SWALI: Naomba kufahamu maana ya unabii unaozungumzia taifa la Tiro (Isaya 23). Kwamba litafanya ukahaba na falme zote ulimwenguni kisha utajiri wake utakuwa wakfu kwa Bwana. Tafsiri yake ni nini?
Isaya 23:17-18 inasema..
[17]Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia. 18 Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.
[17]Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia.
18 Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.
JIBU: Ukianza kusoma toka mstari wa kwanza wa hiyo sura ya ishirini na tatu (23), utaona Mungu anazungumzia adhabu, aliyoitoa kwa hilo taifa la Tiro lililokuwa na utajiri na mali nyingi kutokana na biashara zake lilizofanya na dunia nzima. Hata kuyakosesha na mataifa mengine, kwa bidhaa zake. Na jambo hilo Mungu akalihesabu kama ni ukahaba, hivyo akalipiga na kuliangusha kabisa likawa si kitu tena kwa muda wa miaka sabini(70).
Ni mfano tu, mataifa yanayokosesha ulimwengu sasa, kwa kuuza bidhaa ambazo ni machukizo kwa Mungu, utakuta taifa linazalisha nguo za mitindo ya nusu uchi, na kuyauzia mataifa mengine, au linatengeneza sinema zenye maudhui za kizinzi na kuyasambazia mataifa mengine yaliyokuwa na maadili.. Huo ndio mfano wa ukahaba ambao taifa la Tiro lilikuwa linafanya.
Isaya 23:15
[15]Basi, itakuwa katika siku ile, Tiro utasahauliwa miaka sabini, kadiri ya siku za mfalme mmoja; hata mwisho wa miaka sabini, Tiro utakuwa kama vile ulivyo wimbo wa kahaba.
Lakini baadaye Mungu alilirudia tena, na kuruhusu lifanikiwe, kama pale mwanzo. Likajikusanyia tena utajiri mwingi sana kwa biashara zake.. Lakini Kwasababu halikutubu, kitabia Mungu akalipiga kwa namna nyingine kwa kuzuia utajiri wao wasiule au kwa lugha nyingine hazina zao zisitunzwe kwa maendeleo yao, Bali Bwana atazizuia zije kutumika kwa kazi yake yeye mwenyewe na watu wake.
Na unabii huo ulikuja kutimia..
ndio maana ya huo mstari wa 18, unaosema..
[18]Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.
Hii ni kufunua nini?
Kufanikiwa kwake mwovu, kunatimiza makusudi mawili la kwanza ni aidha kwenda kujiangamiza mwenyewe (Mithali 1:32, Zab 92:7), au kumkusanyia mtu mwingine mwenye haki.
biblia inasema..
Mithali 28:8
[8]Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.
Watu wengi wanaofanikiwa isivyo halali,mara nyingi mali zao, hula wengine..Ndicho alichokifanya Mungu kwa taifa la Tiro.
Ni kutufundisha pia fedha na dhahabu ni mali ya Bwana. Yeye ana uwezo wa kuzuia na kuachilia, anauwezo wa kuwapa watu wake hazina za gizani ambazo hawajazisumbukia, kwa ajili ya kazi yake.
Hivyo kumbuka Bwana akufanikishapo, tembea na Kristo, kinyume na hapo, mambo hayo mawili yanaweza kukukuta, aidha mafanikio hayo yazidi kukuangamiza ufe uende kuzimu, au yaliwe na watu wengine kabisa wema usiowajua na kazi yako ikawa bure.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Masomo mengine:
Miji ya Tiro na Sidoni ni miji gani kwasasa?
Kwanini Herode aliwakasirikia watu wa Tiro na Sidoni? (Matendo 12:20)
Je ni halali kwa mkristo kufanya biashara ya Forex?
Print this post