Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)

Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)

SWALI: Nini maana ya huu mstari?

Mithali 24:26 “Aibusu midomo atoaye jawabu la haki”


JIBU: Kwa namna nyingine inasomeka hivi “ Atoaye jawabu la haki, ni sawa na mtu abusuye mdomo wa rafiki yake”

Kwa tamaduni za kale za kiyahudi, ishara ya kuonyesha upendo wa dhati kwa mtu ilikuwa ni kubusiana midomo, sio kama sasa inavyotumika kama ishara ya mahusiano ya kimwili.

Na ndio maana katika maandiko utaona mitume wanaagiza watakatifu wasalimiane kwa busu takatifu (Warumi 16:16), halikadhalika utaona Yuda alipomsaliti Bwana alimbusu.

Lakini kwa tamaduni zetu, sasa ishara ya upendo ni kupeana mikono, na mahali pengine kukumbatiana, lakini sio kubusiana.

Tukirudi katika mstari, anaposema, ‘atoaye jawabu la haki’ Yaani mtu ‘anapoamua kwa haki’  au ‘anapozungumza ukweli kwa mwenzake, au kwa jirani yake, bila unafiki au upendeleo, , rohoni anatafsirika kama ni mtu ambusuye rafiki yake, mtu ampendaye rafiki yake sana, kwa kumkumbatia au kumpa mkono.

Tofauti na inavyoeleweka. Na wengi, kwamba ukimweleza mwenzako ukweli, ni kuunda uadui. Lakini Bwana wetu hakulijali hilo, ndio maana japokuwa alichukiwa na viongozi wengi wakidini kwa kuwa kwake muwazi (Yohana 8:40-45), lakini leo hii tunauona upendo wa dhati aliokuwa nao kwetu kwa kufanya hivyo.

Nasi pia Bwana atusaidie tuwe na ‘jawabu la haki’ vinywani mwetu. Tudhihirishe upendo wa kweli.

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.

SAUTI NYUMA YA ISHARA.

MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

Ni nani aliyesema “Nitume mimi”? katika

MIMI SIOMBI KWAMBA UWATOE KATIKA ULIMWENGU.

UNYAKUO WA KANISA UMEPITA LEO!!

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments