Kwanini Mungu alichagua njia ya kifo cha msalaba kuwa njia ya ukombozi na si njia nyingine?, kwamba hakukuwa na njia nyingine ya ushindi? Amen.
Jibu: Ni kweli, MUNGU hakushindwa kutumia njia nyingine ya ukombozi wetu tofauti na hiyo ya kifo cha mwanawe wa pekee, kwani yeye ni MUNGU anayeweza mambo yote.
Lakini siri ya kwanini KIFO kitumike kama NJIA ya ukombozi wa dhambi ya mwanadamu ni matokeo ya dhambi za mwanadamu.
Bwana MUNGU alimwambia Adamu kabla ya kuasi kuwa pindi tu atakapokula matunda ya mti ule wa ujuzi wa mema na mabaya basi atakufa! (Mwanzo 2:17).. Hilo neno ATAKUFA!… Ndilo linalojibu swali letu, kwanini KRISTO afe ili kutukomboa sisi!.
Maandiko yanasema mshahara wa dhambi ni MAUTI! (Warumi 6:23).. Maana yake ili dhambi iweze kulipwa ni lazima MAUTI ihusike.. Kwahiyo KRISTO alipokuja ili aiondoe dhambi ya mwanadamu ilikuwa ni lazima alipe hilo deni!.
Hata mtu aliyepewa mkataba wa kazi, akiukatisha ule mkataba ni sharti alipe gharama za mkataba ule, na vivyo hivyo Kristo ili akatishe mkataba tuliongia sisi na dhambi, ni sharti alipe gharama za dhambi ambayo ni MAUTI.
Kwahiyo alikikubali kifo ili dhambi iondoke kwetu, na hakukuwa na njia nyingine ya mbadala ya kuondoa dhambi!.
Je umempokea YESU kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yako?
Kama bado hufajanya hivyo, ni heri ukafanya hivyo sasa, kwa maana hizi ni siku na ule mlango wa rehema unakaribia kufungwa.
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Fahamu maana ya 2 Wakorintho 8:9 alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri kwa umaskini wake.
MANENO SABA YA YESU MSALABANI.
YESU MNAZARETI, ANWANI YA MSALABA.
Neno I.N.R.I kwenye msalaba wa Yesu maana yake ni nini?
About the author