Kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi ( 1 Wakorintho 7:14)

Kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi ( 1 Wakorintho 7:14)

 SWALI: Je! kulingana na mstari huu, watoto wa wapagani hawataokolewa?

1 Wakorintho 7:14

[14]Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.


JIBU: Ukianzia juu utaona andiko hilo linazungumzia juu ya wandoa wanaoishi pamoja lakini mmojawapo hajaamini. Bwana anatoa agizo kwamba ikiwa bado huyo ambaye hajaamini anaona sawa kuendelea kuishi naye, basi yule aliyeamini asimwache.

Kwasababu kwa kupitia njia hiyo, yule asiyeamini hutakaswa na yule aliyeamini Pamoja na watoto wake pia.

Lakini je mstari huo unamaanisha kuwa mwanandoa mmoja katika familia akiokoka, basi ameiponya familia yote mpaka watoto wake?

Jibu ni la! andiko hilo halikumaanisha hivyo.

Bali linamaanisha kuwa, kwa kupitia yeye, ni rahisi wao kuambukizwa imani na hatimaye kufanya uamuzi wa kuokoka.

Wokovu hauji kwa kurithishana au kwa ‘niaba-ya’ bali kwa mtu mwenyewe kufanya maamuzi binafsi mara baada ya kushawishwa na injili.

Hata sasa tumeona shuhuda nyingi watu wakiwavuta ndugu zao kwa Kristo, aidha kwa injili au mienendo yao, na hatimaye wote kugeuka.

1 Petro 3:1-2

[1]Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 

[2]wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. 

Hivyo kwa hitimisho, watu wote, haijalishi wakubwa au wadogo, aidha wa waamini au wapagani, wote wanahitaji kumwamini Yesu ndipo waokolewe dhambi zao. Lakini hiyo huja kwa ushawishi wetu, kwa jinsi tunavyosema nao, tunavyoenenda katika mwenendo wetu mzuri, tunapozifanya nyumba zetu kuwa makao ya ibada, ni njia rahisi ya kuwashawishi.

Bwana akubariki.

Washirikishena akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

je! Paulo aliwalaani Wagalatia na Wakorintho?

UTAYAFIKIAJE MANENO SAFI YA MUNGU?

Matasa ni nini? (1Nyakati 28:17)

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments