SWALI: Naomba nieleweshwe maana ya huu mstari
Mithali 24:27
[27]Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako.
JIBU: Zamani enzi za biblia, kilimo kilikuwa ni uti wa mgongo wa uchumi wa watu wengi kama ilivyo sasa katika baadhi ya jamii.
Hivyo ilikuwa ni ajabu mtu kutumia rasilimali zake katika kununua au kujenga vitu visivyo na umuhimu sana, kama vile nyumba, nguo za kifahari, magari ya farasi n.k.angali shambani kwake hajajiwekeza vya kutosha.
Watu walikuwa wanakusanya kwanza chakula cha kutosha kujihakikishia shibe kwa miezi au miaka kadhaa, ndipo baada ya hapo hufikiria kutumia hazina zao katika kujenga, au kujiendeleza..lakini hawakujiendeleza kabla ya kuhakikisha mashamba yao yamewanufaisha..
Na ndio hapo Sulemani utaona anatoa ushauri ule ule..
Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba tengeneza kwanza mambo yako uwe imara ndipo yale mengine ya ziada yafuate baadaye.
Ni kawaida ya mwanadamu kupenda, vitu vizuri kwanza kabla hajavitaabikia..
Alikuwepo Gehazi, mtumwa wa Elisha, yeye aliona kusubiri wakati wa Mungu ni kujichelewesha, kutumika kama mtumwa asiye na faida ni kupoteza muda, hivyo, zile zawadi zenye thamani nyingi zilizoletwa na Naamani, na Elisha kuzikataa, yeye akamwona kama alikuwa hapendi mema..lakini Elisha alimwambia maneno haya..
2 Wafalme 5:26
[26]Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng’ombe, na watumwa, na wajakazi?
Alimuuliza Je huu ndio wakati? ..kumbe kulikuwa na wakati lakini haukuwa ule..
Watu wanataka kula vitu vya Bwana lakini hawataki kutengeneza kwanza kazi zao huko mashambani, hawana muda wa kuifikiria kazi ya Mungu, hawana muda na kuhubiri injili ya kweli,wanachokifiria ni matumbo, na kwamba watapata faida gani..
1 Timotheo 6:5-6
[5]… huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida. [6]Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.
[5]… huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.
[6]Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.
.Vilevile hata katika maisha ya kawaida, hekima hizi zinamafunzo, mtu atataka anunue simu ya milioni 2, lakini hana shughuli yoyote ya kumwingizia kipato, badala aitumie kama mtaji, kisha kile akipatacho kama faida ndio atumie kununua hayo mengine..
Bwana atusaidie, katika kuyapangalia maisha yetu ya rohoni na mwilini
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
TENGENEZA NYAVU ZAKO, OSHA NYAVU ZAKO.
Nini maana ya vifungeni viuno vya Nia zenu? (1Petro 1:13).
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
USIWE ADUI WA BWANA
Nini maana ya Ukuta uliopakwa chokaa (Matendo23:3)?
Uchaga ni nini? (Luka 12:24)
NAAM, HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA.
Rudi nyumbani
Print this post