Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?

Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?

SWALI: Naomba kufahamu ni kwa nini katika mikutano mingi ya injili na sehemu za makusanyiko kama mashuleni na sehemu zingine Wanawake ndio hupatwa sana na kusumbuliwa na mapepo?


JIBU: Sababu kubwa ya tatizo hilo ni kitu kinachoitwa “maumbile”. Jinsi Adamu alivyoumbwa ni tofauti na Hawa alivyoumbwa biblia inasema hivyo…Hawa aliumbwa kama msaidizi..alitoka ubavuni mwa mwingine..Kwahiyo ni Dhahiri kuwa kwa namna moja au nyingine yule aliyetoka kwa mwenzake atakuwa dhaifu kidogo kuliko yule muhusika mwenyewe (yaani Adamu) 1Petro 3:7.

Ndio maana unaona mtu wa kwanza kuingiliwa na mapepo pale Edeni alikuwa ni Hawa, na huyo ndiye aliyeharibu mambo yote na kusababisha tuwe hivi tulivyo leo. Na biblia inasema Adamu hakudanganywa bali Hawa. Na ndio sababu biblia imesema wanawake wawe watulivu makanisani na pia hawana ruhusa ya kufundisha. Kwasababu kama wakiachiliwa kuongoza kundi makanisani ni rahisi kwa adui kutumia milango hiyo kama vile Hawa alivyotumika pale Edeni.

Kanisa la kwanza lilianzia pale Edeni, utukufu wa Mungu ulikuwa unashuka wakawa mpaka wanamwona Mungu uso kwa uso..lakini pepo likamwingia Hawa na kumdanganya kuharibu mambo yote….si Zaidi sasahivi?,… kumbuka Hawa aliumbwa pasipo dhambi ya asili hata kidogo lakini aliyaharibu mambo…. si Zaidi uliyezaliwa leo mwenye dhambi ya asili?.

1Timotheo 2:11 “Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.

12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. 13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.

14 WALA ADAMU HAKUDANGANYWA, ILA MWANAMKE ALIDANGANYWA KABISA akaingia katika hali ya kukosa”.

Lakini leo utaona wanawake wachungaji?..Jambo ambalo ni kinyume na maagizo ya Mungu…utasema mbona anajua tu kuhubiri na watu wanaokoka, mbona anaombea watu wanapona, mbona anatoa unabii na unatokea?..hicho sio kigezo!…hata mtu aliyemwasherati anaweza kuhubiri na watu wakaokoka?. Bwana Yesu alisema wengi watakuja siku ile na kusema Bwana hatukutoa pepo kwa jina lako? Hatukutoa unabii kwa jina lako? Lakini atawaambia siwajui mtokako!..Maana yake ni kwamba kutoa pepo, au kujua kuhubiri kwa kupangilia maneno sio kigezo cha mtu kukubaliwa na Mungu…bali kutenda mapenzi ya Mungu ndio kigezo cha kukubaliwa. Kutii Neno lake, Kasome (Mathayo 7:21-23).

Ni rahisi kutafuta maandiko machache machache kuchomeka ili kutetea hoja hiyo ya wanawake kuwa wachungaji…lakini maandiko yamesema wazi… “wanawake wawe watulivu”. Ila kama wewe au mimi tunajiona tunajua Zaidi au watu wa rohoni Zaidi na kuhisi kwamba pengine Mungu ana upendeleo fulani, au pengine alikuwa hamaanishi vile alikuwa anamaanisha vingine kusema vile..Hivyo sisi ni watu wa rohoni sana…Basi mstari huu unaweza ukatufaa Zaidi.

1Wakorintho 14: 34 “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.

35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.

36 Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?

37 MTU AKIJIONA KUWA NI NABII AU MTU WA ROHONI, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.

38 Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga”.

Neno linatuambia kama TUKITAKA KUWA WAJINGA, na tuwe wajinga!..Kama tunataka kuendelea kuwa wajinga kulazimisha kwamba anachoweza kukifanya mwanamke na mwanamume naye anaweza kukifanya pia, au anachoweza kukifanya mwanamume na mwanamke anaweza…basi tumepewa ruhusa ya kuendelea kuwa wajinga hivyo hivyo…

Lakini wanawake na wanaume wanaolisoma Neno na kulielewa sio wajinga. Wanalitii Neno la Mungu na kulifuata.

Bwana atusaidie sana.

Ubarikiwe.

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia masomo kwa njia ya whatsapp ya kila siku basi, bofya hapa uweze kujiunga >>> WHATSAPP Au tuandikie kwa namba hizi +255789001312

Mada Nyinginezo:

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.

RABONI!

MARIAMU

MARIAMU AKUTANA NA ELISABETI.

WALE WAZEE ISHIRINI NA WANNE (24), WANA KAZI GANI?

MUNGU AKIKUPITA LEO, HAIMAANISHI KUWA HAJAKUCHAGUA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments