Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; (Mithali 11:16)          

Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; (Mithali 11:16)          

Huu ni mwendelezo wa Mafundisho maalumu yawahusuyo wanawake.

Mithali 11:16          

[16]Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; ..”

Ujumbe huu ni kwako wewe binti/Mama/ ambaye unapenda kuheshimiwa na Mungu pamoja na wanadamu.

Kumbuka  heshima inatafutwa na si wote wanayo, kwasababu inagharama yake kuipata…heshima sio uzuri, heshima sio elimu, sio u-kisasa, wala sio pesa..Ni thamani yako ya ndani, inayoonwa na wengine.

Dada Ukitaka kufahamu ni nini kitakupa heshima usiwafuate mabinti wenzako,la! Hata na  akili zako pia usizifuate, Bali mtafute aliyekuumba ili akupe siri ni nini kitakuthaminisha hapa duniani kwa wanadamu.

Inatia huruma kuona, mabinti wengi wanadhani wanaheshimiwa kwa urembo wao..hivyo hubuni kila namna ya kujipamba, na kujichubua ngozi zao, wanavaa mawigi na makucha ya bandia, kisha kwa ujasiri wanatembe mbele ya watu..wakidhani kuwa ndio wanaonekana watu wa maana sana kwenye jamii..Ukifanya hivyo Binti umepotea!

Wanadhani kuonyesha miili yao barabarani, na kujifanya wakisasa ni heshima, dada hapo huheshimiwi unasanifiwa tu. Unachofanya ni kujiongezea nafasi tu ya kuwa kiburudisho cha macho ya wahuni..na ndio maana watakupigia miluzi na kukutazama tazama.mara mbili ili kesho urudie kufanya hivyo tena, wajiburudishe macho yao, lakini zaidi ya hapo wewe la FELIA…

Hivyo fahamu heshima yako inatoka wapi..

Biblia inaeleza heshima ya mwanamke inakuja katika mambo haya  saba

  1. Kumcha Bwanari
  2. Adabu
  3. Upole
  4. Kiasi
  5. Utulivu
  6. Kujisitiri
  7. Utiifu

Yote haya utayasoma katika vifungu hivi:

Mithali 31:30

[30]Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;  Bali mwanamke AMCHAYE BWANA, ndiye atakayesifiwa.

1 Timotheo 2:9-11

[9]Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa MAVAZI YA KUJISITIRI, pamoja na ADABU nzuri, na MOYO WA KIASI; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

[10]bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.

[11]Mwanamke na ajifunze katika UTULIVU, AKITII kwa kila namna.

1 Petro 3:3-4

[3]Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;

[4]bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya UPOLE NA UTULIVU, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

Ukiyazingatia haya binti/mwanamke, heshima itakufuata yenyewe…na lolote ulitamanilo kwa Mungu utalipata tu..Kama ni mume bora Mungu atakuletea, tena zaidi ya matarajio yako kama Ruthu alivyoletewa Boazi, 

Kama ni kibali, utakipata tena cheo kikubwa zaidi ya wengi, ikiwa ni utumishi, Bwana ataizidisha karama yako pakubwa sana..Na zaidi ya yote una uzima wa milele. Hata ukienda mbinguni unawekwa kuwekwa kundi moja na akina Sara na Ana na Debora, Mariamu, na wanawake wote mashujaa walioishindania imani ipasavyo.

Lakini kinyume chake ni kweli, usipoyashika hayo, utafanana tu na Yezebeli na ukienda kuzimu utawekwa kundi moja na yeye.

Usiiuze heshima yako.

Jithamini.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)

USHAURI KWA MWANAMKE WA KIKRISTO.

Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?

Wanaowachukua wanawake wajinga mateka ni akina nani?

Kama Malkia Esta alijipamba je! Kuna ubaya gani wanawake wa wakikristo wa leo kujipamba?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments