Je YESU KRISTO alikuwa na wadogo zake?

Je YESU KRISTO alikuwa na wadogo zake?

Swali: Je YESU alikuwa na dada na kaka (ndugu wa kike na kiume), kama watu wengine?


Jibu: Ndio! Bwana wetu YESU KRISTO alikuwa na ndugu wengine wa kike na kiume, waliozaliwa na Mariamu mamaye!, maandiko yanathibitisha hilo katika Mathayo 13:55-56 na Marko 6:3.

Mathayo 13:54 “Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?

55 Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? NA NDUGUZE SI YAKOBO, NA YUSUFU, NA SIMONI, NA YUDA?

56 NA MAUMBU YAKE WOTE HAWAPO HAPA PETU? Basi huyu amepata wapi haya yote?”

Kulikuwa na sababu ya kuanza na “Mwana wa seremala (Yusufu) na  kisha Mariamu mamaye na kumaliza na akina Yakobo, Yusufu, Simeoni na Yuda na maumbu (yaani wadada)”.. Ikimaanisha kuwa iliyokuwa inatajwa hapo ni familia, na si ukoo.

Ikimaanisha kuwa Marimu baada ya kumzaa Bwana YESU hakuendelea kuwa Bikira, bali alizaa watoto wengine pamoja na Yusufu mumewe, na watoto hao walikuwa wakike na kiume kama walivyotajwa hapo juu.

Ipo imani kuwa Mariamu hakuendelea kuzaa watoto wengine baada ya kumzaa Bwana YESU na kwamba watoto hao waliotajwa hawakuwa watoto waliozaliwa na Mariamu bali walikuwa ni ndugu wengine kama watoto wa mjomba, au baba mdogo ambao walikuwa karibu sana na Mariamu na Yusufu..

Hoja hii ni dhaifu na haina ukweli, kwani kusingekuwa na sababu ya MUNGU kuruhusu Mariamu achumbiwe na YUSUFU kama hawakuwa na mpango wowote wa kukutana na kuzaa watoto huko mbeleni,.. Malaika angeweza kumtokea Mariamu hata kabla hajachumbiwa, na hilo lingeweza labda kutufanya tuamini kuwa Mariamu aliendelea kuwa bikira mpaka anakufa!.

Lakini kitendo cha mpango wa MUNGU kuingilia kati wakati ambao tayari Mariamu kashachumbiwa, na kuonyesha kuwa hao tayari wamekusudiwa kuwa mume na mke na kuzaa watoto, na hata hivyo kipindi ambacho Yusufu amekusudia kumwacha Mariamu kwasababu ya ujauzito wake, bado kulikuwa na nafasi ya Malaika kumruhusu Yusufu amwache Mariamu, na kumruhusu akaoe mwanamke mwingine, ili Marimu abaki bikira maisha yake yote.

Lakini tunaona Yule Malaika hakumruhusu Yusufu amwache mkewe, ikifunua kuwa Yule ataendelea kuwa mke na ataendelea kutumika kama mwanamke mara baada ya kumzaa Bwana YESU.

Kwahiyo Bwana YESU alikuwa na ndugu wengine na Mariamu hakupaa, wala hakufa bikira, bali alikuwa na watoto wengine, na kati ya hao (yaani Yuda na Yakobo) ndio walioandika vitabu vya Yuda na Yakobo vya agano jipya katika Biblia.

Lakini pamoja na kuwa Bwana YESU alikuwa na ndugu wengine katika mwili, bado alisema kuwa ndugu zake hasa ni wale wayafanyayo mapenzi ya Baba yake.

Luka 8:19 “Wakamwendea mama yake na ndugu zake, wasiweze kumkaribia kwa sababu ya mkutano.

20 Akaletewa habari akiambiwa, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje wakitaka kuonana nawe. 21 Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya”.

Je umempokea YESU?, Je Umefanyika kuwa ndugu yake Bwana kwa kulishika Neno lake na kulifanya?

YESU ANARUDI.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Ni halali kubatiza watoto wadogo?

HUYU SI YULE SEREMALA, MWANA WA MARIAMU?

Je! Tutatambuana tukifika mbinguni?

JE BIKIRA MARIAMU ALIKUFA?

Ipi tofauti kati ya Sheria na kanuni kibiblia.

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments