Katika maandiko ukikutana na kisa kinaishia kwa kusema ‘hata leo’. Basi kuwa makini hapo kwasababu lipo la kukusaidia.
Kwamfano Ibrahimu alipopanda kule mlimani kumtolea Mungu sadaka kwa Isaka, Mungu alimpa kondoo badala yake, Kwa tukio hilo Ibrahimu akapaita mahali pale Yehova-yire. (Maana yake Mungu-mpaji). Hivyo jambo lile maandiko yanasema liliendelea kutamkwa na watu kwa wakati mwingine mwingi sana kama usemi uliohai ‘Yehova-yire’, Mungu atupaye.
Mwanzo 22:13-14
[13]Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. [14]Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.
[13]Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
[14]Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire,
kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.
Mfano mwingi ni wakati wa Yoshua alipoiangamiza nyumba ya Akani, msaliti, biblia inasema;
Yoshua 7:26
[26]Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa ya mawe hata leo; naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata hivi leo.
Ikiwa na maana bonde hilo liliendelea kuitwa vile vile hadi wakati wa mwandishi. ‘Ipo sababu’.
Mfano mwingine ni kipindi cha Yehu alipoyavunja mahekalu ya Baali..
2 Wafalme 10:27
[27]Wakaibomoa nguzo ya Baali, na kuiangusha nyumba ya Baali, wakaifanya choo hata leo.
Ikiwa na maana mpaka wakati mwandishi anaandika hicho kitabu eneo hilo lilikuwa ni choo.
Mahali pengine ni hapa..
Israeli kuwa hatarini kuvamiwa na wamoabu, wakamlilia Mungu, kisha kawaambia hawatapigana vita bali watakwenda kuokota nyara, kazi yao iwe ni kusifu na kuimba tu. Maadui zao wakauana wao kwa wao Na eneo lile wakaliita bonde la baraka hata leo.
2 Mambo ya Nyakati 20:25-26
[25]Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana. [26]Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipombarikia BWANA; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo.
[25]Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana.
[26]Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipombarikia BWANA; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo.
Mahali pengine ni wakati wa kifo cha Yuda, lile shamba lililonunuliwa liliitwa konde la damu mpaka nyakati za mwandishi..
Mathayo 27:8
[8]Kwa hiyo konde lile huitwa konde la damu hata leo.
Sasa biblia kusema ‘hata leo’ sio tu kutoa uthibitisho wa tukio kwamba kweli lilitokea ..lakini ni vema kujua tafsiri yake rohoni…kwamba kuna minyororo aidha ya baraka au laana inatembea mpaka leo.
Kwamfano watu waliposema Yehova-yire walijua Mungu ni mpaji wakati wote…hivyo wakamwona katika mazingira hayo..ndio maana wakasema ‘hata sasa’ si tu wakati wa Ibrahimu.
Neno hilo lipo hai hata leo rohoni. Ukiamini Mungu aliyomtendea Ibrahimu anakwenda kukutendea na wewe, utapokea…kwasababu lipo hivyo hata leo.
Anaposema mahali pale pakaitwa bonde la baraka hata leo. Ni kweli rohoni hata leo bonde hilo lipo.
Ukiamini kwamba katika kumwimbia Mungu unaingia katika bonde la baraka. Utapokea vingi kwa Mungu, sawasawa na walivyopokea Israeli kipindi cha Yehoshafati vitani.
Hivyo mambo mengi na matukio mengi yanaendelea kutembea katika roho hata sasa…Je! Macho yako yanaona?
Ukiwa mwovu kama Akani, kumbuka bonde la Akori lipo mpaka leo, ikiwa utakuwa msaliti kama Yuda konde la damu lipo hata leo utazikiwa huko.
Chagua mema, yaishi mema, upokee mema
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ