Adabu ni nini biblia?

Adabu ni nini biblia?

Adabu, ni kitendo cha kuonyesha staha, kufuata miiko, kuonyeshaAdabu ni nini biblia? ustaarabu mzuri kwa wengine.

Adabu huonyeshwa kwa Mungu, lakini pia kwa wanadamu.

Adabu kwa Mungu.

> Ni pamoja na mwonekano wako uwapo ibadani.

Yesu alipomwona Petro akiwa uchi alijivika vazi lake kwasababu alitambua anahitaji kuonyesha adabu kwa Mungu wake. (Yohana 21:7).

 >Ni pamoja na kuwa mtulivu: Uwapo ibadani, mazungumzo ya ovyo, yasiyo ya kiibada yaepuke, minong’ono madhabahuni kwa Mungu acha, kuchati, mizunguko zunguko, kutafuna tafutana.havihitajiki,

Adabu kwa wanadamu:

>Ni pamoja na Kuwasalimia wengine. Yesu alisema.

Mathayo 5:47  Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? 48  Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

>Vilevile ni pamoja na kuwasikiliza wengine, kuzuia kinywa chako kunena zaidi ya wastani (Kiasi), kuonyesha upole, kuonyesha kujali, kuonyesha maadili, na kutojishughulisha na mambo ya wengine.

Maandiko yanatufundisha tunda mojawapo la upendo ni adabu.

1Wakorintho 13:4  Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5  HAUKOSI KUWA NA ADABU; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya.

>Vilevile Imetoa agizo kwa wanawake wacha Mungu,kwamba pambo lao mojawapo liwe ni adabu nzuri (1Timotheo 2:9). Ambapo huusisha pia Uvaaji wako kilemba uwapo ibadani ni adabu kwa Mungu wako kwasababu maandiko yameagiza hivyo. (1Wakorintho 11:5). Kujisitiri kwako ni adabu pia.

Lakini zaidi sana imetoa  agizo kwa watawakatifu wote, tuenende kwa adabu kwa wale walio nje (1Wathesalonike 4:12).

Hivyo, sote kwa pamoja tuipe adabu nafasi maishani mwetu,ili tujengwe.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; (Mithali 11:16)

Chamchela ni nini kwenye biblia?(Zaburi 58:9, Amosi 1:14)

UMETEKWA NA UPENDO WA KRISTO?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments