Jibu: Tuanzie ule mstari wa kwanza..
2Timotheo 4:1 “Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;
2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, KARIPIA, KEMEA, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho”.
“Kukaripia” ni kulaani au kukosoa kosa lilolofanyika… Kwamfano mama anaweza kumkaripia mwanae kwa tabia ya Uvivu, kwamba aiache hiyo tabia, kwani ni mbaya na itamletea madhara huko mbeleni..na kukaripia mara nyingi kunaambatana na kutoa elimu,ushauri au darasa juu ya hilo kosa..
Lakini “Kukemea” inaenda mbali zaidi, kwani kunahusisha kulaani kitendo kibaya na kutoa amri ya zuio ya jambo hilo lisiendelee kutokea… Kwamfano Mama anaweza kumkemea mwanae kwa kosa la Wizi, Kwamba tendo hilo ni kosa na lisirudiwe tena! (hiyo inakuwa ni amri, sio ombi tena wala ushauri).
Serikali inaweza kukemea vitendo vya mauaji, ubakaji au rushwa.. kwamba vitendo hivyo ni vibaya na havipaswi kutendeka kwani ni uvunjifu wa sheria, hivyo kutofanya hayo ni amri na sio ombi wala ushauri..
Na katika Biblia, Neno la Mungu linatuagiza “Kukaripia” na “Kukemea”
2Timotheo 4:2 “lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, KARIPIA, KEMEA, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho”.
Zipo tabia au mienendo iliyopo kati ya watu ambayo kiuhalisia inahitaji “kukaripiwa” na mingine “kukemewa” na Neno la Mungu linatufundisha kufanya hivyo bila kuogopa pale inapobidi. (hususani ndani ya kanisa)
Kwamfano vitendo vya wivu, uvivu, uzembe, utegeaji ndani ya kanisa, (hivyo katika hali ya uchanga vinaweza kukaripiwa tu na vikaisha), lakini vinapozidi mipaka vinapaswa vikemewe!.
Lakini vitendo vingine kama vya Ulevi, Uchawi, uzinzi, uasherati, wizi, utukanaji, fitina na vingine vinavyofanana na hivyo, havihitaji kukaripiwa bali KUKEMEWA, kwamba visiendelee kufanyanyika na hiyo inakuwa ni “Amri” na sio “Ombi wala ushauri”, maana yake mtu akiendelea kufanya hayo makusudi baada ya kuonywa mara nyingi, ni haki yake kutengwa kwa muda mpaka atakapojirekebisha ili asilichafue kanisa la Kristo.
1Wakorintho 5:11 “Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
12 Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani?
13 Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu”.
Hapo anaposema “ndugu” anamaanisha Ndugu katika Imani (mkristo), hususani Yule ambaye tayari analijua Neno la Mungu, lakini hataki kubadilika yuko vile vile ndani ya kanisa ni mlevi, au mzinzi, au mwizi, huyo kama amekemewa na hakubali kubadilika, Biblia imetoa ruhusa ya kumtenga kwa muda, ili asilichafue kanisa..
Lengo la kumtenga ni ili atafakari na asione kanisani ni mahali pa kufanyia mchezo, au pango la wanyang’anyi.. Akifanyiwa hivyo itampa muda wa kutafakari na kama ni mtu wa kujali basi atatambua makosa yake na kujirekebisha na hivyo atarudishwa kanisani… Lakini kwa wale wengine walioingia kwenye wokovu hivi karibuni (ambao bado ni wachanga) hao hawawezi kutengwa wanapofanya makosa yale yale waliotokea nayo duniani kwani bado ni wachanga wanahitaji kufundishwa zaidi..Lakini kwa wale wengine waliokaa miaka na hawabadiliki, Neno limeruhusu kuwatenga kwa muda.
Hivyo kwa hitimisho ni lazima kukaripia mabaya, lakini pia kukeme na kuonya pia..Kwani hata Bwana Yesu Kristo huwa anatukemea pale tunapoondoka kwenye njia (Ufunuo 3:19)
Neno hilo “Kukemea” linaweza kutumika pia katika kutoa pepo, kwasababu pepo anapokuwa ndani ya mtu, huwa anamtesa Yule mtu, na si haki yake kumtesa.. hivyo tunapoamuru pepo atoke ndani ya mtu maana yake tunatoa “AMRI” sio “Ombi”.. kwamba hizo shughuli zake anazozifanya ndani ya mtu, zisimame na amtoke Yule mtu, Pepo hatulikaripii bali tunalikemea (Luka 9:42)
Bwana atubariki na kutusaidia sote.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MAMBO MANNE(4) YAFANYAYO NENO LA MUNGU.
Vita vya kiroho, na mwamini Mpya.
Yesu alikuwa na maana gani aliposema ‘tena siku ile hamtaniuliza neno lolote (Yohana 16:23)
NAYE ALIKUWA HANA BUDI KUPITA KATIKATI YA SAMARIA.
Kumwambia mtu mwenye dhambi kuwa atakwenda kuzimu asipotubu Je! ni kuhukumu?
About the author