JINA LAKO LIMEANDIKWA WAPI?

JINA LAKO LIMEANDIKWA WAPI?

Je jina lako limeandikwa wapi?, kwenye nyaraka za umma?, kwenye vitabu vya simulizi?, kwenye vitambulisho vya umma?, kwenye orodha ya wafungwa?, kwenye orodha ya wahalifu?, kwenye vilinge vya wachawi?, kwenye vitabu vya washirika wa kanisa?, kwenye vitabu vya walipa kodi na watoaji zaka?.. au limeandikwa wapi?.

Ni muhimu kujitathmini ni wapi jina lako lipo wapi?.. Kama jina lako litakuwepo kila mahali pa heshima duniani na likakosekana mbinguni, heshima yako ni bure, hadhi yako ni bure, uzuri wako ni bure, umaarufu wako ni bure na nguvu zako ni bure.

Hata kama jina lako litakuwa limeandikwa Kanisani, kama mtoaji mzuri, au mshirika mzuri bado kama halipo mbinguni wewe au mimi si kitu kabisa.

Kama kanisa lina washirikia efu, na hakuna hata mmoja aliyeandikwa mbinguni bado hilo kanisa ni bure, ndivyo Biblia inavyotufundisha kuwa kanisa halisi ni la watu waliondikwa majina yao mbinguni.

Waebrania 12:23 “Mkutano mkuu na KANISA LA WAZALIWA WA KWANZA WALIOANDIKWA MBINGUNI, na MUNGU MWAMUZI WA WATU WOTE, na roho za watu wenye haki waliokamilika”.

Hata mtu akitenda miujiza mingi na miujiza  na akafanikiwa sana na akafurahi na kushangilia kama jina lake halipo mbinguni bado ni kazi bure..

Luka 10:20 “Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini KWA SABABU MAJINA YENU YAMEANDIKWA MBINGUNI”.

Je jina lako limeandikwa mbinguni?.. Utauliza je jina la mtu linaandikwaje mbinguni?

Ndio jina la mtu linaandikwa mbinguni baada ya kuzaliwa mara ya pili, maana yake kuokoka na kuacha dhambi na kuishi maisha matakatifu yanayompendeza MUNGU, lakini pia jina la mtu linaweza kufutwa mbinguni ikiwa mtu huyo atarudi nyuma na kuiacha ile njia nyoofu ya usafi na utakatifu.

Kutoka 32:33 “Bwana akamwambia Musa, Mtu ye yote aliyenitenda DHAMBI NDIYE NITAKAYEMFUTA KATIKA KITABU CHANGU”.

Je umeokoka na kusimama?.. au maisha yako ni ya uvuguvugu?, leo upo kanisani kesho kwenye vijiwe vya usengenyaji?.. leo unaomba kesho unakula rushwa?, leo unamwimbia Mungu kesho unamwimbia ibilisi, simu yako imejaa uchafu na wakati huo huo ina nyimbo za injili.

Fahamu maisha ya uvuguvugu yanaondoa jina lako kwenye kile kitabu cha uzima, maisha ya kusita sita kumtafuta MUNGU yanalifuta jina lako mbinguni, na siku ya mwisho ni majina yetu ndiyo yatakayotafutwa ndani ya kile kitabu cha uzima, na si picha zetu, wala sifa zetu, wala umaarufu wetu…na majina yakikosekana hakuna nafasi ya kuingia malango ya mbinguni.

Ufunuo 20:15 “Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.

Bwana atusaidie tuweze kusimama na kuishi maisha ya kumpendeza yeye daima.

Shalom.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply