MAMBO MANNE(4) YAFANYAYO NENO LA MUNGU.

MAMBO MANNE(4) YAFANYAYO NENO LA MUNGU.

(Masomo maalumu kwa wahubiri).

Kama Mhubiri basi fahamu mambo haya manne..

2 Timotheo 3:16 “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki”.

Nataka tuone mambo haya manne (4), ambayo Neno la Mungu linafanya, ili tusikose shabaha katika utumishi wetu.

Hapo anasema “kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa MAFUNDISHO, na KUONYA na KUONGOZA na KUADIBISHA”

Na hakusema kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa “kuchekesha na kuburudisha na kuchangamsha na kusisimua”

Hebu tuangalie jambo moja baada ya lingine ambalo Neno la Mungu linafanya.

  1. KUFUNDISHA.

Hapo Neno linasema “..lafaa kwa mafundisho”.. sasa mafundisho yanayozungumziwa hapa si yale ya jeografia au sayansi bali  ya yale ya Uzima (yampayo mtu uzima wa roho yake).

Tito 2:1 “Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima”.

Mafundisho yenye uzima ni yale yote yamtoayo mtu katika mkondo wa dhambi, kwani dhambi ndio adui wa kwanza wa mtu alitaye mauti (Warumi 6:23).

Hivyo msingi wa mafundisho ya kila mhubiri ni lazima yategemee Neno la Mungu (yaani biblia).

2. KUWAONYA WATU MAKOSA YAO.

Kuna tofauti ya kuonya na kuhukumu. 

Kuhukumu ni kutoa tamko la mwisho la mwenendo wa mtu, jambo ambalo ni Mungu pekee ndiye awwzaye kufanya..

Lakini “Kuonya” ni kumtahadharisha mtu kuhusiana na hatari iliyopo mbele yake kulingana na mwenendo anaoenda nao, ikiwa hatabadilika.

Kwamfano mtu anayeiba, ukimwambia aache wizi na ukamfahadharisha madhara yake kuwa yanaweza kumpelekea hata kifo (kuchomwa moto na watu)....hapo hujamhukumu bali umemwonya.

Na vivyo hivyo unapomtahadharisha mtu kuhusiana na madhara ya kuiba au dhambi/mwenendo mwingine wowote ulio mbaya kwamba ataenda kuchomwa kwenye moto wa milele kama asipobadilika hapo hujamhukumu bali umemwonya, na ndio kazi ya Neno la Mungu lenye pumzi ya uhai, ni kuwaonya watu makosa yao.

2 Timotheo 4:2 “lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho”.

Na kuonya inapaswa iwe sehemu ya mahubiri kwa kila mhubiri ya kila siku..

 Waebrania 3:13 “Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi”. 

Wapo watu wasemao kuwa zisihubiriwe sana habari za hukumu ijayo kwani kwa kufanya hivyo ni kuhukumu na kuwatisha watu.

Ni kweli mambo yajayo yanatisha, lakini sasa yamewekwa wazi katika biblia pasipo vificho, sasa kama kwenye biblia imeyaweka wazi pasipo mafucho kuna haja gani ya mhubiri kuyaficha??.

Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Soma tena Wagalatia 5:19-20 na 1Wakorintho 6:9 utaona mambo hayohayo.

Kwahiyo kama mhubiri Onya, karipia na kemea.

3. KUONGOZA.

Biblia inasema Neno la Mungu ni mwanga na taa ya njia yetu (Zaburi 119:105). 

Kama vile taa inavyoweza kumwongoza mtu katika giza nene vivyo hivyo na Neno la Mungu.

Mtu anaposikia Neno la Mungu na kulitii basi lile Neno linakuwa ni dira ya maisha yako, na mwongozo sahihi wa namna ya kuishi.

Kwasababu ndani ya biblia kuna mwongozo sahihi wa namna ya kuishi duniani, ( kiroho na kimwili)..

Zaburi 119:9 “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? 

Kwa kutii, akilifuata neno lako”

4. KUADIBISHA.

Kuadibisha maana yake ni kumfanyaa mtu awe na adabu.

Ili mtu awe na adabu katika mwenendo ni sharti apokee Neno la Mungu lenye uzima, na ni lazima kila mtu aliyempokea Bwana YESU awe na adabu.

Warumi 13:12 “Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. 

13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu”.

 1 Wathesalonike 4:12 “…mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote”.

Bwana atusaidie tuyafanye hayo na zaidi ya hayo, tuwapo katika kufundisha au kuhubiri, vile vile tuadibike, na kuonyeka, na kufundishika na kuongozeka tusikiapo Neno la MUNGU.

Maran atha!.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; (Mithali 11:16)          

Adabu ni nini biblia?

HERI, WALE MUNGU ASIOWAHESABIA MAKOSA YAO.

MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.

MAFUNDISHO YA NDOA.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments