UMEUFIKILIA MLIMA SAYUNI?.

UMEUFIKILIA MLIMA SAYUNI?.

Waebrania 12:22 “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi”

Nyakati za Nabii Musa,Ulikuwepo mlima uliojulikana kama mlima wa Mungu, au Sinai, au mlima Horebu.

Katika mlima huo, Mungu aliposhuka hakuruhusiwa mtu mwingine kuusogelea isipokuwa Musa tu peke yake, hata mnyama aliyekaribia alikufa.

Kwani ulikuwa umejaa utukufu wa MUNGU, ulioambatana na radi na umeme na ngurumo zinazotisha.

Na kutokana na hali hiyo, ni Musa tu peke yake ndiye aliyepata kibali cha kuusogelea mlima huo na kusikia sauti ya MUNGU, wengine wote walibaki chini, kusubiria kusikia kile Musa alichoambiwa na MUNGU.

Lakini katika agano jipya, tunasoma kwamba upo mlima mfano wa huo, lakini si katika mwili bali katika roho, na mlima huo una utukufu mkubwa kuliko ule wa Sinai, Musa alioupanda.

Mlima huu wa rohoni, nao pia unaitwa Sinai, ambao umejaa malaika wa Mungu, na wenye utukufu mwingi.

Tofauti na mlima ule wa kwanza wa mwilini ambao ni Musa tu ndiye aliyeruhusiwa kuupanda, mlima huu wa rohoni unapandwa na mtu yeyote aliye ndani ya imani kamili ya YESU KRISTO.

Waebrania 12:21 “Na hayo yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka.

Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi”,

Na faida za kuupanda mlima huu (Sinai ya rohoni) ni kwamba mtu atapata nafasi ya kumkaribia MUNGU zaidi na kumsikia MUNGU zaidi kuliko Musa alivyomsikia kule Sinai,

Pia atashuka na utukufu mkuu zaidi ya ule Musa aliokuwa nao aliposhuka hata uso wake ukang’aa.

Swali linarudi je wewe ni miongoni mwa watu walioufikia huo mlima wa MUNGU?.

Lakini labda utajiuliza pia mtu ataufikiaje huo mlima?..

Biblia imetupa majibu..

Zaburi 24:3 “Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?

4 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.

5 Atapokea baraka kwa BWANA, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake”.

Sasa tunapataje mikono safi na mioyo myeupe, itakayotufanya tustahili kufika katika mlima huo mtakatifu?.

Njia ni moja tu, kumwamini Bwana YESU, Kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha na kupokea Roho Mtakatifu, na kila siku kuishi maisha  ya utakatifu.

Kwa njia hiyo basi tutaweza kufikia kilele cha baraka, kwani ni Neema kuu tulipewa ya sisi kuufikia mlima wenye utukufu zaidi ya ule Musa aliopanda.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply