USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)

USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)

Jina la Bwana Yesu litukuzwe Daima. Nakukaribisha katika kuyatafakari maneno ya Mungu.

Lipo andiko ambalo tunaweza kuona ni la kinyonge lakini linatiba kubwa sana kama tukilitumia. Embu tuone ni nini mwandishi huyu mwenye hekima  aliomba Kwa Bwana 

Mithali 30:7-9

[7]Mambo haya mawili nimekuomba;  Usininyime [matatu] kabla sijafa. [8]Uniondolee ubatili na uongo;  Usinipe umaskini wala utajiri;  Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. [9]Nisije nikashiba nikakukana,  Nikasema, BWANA ni nani?  Wala nisiwe maskini sana nikaiba,  Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.

Nataka uone hapo aliposema..

“Usinipe umaskini wala utajiri;”

Katika maombi yetu ni rahisi sana kumwomba Mungu asitupe Umaskini, lakini ni ngumu sana kumwomba Mungu  asitupe “UTAJIRI”.. Nadhani huo ndio ukweli..

Utajiri ni Ile Hali ya kuwa na uwezo wa kumiliki au kuwa na vitu vingi.

Lakini huyu mtu hapa anamwekea Mungu mipaka katika maeneo hayo mawili, yaani Utajiri na Umaskini, Kwa lugha nyingine anamwambia Mungu sitaki UTAJIRI.. na sababu anaitoa pale “Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, BWANA ni nani?”

Alijua Kuna madhara ya kuwa na tamaa ya kutaka vitu vingi, mfano kuwa na mabilioni ya pesa kwenye akaunti, kuwa na mahekari ya mashamba mengi, kuwa na nyumba nyingi za kuishi na za kupanga, kuwa na magari mengi n.k. Alijua hayo ni matamanio ya Kila mwanadamu lakini alikataa kuyaomba kabisa.

Lakini Watu wengi tunaposoma huu mstari tunaelekeza mawazo yetu kwenye mambo ya Mali tu. Lakini Bwana anamaanisha pia utajiri wa kiroho.

Uchu huu wa kupata Kila kitu, kuwa na Kila kitu, umewavaa watu wengi hata watumishi wa Mungu. Labda utaona anakwenda mbele za Mungu, maombi yake na matazamio yake ni kuwa na upako kuliko watu wote, anachotaka ni Mungu ampe karama zote za Roho. Yeye naye awe Nabii, awe Mchungaji, awe mwinjilisti, awe mwalimu, awe mtume, awe  na karama zote 9 za Roho. Yaani atakaposimama mimbarani watu wamwone yeye ni kama Yesu. Awe mhubiri wa Dunia nzima wa kimataifa, mwenye mafunuo mengi kuliko wote duniani, mwenye kanisa kubwa kuliko yote duniani.

Maombi ya namna hii ni maombi ya utajiri. Na mara nyingi tunapoomba hivi Bwana Huwa hatupi, kwasababu si mapenzi ya Mungu kuomba vitu vilivyo zaidi ya uwezo wetu alivyotukirimia. Kila mmoja kawekewa kipimo chake na Mungu. Na katika hicho ndio tunaomba Mungu akibariki. Lakini si kila huduma Kila karama itakuwa ni yako.

1 Wakorintho 12:28-30

[28]Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.

[29]Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza?

[30]Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri?

Hivyo pale tunapokuwa na Nia ya kiasi, ndipo Mungu anapotuongezea  neema, na ndio tutakapomtumikia Mungu vizuri. Hekima inatufundisha tubadilishe matamanio. Yetu kutoka katika UCHU, mpaka “kutosheka na mishahara yetu”. Na hivyo tutafanya vizuri zaidi katika huduma, karama, na utumishi wetu Kwa ujumla. Watu watasaidika na kile ulichonacho sasa, kuliko kile usichokuwa nacho unakingoja.

Nabii Eliya ambaye alikuwa ni mkuu Kwa nguvu za Mungu, lakini pamoja na hayo hata katika maombi yake alisema “Mimi SI mwema kuliko Baba zangu (1Wafalme 19:4)”akataka Bwana asitishe huduma yake. Kwasababu aliona kama kipimo kile hakustahili kupimiwa.. Hakuwa na uchu wa kiroho. Si ajabu Kwanini Mungu akamtumia Kwa viwango vikubwa namna Ile.

Bwana atusaidie tuonyeshe sasa bidii katika nafasi zetu alizotukirimia leo, zaidi vile ambavyo tunavitazamia kesho. Tutumike Kwa kadiri ya alivyotujalia.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Mithali 24:17 inamaana gani kusema Tengeneza kazi yako huko nje?

Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)

Bilauri ni nini kibiblia?(Ufunuo 21:11,22:1)

Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?

Nini maana ya Mithali 19:21Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.

Biblia inasema askofu anapaswa awe mume wa mke mmoja! Je! Wale wasiooa kwa ajili ya injili hawawezi kuwa maaskofu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments