Kama wewe ni msafiri utakuwa umegundua kuwa nyasi zilizopo katikati ya barabara zenye vumbi huwa haziathiriwi na tairi za gari.
Utakuta barabara inapitiwa kila siku na magari yenye tairi zenye nguvu na nzito lakini katikati ya barabara utaona mstari wa nyasi, zilizo salama kabisa.
Ikifunua kuwa si kila kilichopo katikati ya hatari kipo hatarini, kuna watu wanaonekana kama wapo katikati ya changamoto na hatari nyingi lakini wapo salama, na kuna wengine wanaonekana kama wapo pembezoni (mahali salama) lakini ndio wapo hatarini.
Watu waliosimama kweli na YESU, wanaonekana ambao hawasogezi mguu wao kulia wala kushoto, ni watu wanaoonekana wamwisho kabisa duniani, na wenye wanaopotea, watu waliojikana nafsi kwaajili ya YESU ni watu wanaonekana wamepotea,
Watu wanaotukanwa, na kudhalilika kwaajili ya misimamo yao ya kiimani wanaonekana kama wamepotea lakini ukweli ni kwamba wao ni mfano wa nyasi zilizopo katikati ya barabara, hazikanyagwi wala kuathiriwa na tairi za magari.
Siku zote wanasimama na Zaburi 23..
Zaburi 23:1 “BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji”
Kama ulikuwa unasuasua katika Imani na Wokovu, huu ni wakati wako wa kusimama katika njia kuu.
Simama kwa imani na tembea kwa ujasiri katikati ya njia yako ya wokovu, usisogeze mguu wako kushoto wala kulia nawe utakuwa salama, na utaona wema wa MUNGU.
Mithali 4:25-27 “Macho yako yatazame mbele.
26 Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike;
27 Usigeuke kwa kuume wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni”.
Vile vile kama bado haujaokoka, fahamu ya kuwa hizi ni siku za mwisho, na Bwana amekaribia sana kurudi. Na upendo wake kwako ni ule ule usio na mwisho,
YESU anawapenda watu wote wa kike na kiume, wakubwa kwa wadogo, walio na maradhi na wenye afya, wenye uwezo na wasio na uwezo,
Maandiko yanasema kwa moyo mtu huamini hata kupata Haki na kwa kinywa hata kupata wokovu.(Warumi 8:9-10).
Leo hii mwamini moyoni na mkiri kinywani ubadilike na kuwa mwana wa MUNGU, Mzao wa mbinguni.(1Peteo 2:9).
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ