Fahamu maana ya 2 Wakorintho 8:9 alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri kwa umaskini wake.

Fahamu maana ya 2 Wakorintho 8:9 alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri kwa umaskini wake.

SWALI: Nini maana ya 2 Wakorintho 8:9

isemayo alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri kwa umaskini wake.

2 Wakorintho 8:9

[9]Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.


JIBU: Katika sura hii mtume Paulo anawaandikia wakorintho juu ya huduma ya utoaji kwa watakatifu walio maskini katika makanisa mengine, ya mbali

Na hapa anawasisitiza kukubali kutoa kwa kufuata kielelezo cha Kristo katika eneo la neema yake..Jinsi alivyokubali kuwa maskini, kwa kuacha enzi na utukufu na mamlaka juu mbinguni, na kuja duniani, katika hali ya chini sana (ijapokuwa hakuwa duni), ili tu atukomboe sisi tulio katika hali ya ufukara wa roho. 

Kwasababu kama asingeweza kujishusha vile, na kukubali kuhesabiwa si kitu (ijapokuwa alikuwa na nguvu), matokeo yake ni kwamba asingekwenda msalabani kusulubiwa kwa ajili yetu tena uchi, na mwisho wake kusingekuwa na  msamaha wa dhambi.

Isaya 53:3

[3]Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. 

 

Lakini sasa tumepokea neema na utajiri wote wa rohoni kupitia yeye kujishusha kwake.

 

Waefeso 1:3

[3]Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; 

Vivyo hivyo Mtume Paulo anawahimiza  Wakorintho waige mfano huo huo, katika eneo la kuwahudumia watakatifu wengine. Akitumia mfano wa Wamakedonia ambao walikuwa ni maskini, na wenye dhiki lakini walikuwa tayari kutoa kwa moyo na furaha kwa watakatifu maskini waliokuwa Yerusalemu.

2 Wakorintho 8:1-3

[1]Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia; 

[2]maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. 

[3]Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao; 

Halikadhalika Bwana anataka na sisi tuhudumiane katika ufahamu wa Kristo, yaani kuwa tayari kuwasaidia watakatifu wengine hata katika hali zetu za dhiki.

Lakini mtazamo ambao si sahihi kuhusiana na vifungu hivi ni kudhani kwamba andiko hilo moja kwa moja linamaanisha  lengo la Bwana Yesu kuwa maskini duniani ni ili sisi tuwe matajiri kifedha. Ni kweli kupitia Yesu, tunabarikiwa mwilini, lakini hicho sio kinachozungumziwa hapo.  Bwana Yesu kuwa maskini ni kutupa utajiri wa roho zetu, pamoja na ule wa ulimwengu ujao.

Bwana akubariki.

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)

Kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi ( 1 Wakorintho 7:14)

Nini maana ya waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo? (Matendo 11:23)

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments