Nini maana ya “wazimu” katika biblia?

Nini maana ya “wazimu” katika biblia?

Wazimu ni “ugonjwa wa akili”.. Mtu mwenye wazimu ni mtu mwenye matatizo ya akili. Kwahiyo katika maandiko popote palipoandikwa neno wazimu, pamemaanisha mtu mwenye shida ya akili. Na wazimu huu upo katika mwili na vile vile upo katika roho.

Katika mwili ni ile hali mtu anakuwa hajitambui, yaani kwaufupi anakuwa kama kichaa. Mfano wa wazimu wa mwilini katika biblia… ni wakati ule  Daudi alipojigeuza na kujifanya mwenye wazimu..

1Samweli 21:12 “Naye Daudi akayatia maneno hayo moyoni mwake, akamwogopa sana Akishi, mfalme wa Gathi.

 13 Akaubadilisha mwenendo wake mbele yao, akajifanya mwenye WAZIMU mikononi mwao, akakuna-kuna katika mbao za mlango, na kuyaacha mate yake kuanguka juu ya ndevu zake.

14 Ndipo huyo Akishi akawaambia watumishi wake, Angalieni, mwaona ya kuwa mtu huyu ANA WAZIMU; basi, maana yake nini kumleta kwangu?

15 Je! Mimi nina haja ya watu wenye wazimu, hata mmemleta kiumbe hiki ili aonyeshe WAZIMU WAKE machoni pangu? Je! Huyu ataingia nyumbani mwangu?”

Lakini wazimu katika roho ni ile hali ambayo mtu anakuwa hajitambui katika roho, anakuwa anaonyesha tabia za utahira katika mambo ya rohoni, hawezi kuyaelewa wala kuyapambanua, anakuwa anafanya mambo ya ajabu ajabu tu katika roho, sawa na mtu mwenye wazimu katika mwili, mifano wa watu  kwenye maandiko waliokuwa na wazimu wa rohoni ni Balaamu na Kaini.

Balaamu alifikia hatua ya kuongea na punda, halafu hata hashangai!, wala kujiuliza!…Inakuwaje kuwaje punda anaongea…na yeye bila kufikiri akawa anajibizana na punda!, jambo ambalo ni la kiwazimu.. mtu mwenye akili zake timamu za kiroho, hawezi kuonyesha hizo tabia…

Hesabu 22:27 “Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajilaza chini ya Balaamu; hasira yake Balaamu ikawaka, akampiga punda kwa fimbo yake.

28 Bwana akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi?

  29 Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi”.

Hivyo Balaamu alikuwa ni mfano wa watu wenye wazimu wa rohoni, na hata biblia inasema hivyo katika…

2Petro 2:15 “wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu”.

lakini alikaripiwa kwa uhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia WAZIMU WA NABII YULE”.

Vile vile, Kaini alikuwa na wazimu, kwasababu mtu mwenye akili timamu za rohoni, hawezi kujibizana na muumba wake, lakini Kaini aliweza kufanya hivyo..

Mistari mingine inayozungumzia wazimu wa rohoni ni pamoja na 1Timotheo 6:4, kumbukumbu 28:28, Zekaria 12:4, na Yeremia 25:16.

Bwana atusaidie na kutuepusha na wazimu, hususani wa kiroho ambao ndio mbaya zaidi..kwasababu huo unatufanya tusiweze kupambanua wala kuelewa mambo ya rohoni. Ambayo madhara yake ni kifo kiroho. Tusiwe kama Kaini au Balaamu.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Je mtu anayeua anabeba dhambi zote za yule aliyemuua?

WAOMBEENI WANAOWAUDHI.

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.

JE! UNAIONA ILE NCHI NZURI YA KUMETA-META MBELE YAKO?

Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni  ipi?

CHAPA YA MNYAMA

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments