MIMI SIOMBI KWAMBA UWATOE KATIKA ULIMWENGU.

MIMI SIOMBI KWAMBA UWATOE KATIKA ULIMWENGU.

Shalom, ulishawahi kuutafakari vizuri huu mstari?

Yohana 17:14 “Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

15 MIMI SIOMBI KWAMBA UWATOE KATIKA ULIMWENGU; bali uwalinde na yule mwovu”.

Embu takafakari, Bwana Yesu anasema sisi(watakatifu), sio wa ulimwengu huu, akiwa na maana kuwa hapa dunia hapatustahili kwa namna yoyote ile, kwasababu sio mahali petu, tunapaswa tukishamwamini tu yeye, tuondolewe, twende zetu mbinguni nyumbani kwetu, lakini wakati huo huo bado anasema, “Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwenguni”..

Yaani kwa lugha nyepesi tunaweza kusema, unapelekwa kwenye nyumba ya mtu mwingine, ambaye itikadi zake na za kwako haziendani kabisa, Na pale unapojaribu kutoka na kurudi nyumbani kwako, unazuiwa,unaambiwa uendelee kubaki pale pale, hakuna kuondoka. Si kazi rahisi kama unavyodhani.

Ndicho anachokifanya Mungu sasa kwa watoto wake, na anafanya hivyo kwa makusudi maalumu. Na makusudi yenyewe ni ili sisi tuiangaze NURU yake kwa walimwengu. ukiokoka, jiandae kuendelea kuishi katika mazingira haya haya ya walimwengu kwa kipindi Fulani kirefu tu.. tukisema ulimwenguni tunamaanisha miongoni mwa waovu, Hilo huwezi kuliepuka. Ni mara chache sana itatokea Mungu kukuweka katika mazingira ambayo utaishi na wapendwa wenzako, mnaoendana.

Utawekwa katikati ya watu wasioendana na wewe kabisa, ukaishi nao, Na pengine umemwomba Mungu mara nyingi akuondoe hapo, lakini unashangaa, ombi hilo halijibiwi,lakini mengine yanajibiwa. Ukiona hivyo likumbuke tu hilo Neno la Bwana Yesu.. “Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwenguni, bali uwalinde na yule mwovu”..

Pengine umeokoka, lakini mazingira ya kazini kwako, hayana utukufu kabisa, umezungukwa na watu waovu na wenye mizaha kila namna, na umemwomba Mungu sana, akufungulie mlango wa kazi nyingine nzuri zaidi yenye wapendwa wenzako. Ndugu kama umeomba sana na bado hujaona jibu lolote, ufahamu kuwa  umewekwa ulimwenguni  Huwezi kuondolewa, unachopaswa kufanya ni kuyatenda mapenzi ya Mungu hapo hapo ulipo, kwasababu huwezi jua kuwa ni Mungu kakuweka hapo ili awaokoe wengine kwa ile nuru yako unayoangaza.

Mtazame Danieli, alipopelekwa kwenye ufalme wa Nebukadreza, alikutana na mambo mengi sana ya kipagani, yanayokinzana na dini ya kiyahudi kwa kila kitu, lakini katika upagani wote ule, alimcha Mungu, na kumdhihirisha, na mwisho wa siku Mungu wake akatukuzwa katikati ya mataifa yote ulimwenguni kupitia yeye.

Hivyo na wewe uliyeokoka, inawezakana kabisa mazingira uliyopo, yasiwe mazuri, unatamani hata unyakuo upite leo uende zako mbinguni, au umetamani Mungu akuchukue uende ukaishi naye milele mbinguni, au unatamani walau akuweke katika mazingira mazuri yenye utulivu Fulani wa kiroho. Jambo unaloliomba ni kweli kabisa ni la ki-Mungu, na ni kweli ingepaswa iwe hivyo. Lakini usivunje moyo pia unapoona ombi hilo halijajibiwa kama ulivyotamani, badala yake, endelea kuyatenda mapenzi ya Mungu hapo mahali ulipo, wahubirie wengine habari njema, wakumbushe juu ya tumaini la uzima wa milele, na mwisho wa siku utakuwa umelitimiza kusudi la Mungu alilolikusudia katika maisha yako. Kwasababu Bwana Yesu hakuomba tuondolewe ulimwengu kwenye maudhi na makwazo, japokuwa alijua kabisa kuwa sisi sio wa ulimwengu huu. Bali alitaka tuendee kuishi nao kwa makusudi hayo waione nuru yake kwa kupitia sisi.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

AHADI YA ROHO ILIYOSALIA SASA KWA KIPINDI CHETU.

ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.

KWANINI MIMI?

Je aliyezungumza na Musa kule jangwani ni Mungu mwenyewe au malaika wake?

KWASABABU MUDA TULIOBAKIWA NAO SI MWINGI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ezra ndambuki, from Kenya Mombasa county
Ezra ndambuki, from Kenya Mombasa county
1 year ago

Hapo nisawa kabisa mwalimu wangu, umenifundisha Jambo jema kabisa
Kumbe wokovu sio rahisi vile tunavyodhania?
Sasa mtumishi wangu niwangapi basi watakao enda na YESU kwa maana mazingira yetu hasa katika makazi yetu, vishawishi, , matani matusi, mizaa kwawingi zimekita.
Naomba usaidizi wa kushinda mambo haya kwakua nimejua ukweli