SWALI: Nifanye nini ili niwe nina uhakika kuwa hata nikifa ghafla leo hii, nina uhakika wa kwenda mbinguni kwa asilimia zote?
JIBU: Moja ya swali ambalo ukiwauliza wakristo wengi watakujibu kirahisi ni kuhusu kuokoka..Ukimuuliza Je! Umeokoka atakuambia ndio nimeokoka, lakini ukimuuliza, Ikitokea mfano umekufa ghafla leo Je! unao uhakika wa kwenda mbinguni?..Hapo ndipo utakapopata majibu tofauti tofauti, wengine watasema, siwezi kusema hilo Mungu ndio anayejua, wengine watasema kwa kweli hapo sijui, wengine watasema mimi sio Mungu na wengine watesema “natumaini” nitakwenda mbinguni, wengine watasema “ninaamini” itakuwa hivyo..Na wachache sana watasema ninao uhakika nitakwenda mbinguni..
Na katikati ya hao wachache wanaosema ninaohakika, ukiwauliza swali ni kipi kinakupa uhakika huo wa kwenda mbinguni, wengine wanatasema kwasababu ninaishi katika Maisha ya toba kila siku.
Lakini biblia inatuambia kila aliyemwamini mwana wa Mungu ni lazima awe na uhakika ya kuwa anao uzima wa milele ndani yake, na kwamba hata akifa leo atakuwa anaishi..
1Yohana 5:13 “Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu”.
Sasa wengi wanakosa Uhakika huu kwasababu hawajakamilishwa katika IMANI ya YESU KRISTO. Na ndio hapo utaona mtu anasema nimeokoka lakini bado anayo hofu akifa leo hajui atakwenda wapi, motoni au mbinguni? Maisha ya kubahatisha. Wengi hawafahamu kuwa Kuokoka ni Neno lenye maana pana sana, na hivyo sio suala la kuongozwa sala ya toba tu na kubaki kama ulivyo. Kuokoka ni jambo linaloleta badiliko ndani ya Maisha ya mtu. Bwana Yesu anafanya kazi ya kuyageuza Maisha ya mtu mpaka mtu huyo anafikia kiwango cha kupata uhakika wa uzima wa milele mwenyewe ndani yake bila hata ya kujilazimisha, au kihisihisi kama anao au hana..Ndani yake kunabubujika uzima wa milele.(Yohana 4:14)
Ni hatua (process)..sio tu kuongozwa sala Fulani ya toba halafu unaendelea kuishi Maisha ambayo ni kinyume na Kristo, halafu ukadhani uhakika huo utakuja wenyewe ndani yako.
Na hiyo inakuja kwa kuyatii maagizo yote Bwana anayompa mtu baada ya kutubu kwake. Akikuambua unapaswa ukabatizwe katika ubatizo sahihi mara baada ya kuokoka kwako, unatii kwa kufanya hivyo, akisema tena..
Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”.
Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”.
Unafanya hivyo kwa kujitenga na mambo yote mabaya ya kidunia hii, kama vile ulevi, sigara,disko, anasa, matusi, miziki ya kidunia, rushwa, visasi, chuki, uasherati, utoaji mimba, vimini, mahereni, mawigi, suruali, lipsticks, wanja, n.k. unajitwika msalaba wako na kumfuata Yesu.
Na ukishafanya hivyo kwa kutii maagizo yote aliyokupa sasa hapo ndipo kuna amani Fulani inayotoka kwake na kuingia ndani yako, na hiyo ndiyo inajenga uhakika huo na kukushuhudia kuwa wewe ni mwana wa Mungu. Na hata ikitokea umekufa kwa ghafla haijalishi ni katika hali gani, huna wasiwasi kwasababu mbinguni utakwenda, kwasababu unashuhudiwa moyoni.
Lakini tukisema sisi tunaishi katika Maisha ya toba huwa tunatubu kila siku, na kila dakika na huku nyuma bado Yesu hajaleta badiliko lolote ndani yetu, hapo bado
tunajidanganya..Na mbinguni hatutakwenda. Hatubaatishi kwenda mbinguni, kwamba tunaotea saa atakayokuja atukute tumetubu.. Hivyo kumwamini Yesu na kuwa na uhakika wa uzima wa milele ni Zaidi ya kuongozwa sala ya toba, au kutubu mara kwa mara.. ni pamoja na kuyatii na kuyaishi yale yote anayokuagiza tangu siku ile uliposema nimeamua kumfuata Yesu.
Yohana 5:24 ‘Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani’.
Natumai kuanzia leo wewe uliyeokoka ambaye umekuwa huna uhakika kuwa utakwenda mbinguni au la, naamini utaanza kuchukua uamuzi huo mpya wa kumfuata Yesu kwa moyo wako wote na kuyatii yote anayokuambia.., ili na wewe akupe uhakika huo wa kwenda mbinguni, lakini ukibakia katika hali hiyo hiyo ni uthibitisho kuwa huwezi kwenda mbinguni,..
Na kama Bado utakuwa bado hujamwamini Bwana Yesu na wewe unataka leo hii kuokoka, Yesu aanze kuyatengeneza Maisha yako upya, Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGU. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE. ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE. AMEN.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGU. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithibitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Fanya hivyo na Bwana atakusaidia
Kwa mawasiliano/mafundisho zaidi kwa njia ya whatsapp, tutumie ujumbe kwenye namba hizi: +255789001312/ +255693036618
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Ubarikiwe sana.
Tafadhali share ujumbe huu na kwa wengine. Vilevile ikiwa utapenda tuwe tunakutumia masomo haya katika inbox yako ya facebook au whatsapp utatumia ujumbe,
Mada Nyinginezo:
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
TUMAINI NI NINI?
Waoga ambao hawataurithi uzima wa milele ni watu wa namna gani?(Ufunuo 21:8).
NIFANYE NINI ILI MUNGU AYAJIBU MAOMBI YANGU?
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
Biblia inasema tusiwe kwazo kwa yeyote, je! inawezekanikaje kwa dunia hii ya sasa?(2Wakorintho 6:3).
Zeri ya Gileadi ni nini?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Amen ubarikiwe sana mtumishi
Hasante sana kwa mafunzo yenu yanazidi kunijenga katika Imani. Barikiwa
Amen. nawe pia uzidi kubarikiwa..
Amen twashukuru kwa baraka hizo.
NAHUKURU SANA KWA MAFUNDISHO MEMA MUNGU ALIYOTUPATIA KUPITIA MTUMISHI WKE WEWE NINA IMANI NI MSAADA KWANGU NA VIZAZI VYETU VYOTE KWANI YATAVIONGOZA KATIKA NJIA IMPENDEZAYO YEYE NAAM NAOMBA MUNGU AZIDI KUKUBARIKI