi  ikiwemo kuukosa uzima wa milele katika siku ya mwisho, lakini katika maisha haya dhara lake kubwa kuliko yote ni LAANA!.

Mtu asiyempenda Bwana MUNGU wake, anajiletea laana juu yake, na uzao wake na vyote alivyonavyo..

1Wakorintho 16:22 “Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha”.

Jifunze kumpenda Mungu kwakuwa yeye ndiye aliyekuumba.

Ukimpenda utamkaribisha YESU maishani mwako,

> Ukimpenda utaacha hizo dhambi unazozifanya (Zaburi 97:10)

> Ukimpenda utatafuta kujua kusudi lako kuja duniani ni lipi

> Ukimpenda hutaendelea na maisha ya uvuguvugu

> Ukimpenda hutafanya matambiko na mila

> Ukimpenda hutaabudu sanamu wala kudharau maagizo yake.

Ukimpenda utafanya yote yaliyoandikwa katika Biblia.

Kwa mapana kuhusiana na jinsi ya kumpenda Bwana kwa moyo wote, roho yote, nguvu zote na akili zote, fungua link hii hapa chini. >>

Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo,roho, akili na nguvu zetu zote?

 

Zaburi 145:20 “Bwana huwahifadhi wote wampendao, Na wote wasio haki atawaangamiza”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.

UVUKISHE MIPAKA UPENDO WAKO.

NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?

UPENDO WA KRISTO WATUBIDISHA;

JE UNAO UHAKIKA BWANA YESU AKIRUDI LEO UNAKWENDA NAYE?.

Print this post

JE NI MAFUTA GANI UMEPAKWA?.

Je ni mafuta gani umepakwa?.

1 Yohana 2:26 “Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza.

27 Nanyi, MAFUTA YALE MLIYOYAPATA KWAKE YANAKAA NDANI YENU, wala HAMNA HAJA YA MTU KUWAFUNDISHA; lakini kama mafuta yake YANAVYOWAFUNDISHA HABARI ZA MAMBO YOTE, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake”

Awali ya yote hebu tuangalie haya mafuta ya kweli ni ya namna gani kabla ya kujihoji kama yamo ndani yetu au la!.

Kama tunavyosoma hapo juu sifa za mafuta hayo Matakatifu ni “kutufundisha”..Na sio tu kutufundisha, bali “kutufundisha mambo yote”..

Hiyo ndio sifa ya kwanza, lakini sifa nyingine ya pili “YANAKAA NDANI YETU” (yaani moyoni).. Na si nje yetu (kwenye ngozi).. Mpaka kufikia hapo tumeshajua kuwa sio mafuta ya chupa au ya upako yanayozungumziwa hapo..bali ni mafuta mengine tofauti kabisa..

Hebu tusogee mbele zaidi kuangalia kimaadiko haya mafuta ni kitu gani na ni kwa namna gani “yanatufundisha habari za mambo yote”..

Kupitia maandiko yafuatayo tutapata majibu…

Yohana 14:26 “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, ATAWAFUNDISHA YOTE, na kuwakumbusha yote niliyowaambia”.

Kumbe kitu peke pekee chenye uwezo wa kutufundisha mambo yote ni Roho Mtakatifu?.

Bila shaka Yale mafuta yanayotajwa na Mtume Yohana katika 1Yohana 2:27 si mengine zaidi ya “Roho Mtakatifu”.

Na tunazidi kulithibitishaje hilo?.

Kwa kuvichunguza vitabu hivi viwili (1Yohana 2:27 na Yohana 14:26). Tunaona vyote vimeandikwa na mtu mmoja ambaye ni Mtume Yohana kwa uongozo wa Roho Mtakatifu.

Sasa isingewezekana kwa Yohana kumaanisha vitu viwili tofauti katika maandiko hayo mawili…bali alimaanisha kitu kile kile kimoja ambacho ni Roho Mtakatifu.

Na Roho Mtakatifu pekee ndiye anayekaa ndani yetu mandiko yanasema hivyo..

1 Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?”.

Soma pia..

2 Timotheo 1:14 “Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu”.

Na ni kwa namna gani “Ajapo Roho Mtakatifu, hamna haja ya mtu kutufundisha”?..

 Turejee Waebrania 8:10-12.

Waebrania 8:10 “Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.

11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena”.

Roho Mtakatifu ambaye ndiye “Mafuta ya Mungu ndani yetu” anapoingia ndanj ya mtu, yule mtu anakuwa na shauku ndani ya noyo wake wa kumtafuta Mungu mwenyewe, hahitaji kusukumwa na mtu,

Vile vile yule Roho Mtakatifu anakuwa anamfundisha kwa mafunuo ambayo hawezi kuyapata kutoka kwa watu..

Je umepakwa  mafuta na Bwana? Ambaye ni Roho Mtakatifu wake?..Kumbuka wote wasio na Roho Mtakatifu hao sio wake kulingana na Biblia (Warumi 8:9).

Na pia huwezi kujua yote pasipo Roho Mtakatifu..

1 Yohana 2:20 “Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote”

Kanuni ya kupokea Roho Mtakatifu, kwa mujibu wa Biblia ni ile iliyotajwa katika Matendo 2:38.

Matendo  2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.

Epuka elimu za uongo za kutumia mafuta ya kupikia au ya mizeituni kuvuta au kuimarisha ukaribu wako na MUNGU, ni hatari kubwa sana.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mafuta mabichi ni mafuta ya aina gani? (Zaburi 92:10)

Zaburi ya Pili ni nini? (Matendo 13:33).

UVUKISHE MIPAKA UPENDO WAKO.

Je tunajazwaje maarifa ya mapenzi yake? (Wakolosai 1:9)

Biblia inamaana gani inaposema “Mungu wa neema yote” (1Petro 5:10)

Print this post

Ni kwa namna gani YESU KRISTO atawahukumu walio hai na waliokufa?

Swali: Biblia inasema kuwa Bwana Yesu atawahukumu walio hai, na waliokufa (2Timotheo 4:1)

Jibu: Turejee..

2Timotheo 4:1 “Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, ATAKAYEWAHUKUMU WALIO HAI NA WALIOKUFA; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake”..

Maneno kama haya yanarudiwa tena katika kitabu cha 1Petro 4:5

1Petro 4:5 “Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu WALIO HAI NA WALIOKUFA”.

Zamani na hata sasa, ipo imani ya kwamba mtu akishakufa ndio tayari “kashahukumiwa” hakuna tena hukumu huko aendako.. maana yake mitihani aliyopitia akiwa duniani tayari ni hukumu tosha, hakuna tena hukumu baada ya kifo.

Lakini Biblia inatufudisha jambo jingine tofauti na hilo, kwamba watu wote ambao wamekufa pasipo kujalisha wamekufaje siku ya mwisho watafufuliwa na Bwana YESU na  kuhukumiwa..

Yohana 5:25 “Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.

26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.

27 Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.

28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.

29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu”.

Soma pia Mathayo 11:24 utaona kuwa hata baada ya hukumu ya moto ya Sodoma na Gomora bado watu wa miji hiyo watasimama tena kuhukumiwa katika siku ya mwisho..

Kwahiyo hukumu si ya walio hai tu, bali watu wote, (walio hai na waliokufa)..

Je umempokea YESU?.. Kumbuka sasa anasema nasi kama Mwanakondoo, lakini siku ya mwisho atakuwa ni Mhukumu.. wakati mlango wa Neema utakapofungwa, hakutakuwa na nafasi nyingine ya kutubu wala kupokea wokovu, bali kitakachokuwa kimesalia na hukumu..

Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.

12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao”.

Mpokee YESU leo, kama bado hujafanya hivyo.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Fahamu maana ya Mithali 21:3 Kutenda haki na hukumu  Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.

Nini maana ya Hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma?

ITAFAKARI SIKU YA HUKUMU.

NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.

Kuna hukumu za aina ngapi?

Print this post

Kughofiri ni nini (Zaburi 79:9).

Swali: Kughofiri ni kufanya nini kama tunavyosoma katika Zaburi 79:9?.


Jibu: Turejee..

Zaburi 79:9 “Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie, Kwa ajili ya utukufu wa jina lako. Utuokoe, UTUGHOFIRI dhambi zetu, Kwa ajili ya jina lako”.

Maana ya “Kughofiri” ni “kuondoa”.

Neno hilo limeonekana mara moj tu kwenye Biblia…na maana yake ni ile ile na ya kusamehe..

Lakini Biblia inazidi kutufundisha kuwa Bwana anatuokoa na kutusamehe pia makosa yetu kwaajili ya jina lake.

Maana yake pia kwa utukufu wa jina lake, anapotusamehe makosa basi pia jina lake linatukuzwa zaidi, hivyo ni fahari ya Mungu pia kutusamehe sisi.

Isaya 43:25 “Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako”

Sasa swali kama Mungu anafurahia kutusamehe makosa yetu kwanini tusitumie hiyo fursa kuungama?.

Je umempokea YESU?.. Umetubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha?kama bado je unasubiri nini?…

Tubu leo upate msamaha wa dhambi, na  upate ondoleo la dhambi pia.

Luka 24:46 “Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;

47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu”.

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NGUVU YA MSAMAHA

UMUHIMU WA KUOMBA MSAMAHA.

KAMA NISIPOKUTAWADHA, HUNA SHIRIKA NAMI

NINI MAANA YA UKOMBOZI?

ZIFAHAMU ALAMA KUU NNE ZA KRISTO NDANI YAKO.

Print this post

KUJITAKASA NI MUHURI WA UTAKATIFU

Biblia inasema watakatifu waliopo duniani ndio Bwana wanaompendeza.

Zaburi 16:3 “Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao”.

Lakini swali ni je! anaposema “Watakatifu”..anamaanisha ni watu wasiokosea kabisa?…kwamba hawawezi kabisa kufanya makosa na kwamba wamekamilika kwa asilimia zote?.

Jibu ni Ndio! … watu wote waliompokea YESU na kupokea Roho Mtakatifu wamekamilika kwa asilimia zote katika vigezo vya “Kuokolewa”, mbele za Mungu lakini si katika vigezo vya kutokosea kabisa (Yaani kufanya mistakes).

Kukosea kusoma maandiko wakati wa mahubiri hayo ni makosa (mistakes), kusahau kutimiza ahadi uliyoitoa kwa mtu ni makosa..

Sasa makosa ya namna hiyo hayawezi kumpokonya mtu haki ya kuwa “MTAKATIFU” mbele za MUNGU.

Vile vile ikiwa mtu kampokea YESU leo na bado hajajua kuwa “anapaswa akabatizwe” ili akamilishe wokovu wake (sawasawa na Marko 16:16).

Na akawa katika hali hiyo hiyo ya kutobatizwa lakini bado anafanya mengine ya imani yaliyo sahihi bado hiyo haimwondolei sifa ya kuwa MTAKATIFU MBELE ZA MUNGU…yupo miongoni mwa watakatifu wa Bwana waliopo ulimwenguni.

Halikadhalika na mambo mengine yote ambayo mtu hajayajua wala kuyasikia kama ni makosa katika hatua zake za awali za wokovu, hayawezi kumpokonya haki ya kuwa mtakatifu mbele za MUNGU.

Lakini anaposikia au kuujua ukweli na kuupinga au kukataa mabadiliko anapoteza moja kwa moja sifa ya kuwa MTAKATIFU mbele za MUNGU.

Kwa namna gani?

Hebu tusome

Ufunuo 22:1″Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; NA MTAKATIFU NA AZIDI KUTAKASWA

Nataka tuone hapo…“NA MTAKATIFU NA AZIDI KUTAKASWA”..

Kama MTAKATIFU ameshakamilika hafanyi makosa kwanini tena hapo maandiko yaseme…“NA AZIDI KUTAKASWA”..

Kumbe MTAKATIFU bado anaweza KUTAKASWA.

Maana yake ni kwamba hakuna kipimo fulani  maalumu kwamba hapa mtu kashafikia  UTAKATIFU wa mwisho…

UTAKATIFU ni jambo endelevu, kwamba kila siku tunajiona kasoro zetu na kufanya mabadiliko.

Unaweza kujiona leo upo sawa kabisa kiimani na kiutakatifu..lakini baada ya mwezi mmoja uliposoma Neno ukajigundua kuna mambo ulikuwa unakosea hivyo ukajirekebisha,….hapo maana yake “umejitakasa”.

Sasa kipindi ambacho hukuwa unajua makosa, haimaanishi kwamba haukuwa mtakatifu..La! Ulikuwa mtakatifu…

Lakini siku ulipojua jambo fulani ni kosa na kubadilika..hapo “ulizidi kuwa mtakatifu”…na siku utakapojua jambo jingine ambalo leo hii hulijui. Na jambo hilo ukaliacha “hapo utazidi kuwa mtakatifu mara mbili zaidi”.

Kwahiyo ili tuweze kuhesabika ni watakatifu ni lazima “TUJITAKASE”.

Je na wewe ni Mtakatifu?..Je na wewe unajitakasa?.

Swali unajitakasaje?.

Unajitakasa kwa kukaa mbali na kila aina ya vichocheo vya dhambi, na kwa kusoma Neno na maombi pamoja na kukusanyika na wengine (kufanya ibada).

Kuna mambo hutaweza kujua kuwa ni makosa pasipo kusoma Neno, kuna mambo huwezi kujua kuwa ni makosa usipokuwa mwombaji n.k

Bwana akubariki na kuzidi kutusaidia..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

Zaburi ya Pili ni nini? (Matendo 13:33).

Swali: Katika kitabu cha Matendo 13:33 tunasoma pakitajwa “Zaburi ya Pili” je hii zaburi ya Pili ni ipi, nay a kwanza ni ipi na ya mwisho ni ipi?


Jibu: Tuanzie kusoma ule mstari ule wa 32..

Matendo 13:32 “Na sisi tunawahubiri habari njema ya ahadi ile waliyopewa mababa,

33 ya kwamba Mungu amewatimizia watoto wetu ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu; kama ilivyoandikwa katika ZABURI YA PILI, Wewe ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa”.

Andiko hilo ni Mtume Paulo alikuwa akilirejea kutoka katika kitabu cha Zaburi ule mlango wa Pili, ambapo ndipo tunaposoma maandiko hayo..

Zaburi 2:7 “Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa”.

Kwahiyo tafsiri rahisi ya “Zaburi ya Pili” anayoizungumzia Mtume Paulo katika hiyo Matendo 13:33 ni “Zaburi Mlango wa PIli au Zaburi sura ya Pili”.. ndipo unabii huo unapotokea.. Na Zaburi ya Tatu ni Zaburi mlango wa tatu… na Zaburi ya mia na hamsini ni Zaburi mlango wa mia na hamsini (150).

Lakini pia tunasoma mahali pengine, mwandishi wa kitabu cha Wabrania akinukuu Zaburi hiyo ya Pili..

Waebrania 1:5 “Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, NDIWE MWANANGU, MIMI LEO NIMEKUZAA? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?”

Na tena akarudia katika ule mlango wa tano.

Waebrania 5:5 “Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.”

Je umempokea YESU?.. kama bado unasubiri nini?. Fahamu kuwa hizi ni siku za mwisho na YESU amekaribia sana kurudi.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Fahamu mana ya Zaburi 48:14 Yeye ndiye atakayetuongoza

Mafuta mabichi ni mafuta ya aina gani? (Zaburi 92:10)

Fahamu maana ya Zaburi 125:3 “ Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki.

Uele ni nini katika biblia? (Zaburi 91:6)

Nini maana ya neno kumwamba (Zaburi 78:19)

Print this post

FUPISHA MUHULA WA MASHETANI.

Mathayo 8:29

[29]Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?

Mashetani yanajua kila jambo lipo katika mpangilio wa muda wake, yanajua kuwa tayari hukumu ilishatolewa ya wao kutupwa katika ziwa la moto lililo hatma yao ya milele..

Lakini utekelezaje wake, utakuja baadaye, ambao utakuwa ni mwisho wa dunia, utakao asisiwa na Bwana Yesu Kristo mwenyewe.(Mathayo 25:41)

Wengi tunadhani mapepo, hushindana na sisi, kwa kutuonea wivu, hilo ni kweli kwa sehemu, lakini sababu kubwa ya mapepo na shetani kushindana na sisi…ni wao kujilinda…na adhabu ijayo.

Na wanajua mwanadamu ndiye anayeweza kuiharakisha hiyo siku au kuikawiisha hiyo siku. Ndio maana yanafanya kazi kubwa sana kuwaharibu wanadamu ili siku hiyo isifike upesi.

Hizi ni njia tatu mapepo, hufanya kwa watu ili kukawiisha muhula wao usiwafikie haraka.

1) Kuchochea maovu.

2) Kukengeusha Imani za watu

3) Kukawisha injili

1) Kuchochea maovu.

Maovu mengi, humsukuma Mungu kuwa mvumilivu na wanadamu, ili wafikie toba wasiangukie hukumu ya mapepo..Kama wanadamu wasingekuwa na shingo ngumu, mwisho wa dunia na hukumu yao ingeshafika zamani sana.. hivyo mapepo wanabuni kazi mbalimbali ili kuwafanya wanadamu wazidi kupotoka.

2 Petro 3:9-11

[9]Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

[10]Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

[11]Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,

2) Kuikengeusha Imani

Luka 18:8

[8]Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?

Kristo anatarajia kanisa lake kusimama katika msingi wa imani kamili ambayo haijaharibiwa wala kuvurugwa na mapokeo na mafundisho ya uongo.. hii ndio sababu ya shetani kuinua makundi ya manabii wa uongo, kufundisha injili nyingine ambayo Kristo hajaileta duniani. Matokeo yake ndio kuwa na kundi kubwa la wakristo lakini dhaifu wasio tayari kumlaki Bwana mawinguni.

3) Kukawiisha Injili.

Mathayo 24:14

[14]Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.

Injili ya kweli adui huipiga vita vikubwa..Na wanajua ikihubiriwa ulimwenguni kote, basi ushuhuda wa Mungu utakuwa umefika na hakuna atakayekuwa na udhuru.

Sasa mimi na wewe hatuna budi kusimama katika utakatifu lakini pia imani na injili kuisambaza ili watu waokolewe…

Kumbuka tayari tupo kwenye siku za mwisho, Amka simama na Bwana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.

Je mkristo anaweza akawa na mapepo?

Shetani anaishi wapi, Je! Amefungwa au yupo kuzimu?

Print this post

MAANA HUYAWAZI YALIYO YA MUNGU, BALI YA WANADAMU

Jina la YESU KRISTO libarikiwe. Karibu katika kuyatafakari maneno ya Uzima,

Si kila sauti inayokujia kwa faraja, ina lengo la kukupa faraja.. si kila sauti inayokujia kwa kukupa matumaini ina lengo la kukupa matumaini mwisho wake.  Hebu tujifunze juu ya Bwana wetu YESU KRISTO, alivyoweza kuzipambanua roho..

Mathayo 16:12 “ Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.

22  Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.

23  Akageuka, akamwambia Petro, NENDA NYUMA YANGU, Shetani; u kikwazo kwangu; MAANA

HUYAWAZI YALIYO YA MUNGU, BALI YA WANADAMU.

Nataka tuone hilo neno “MAANA HUYAWAZI YALIYO YA MUNGU, BALI YA WANADAMU.”.. Kumbe mawazo ya shetani siku zote sio ya mapepo, wala ya mashetani yake bali ya wanadamu!.. Maana yake shetani anaangalia ni nini wanadamu wanakipenda zaidi na kuvitamani na kupitia vitu wanadamu wanavyovipenda na kuvitamani na kuvitafuta ndio vitu hivyo hivyo anatumia kuwaangusha chini katika hatua za mwanzo.

Hapa anajua mwanadamu anapenda “faraja na kutiwa moyo” anakuja kwa gia hiyo hiyo kwa Bwana YESU, akitaka kumfariji kwamba “hatapata mateso, hatakwenda msalabani”.. kwsababu anajua hayo ndio mawazo ya wanadamu siku zote, kutafuta faraja, kutiwa moyo n.k.

Lakini kwasababu YESU KRISTO ni “MWAMBA MGUMU”.. anayajua mawazo ya kila mtu kabla hata hajaambiwa, pale pale alimwona shetani ndani ya Petro, na kumkemea..

Ni kanuni hiyo hiyo shetani anaiendeleza hadi leo,  hajabadilika,  shetani anayasoma mawazo ya wanadamu wanataka nini na kupenda nini, anajua wanadamu , wanapenda kutiwa moyo, hawapendi kukemewa kemewa, hawapendi kukatishwa tamaa..

Sasa ili baadaye afanikiwe kumkatisha mtu tamaa kikweli kweli, ni lazima aanze kama na kwa kumfariji sasahivi, ili baadaye amvunje moyo kweli kweli, na asiweze kusimama tena,  ni lazima aanze sasa hivi kama kwa kumtia moyo..ndicho alichokuwa anataka kujaribu kukifanya kwa Bwana YESU lakini alishindwa.

>Biblia imesema imetupasa “Kuokoka” lakini shetani atakuambia “Bado wakati ngoja kwanza utafute maisha”

>Biblia imesema imetupasa “Kuwa waombaji” lakini shetani atakuambia “wewe upo bize sana, unachoka na kazi”

>Biblia imesema imetupasa “Kuhudhuria kanisani kila jumapili na hata katikati ya wiki (Waebrania 10:25)” lakini shetani atakuambia “kazi zimekuwa nyingi, Mungu atakuelewa tu”.. Ni kama neno la faraja lakini mwisho wake ni huzuni kubwa.

>Biblia imesema imetupasa “Kumtumikia Mungu (Yohana 9:4)” lakini shetani atakuambia “bado wakati, wapo wanaokuombea”

> Biblia imesema imetupasa “kujikana nafsi na kubeba msalaba tunapookoka”.. Lakini shetani atakuambia “usiogope siku moja utajikana tu, ila sasahivi endelea tu kuwa hivo hivo vuguvugu, hakuna mtakatifu duniani”

> Biblia inasema “usiwe mzinzi, na ukizini utakufa” lakini shetani anakuambia hutapata madhara wala hutakufa wapo wanaofanya na wanaishi mpaka leo..

Hayo yote ni mawazo ya shetani ndugu, ambayo ni ya wanadamu!.. Ni lazima tuwe makini katika hili, si kila sauti au wazo linalokuja kwa faraja na matumaini ni la MUNGU, angalia na pima je! Hilo wazo linakubaliana na wazo la MUNGU, kama linakinzana na Neno la MUNGU basi hata kama linakuja kwa sauti ya faraja kiasi gani usisikilize!.. bali sema “NENDA NYUMA YANGU SHETANI KWANI HUYAWAZI YALIYO YA MUNGU BALI WANADAMU”..

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je wakati Bwana YESU anazaliwa shetani alikuwa amefungwa?

SADAKA INAHARIBU NGUVU ZA MADHABAHU ZA MASHETANI.

Je! Yesu aliwezaje kuchukuliwa na shetani juu ya kinara cha hekalu kujaribiwa?

Je! Shetani anao uwezo wa kuumba, kama Mungu?

Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)

Print this post

UMEELEWA MAANA YA KUZALIWA KWA MBEGU ISIYOHARIBIKA?

1 Petro 1:23-25

[23]Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. 

[24]Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka; 

[25]Bali Neno la Bwana hudumu hata milele. 

Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu. 

Neno la Mungu linatuonyesha mtu aliyeokoka, anatambulika kuwa amezaliwa mara ya pili kwa mbegu isiyo haribika…lakini wengi hawajui makusudi ya kuzaliwa kwa mbegu hiyo ni nini?

Kabla ya kuona mbegu isiyo haribika, ifahamu kwanza mbegu iharibikayo ni ipi..

Katika habari hiyo tunaonyeshwa mbegu iharibikayo mfano wake ni ile ya mwanadamu .maana yake ni kuwa wewe ulizaliwa kwa mbegu ambayo inaanza katika mtoto, kisha ujana wenye nguvu, lakini baadaye utaishia na kuchakaa, na kuchoka kwa kuishiwa nguvu na hatimaye kufa…ndio hapo anasema mwili wote ni kama nyasi hukauka na kuanguka…kwasababu asili ya mbegu hii si ya kudumu daima.

Vivyo hivyo na mbegu nyingine zote za hapa duniani mfano, za wanyama, samaki, mimea zote ni mbegu ziharibikazo huisha ubora kulingana na wakati.

Lakini ukizaliwa kwa mbegu isiyo haribika maana yake ni kuwa ubora wako haupungui wala hauishi kulingana na wakati ..

Mtu aliyezaliwa kwa mbegu hii ambayo ni Neno la Mungu…huwa hazeeki rohoni, haishiwi nguvu wala hafi kiroho..

Lakini utashangaa mtu anasema kazaliwa mara ya pili, hapo mwanzoni alianza vizuri sana na Bwana, anaomba, anasoma Neno, amesimama, anamtumikia Bwana kwa bidii na uaminifu, lakini baada ya muda anaanza kupoa, hatimaye anaacha hata kuabudu na mwisho anakufa kiroho….miaka miwili nyuma alikuwa ameokoka lakini leo ni mtu mwingine kabisa…hapo ni lazima ujiulize je huyu mtu alizaliwa kwa mbegu ipi?

Kama ni mbegu isiyoharibika mbona wokovu wake unaharibika kulingana na wakati ..kikawaida mwamini kwenye maisha ya kiroho hufanyika upya siku baada ya siku, huama kutoka utukufu mmoja hata mwingine imani moja hata nyingine…lakini wewe unaharibika siku baada ya siku, je wewe ni mbegu gani?

2 Wakorintho 3:18

[18]Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho. 

2 Wakorintho 4:16

[16]Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. 

Ikiwa unajiona wewe umezaliwa kwa mbegu isiyoharibika, basi onyesha hivyo kwa ubora wako wa kiroho na kiiamani kila siku…ikiwa ni mchungaji onyesha mwendelezo wa kulisimamia kundi la Mungu katika nyakati zote iwe ni ngumu na nyepesi, ikiwa ni mwinjilisti, hupaswi kuacha kuhubiri maisha yako yote, ikiwa ni mhudumu wa kanisani, simama katika nafasi yako kwa ubora wote…usiseme yatosha, usiseme nimechoka,.kwasababu hukuzaliwa kwa mbegu ichokayo, isinyaayo, bali kwa Neno la Mungu lidumulo milele. Ikiwa ni mwombaji, usianze kusema hapo zamani mimi nilikuwa nina uimara kimaombi, kinyume chake onyesha vitendo, hata sasa moto wako ni ule ule tena na zaidi.

Unyesha ubora huo na amani ya Bwana iwe pamoja nawe.

Maran Atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Shuhuda za Mungu ni zipi?

Bawa la mbuni hufurahi; Lakini mabawa yake na manyoya yake, je! Yana huruma? 

TIA MIZIZI CHINI, ILI UZAE MATUNDA JUU.

 

 

Print this post

Shuhuda za Mungu ni zipi?

SWALI: Mara nyingi biblia inataja “shuhuda za Mungu” Je hizi shuhuda ni zipi?

Mfano katika vifungu vifuatavyo Neno hilo utaliona;

Zaburi 119:2

[2]Heri wazitiio shuhuda zake,  Wamtafutao kwa moyo wote.

Zaburi 119:22

[22]Uniondolee laumu na dharau, Kwa maana nimezishika shuhuda zako.

Zaburi 119: 24

[24]Shuhuda zako nazo ndizo furaha yangu, Na washauri wangu.

Zaburi 119:99

[99]Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.

Soma pia…Zab 119:119, 144, 132:12

Hizi shuhuda ni zipi?

Shuhuda ni neno linalozaa ushuhuda au kushuhudia.

Ni kitendo cha kuthibitisha ukweli wa jambo.

Kwamfano nikisema yule “mtu ni mkarimu”. Hapo nimemshuhudia kwasababu nimeona kitu hicho ndani yake, aidha amenitendea mimi ukarimu au kamtendea mwingine..

Tofauti na kama angejisemea mwenyewe..

Hivyo Mungu naye ana vitu amevihakiki kuwa ni kweli, na hizo ndizo zinazoitwa shuhuda zake..

Mpaka jambo Mungu amelihakiki mwenyewe ni kutuhakikishia kuwa hatupotei tukilifuata, tofauti na kama tungeshuhudiwa na wanadamu…kwasababu shuhuda za wanadamu zina udanganyifu mwingi nyuma yake.

Sasa shuhuda kuu za Mungu ni zipi.

Yesu Kristo ni mwana wa Mungu na ndiye uzima wetu.

1 Yohana 5:7-12

[7]Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.

9… Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.

[10]Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.

[11]Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.

[12]Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.

Huu ndio ushuhuda mkuu wa Mungu, na huu ndio tuliopewa tuuhubiri kwa ulimwengu pia kwamba kwa Yesu kuna ukombozi, na uzima..

Matendo ya Mitume 4:33

[33]Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote.

Sisi (tulioamini) ni wana wa Mungu Huu ni ushuhuda mwingine wa Mungu mwenyewe ndani yetu kupitia Roho wake Mtakatifu.

Warumi 8:16-17

[16]Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

[17]na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.

Si Kristo tu peke yake ni mwana wa Mungu, na sisi pia tunapomwamini tunafanyika watoto wake (Yohana 1:12 )watoto wa Mungu mfano wa Kristo.

Hivyo tunapopitia mateso kama yeye, hatupaswi kuwa na hofu au manung’uniko, kinyume chake ndio tujipige vifua vyetu kushangilia, kwani hata yule wa pekee(Yesu), aliyapitia hayo…kwasababu kama vile alivyopata mateso na alivyorithi utukufu vivyo hivyo na sisi tutarithi utukufu wake.

Mungu anataka tutembee kwa ujasiri hapa duniani, tusiishi kama yatima, tuishi tukijua kuwa tunaye Baba mbinguni anayetutazama na kujishughulisha sana na mambo yetu yote, kwasababu yeye mwenye ametuthibitisha kuwa sisi ni wana wake…Kama yeye ametuthibitisha nafsi yako kwanini ipinge? Wanadamu kwanini wapinge, ulimwengu kwanini upinge?

Hivyo kwa hitimisho ni kuwa tunaposema tumezishika shuhuda zake maana yake ni kuwa tumeamini wokovu na uzima utokao kwa Kristo Yesu, lakini pia tumekubali kuwa wana wa Mungu, yaani tukubali dhiki kwa ajili ya jina lake, tuishipo maisha ya kumpendeza yeye, lakini pia kupokea tumaini la utukufu lililo mbele yetu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

DHAMBI HAIWEZI KUKAA NA MSHAHARA WAKO.

USHUHUDA WA RICKY:

FUNGUA KINYWA CHA ROHO MTAKATIFU KIHUDUMU.

Print this post