WALE WAZEE ISHIRINI NA WANNE (24), WANA KAZI GANI?

WALE WAZEE ISHIRINI NA WANNE (24), WANA KAZI GANI?

Wale wazee ishirini na wanne na akina nani na kazi yao ni ipi?


Kama wengi wetu tunavyofahamu Malaika watakatifu wamesifika kwa kazi moja kuu nayo ni kumsifu Mungu na kumwimbia, lakini mbali na sifa hiyo wamepewa pia kazi nyingine maalumu ya kufanya nayo ni ile ya kuwahudumia watakatifu..

Waebrania 1:14 “Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?’’

Sasa hapa kwenye kuwahudumia watakatifu wengi tunadhani ni kuwalinda watakatifu dhidi ya adui tu basi..Lakini nataka nikuambie sio tu kuwalinda peke yake, vipo na vipengele vingine sana ambavyo Mungu akitufunulia tutashangaa sana, tutasema hata na hiki?.

Tukisoma Ufunuo sura ile ya 4 na ya 5 tutaona Yohana, akipewa neema ya kipekee ya kufunguliwa malango ya Mbinguni na kuonyeshwa kwa wazi mambo yaliyomo kule, na mfumo wake mzima jinsi ulivyo na ngazi zake zote zilivyo jipanga kabla ya kumfikia Mungu mwenyewe. Jambo ambalo hata Ezekiel hakuonyeshwa kwa uwazi kama alivyoonyeshwa Yohana, Kama ukisoma pale utaona picha nzima iliyopo ni kwamba kabla hujakifikia kile kiti cha enzi, utakutana kwanza na jeshi la malaika watakatifu maelfu kwa maelfu wamepazunguka pale kwenye enzi ya Mungu.

Kisha utaona tena katikati ya wale malaika, wapo wazee ishirini na wanne (24), wamekizunguka tena kile kiti cha enzi, na katikati ya wale wazee ishirini na wanne (24), wapo wale wenye uhai 4 waliojaa macho mbele ya nyuma (Ufunuo 4:6), na katikati ya wale wenye uhai wanne kipo kiti cha enzi cha Mungu mwenyewe.

Ufunuo 5:11 “Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,

12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na Baraka”.

Sasa tofauti na wengi tunavyodhani kuwa wale wazee ishirini na nne 24 (ni) wale watoto 12 ya Yakobo, na wale mitume 12 wa Bwana Yesu, ambao jumla yao ni 24. Lakini Mtazamo huo sio sahihi, Yohana akiwa mmoja wa mitume wa Bwana akiwa duniani hawezi kujiona tena mbinguni, ameketi na tena ameshikilia maombi ya watakatifu..Uona hilo haliwezekani.. kitendo cha wale kuitwa wazee haiwafanyi wao kuwa wanadamu..Tutaliona hilo muda mfupi mbeleni kidogo.

Kumbuka Mungu kawaumba malaika na maumbile mengi tofauti tofauti kulingana na kazi zao walizowekewa kuzifanya kwa ajili yetu sisi..Na Hawa wazee ishirini na nne (24) ni aina nyingine ya malaika watakatifu. Ambao wamechukua mfano wa wazee kwa maumbile yao, kama tu wale wenye uhai wanne, walivyokuwa na mfano wa viumbe vinne tofauti, ambapo wa kwanza alikuwa mfano wa simba, hiyo inamaanisha kuwa zipo tabia za simba waliziwakilisha, mwingine mfano wa ndama, wakiwakilisha tabia ya ndama achinjwaye, mwingine mfano wa sura ya mwanadamu, na mwingine mfano wa tai arukaye..wote hao waliwakilisha tabia Fulani zinazofanana na hao wanyama katika kuwahudumia watu..

Ukisoma juu ya ufunuo wa ile mihuri saba ndipo utafahamu vizuri ni jinsi gani maumbile yao yalifunua kazi za katika kanisa kwa kipindi husika..Na kama ulikuwa hujafahamu bado wakati huu tuliopo wa kanisa tupo chini ya mafuta ya mwenye uhai wa nne ambaye anafananishwa na tai arukaye..Tai ni mnyama anayeona mbali, na manabii wa Bwana wanafananishwa na Tai,..Katika wakati huu tunaoishi sasa, kama hutapewa jicho la TAI la kuona mbali, utachukuliwa na maji na udanganyifu wa shetani unaoendelea sasa hivi kwa kasi..

Kama hujapata kujua ufunuo wa kitabu kile cha mihuri saba, basi utanitumia ujumbe inbox nikutumie somo lake.

Sasa tukirudi kwa wale wazee ishirini na wanne (24), hawa wanaoonekana kama wazee, Ni kundi lingine la malaika wa Mungu wenye mfano wa tabia za wazee, siku zote wazee wanasifika kwa kuwa na hekima, na ndio wanaopewa kipaumbele katika mashauri, na viti vya mbele hata leo hii washauri wa Raisi asilimia kubwa ni wazee, hiyo yote ni kwasababu ya uzoefu wao katika mambo mengi na hekima..

Vivyo hivyo na kundi hili la malaika hawa, ni malaika Mungu aliowachagua, kuizunguka enzi yake, na kwa kupitia hao Mungu alichagua maombi ya watakatifu yapitie kwanza kwao, kisha kwa mwana-kondoo na moja kwa moja kwake. Si kila jukumu wamepewa malaika wote, wapo malaika wanaohusika na kupigana na sisi vitani kama Mikaeli na malaika zake, wapo wajumbe kama Gabrieli, wapo wanasimama kwa kila huduma, kama ilivyokuwa kwa Petro, na Paulo, biblia inasema walikuwa na malaika zao.

Vilevile na wazee ishirini na wanne (24), ni malaika waliokaribu sana na Mungu, kupeleka mashauri yao na hoja zao zenye hekima.

Ufunuo 5:8 “Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.

9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa”,

Moja ya jambo ambalo Mungu analiheshimu ni pale anapoona malaika zake watakatifu wanashiriki katika kuyawasilisha maombi yetu kwa Mungu..Na ndio maana Bwana Yesu alisema..

Mathayo 18:10 “Angalieni msidharau mmojawapo wa wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni”

Hivyo ndivyo malaika wanavyofanya kazi usiku na mchana kuwahudumia wale watakaoukiri wokovu. Leo hii ukimkosesha, au ukimdharua mtakatifu ambaye ni mchanga kiroho ukamzuia asiendelee katika njia yake ya utakatifu..Jiangalie sana, Mungu anawasikiliza malaika zake kushinda hata wewe unavyoweza kufikiri.. wakipeleka mashtaka mabaya kwako mbele zake, sijui ni nini kitakupata, Na ndio maana wanajizuia wakati mwingine kufanya hivyo..soma

2Petro 2:11 “Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu; ijapokuwa malaika ambao ni wakuu zaidi kwa uwezo na nguvu, hawaleti mashitaka mabaya juu yao mbele za Bwana.

12 Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;

Hivyo kama wewe ni mtakatifu basi furahi kwasababu mbinguni unatazamwa sana. Lakini ikiwa wewe upo nje ya Kristo, unatazamia vipi maombi yako yatamfikia Mungu ukiwa katika hali hiyo, ni nani yupo upande wako kukusaidia?, Unategemea vipi Mungu akutumie malaika zake wakulinde?, Unategemea vipi Mungu akusikie wewe. Huoni kuwa maisha yako yapo hatarini. Leo hii shetani akisema ninaitaka roho ya huyu mtu, ni nani atakutetea, Kristo hayupo upande wako, vilevile na malaika zake hawapo upande wako.

Usisubiri Mungu awatumie malaika hawa kukuletea mapigo, Kwasababu upo wakati utafika huduma yao itakuwa imeisha kwa watakatifu. Watapewa kazi nyingine mpya ya kuleta mapigo juu ya hii dunia kama tunavyosoma katika Ufunuo 16, usitamani uwepo huo wakati, kwasababu watu watatamani kifo na kifo kitawakimbia jaribu kufikiri dunia nzima maji yanakuwa damu, jua linashushwa kuwaunguza watu, majipu mabaya ambayo hayajawahi kutokea yanawakuta watu, visiwa vinahama, mwezi unakuwa mwekundu kama damu..Jiulize siku hiyo utakuwa katika hofu kiasi gani…Ukijua kuwa baada ya kufa kwako utakwenda kuzimu moja kwa moja.

Leo dunia ipo katika amani hii ni kwasababu ya neema zake tu utubu. Kwasababu hapendi mtu yeyote apotee..Huu si wakati wa kuitazama dunia tena, bali Mungu hatuna muda mrefu hapa,..parapanda saa yoyote inalia….Ikiwa upo nje ya Kristo na leo hii unasema sitaki tena kuendelea kuishi maisha haya ya kuwa hatarini, basi uamuzi unaoufanya ni sahihi..

Kama upo tayari kufanya hivyo sasa kwa kumaanisha kabisa na wala si kwa kujaribu… Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha sasa ukiwa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI, NAYE NDIYE MFALME ATAKAYEKUJA. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithibitisha toba yako kwa Vitendo. Ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo kuanzia sasa hivi, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Fanya kwanza hayo na YESU KRISTO ataanza kutembea na wewe katika maisha yako kwa namna ya ajabu sana, Nawe pia utaingizwa katika jumuiya hii ya watoto wa Mungu, ambayo Mungu na dunia zinafanya kazi na wewe.

Ubarikiwe.

Tafadhali “Share” Ujumbe huu na kwa wengine. Vilevile kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email au whatsapp, tutumie ujumbe au piga namba hii 0789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

UFUNUO: Mlango wa 4

UFUNUO: Mlango wa 5

UFUNUO:Mlango wa 6-( Maelezo ya Muhuri saba)

Nifanye nini ili niwe na uhakika nikifa naenda mbinguni?

JIHADHARI NA KUOSHWA MIGUU ISIVYOPASWA.

Kwanini kila nikitaka kusali naingiwa na uvivu?

JE! WATOTO WACHANGA WANAWEZA KUHUKUMIWA NA KUTUPWA MOTONI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
9 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
William Ndunda
William Ndunda
1 year ago

Ahsante kwa ufunuo huo… Mwenyezi Mungu akubariki

Fausta Clemence
Fausta Clemence
2 years ago

Kwa Kweli mie Nahitaji kujifunza litany hiki Kwa nguvu na kwa moto mpk nikielewe vizuri sana mamba yako plz

ahimeleki waziri
ahimeleki waziri
1 year ago
Reply to  Admin

0752919403

Jacobo peter
Jacobo peter
2 years ago

Kwani, maono hayo yohana aliyaona kipindi gani? Au nyakati zipi?

William Msanya
William Msanya
4 years ago

Mada iko vizuri namshukuru Bwana kwa kukutumia vizuri kutupatia mafunuo haya ubarikiwe mtumishi