TENGENEZA  NYAVU ZAKO, OSHA NYAVU ZAKO.

TENGENEZA  NYAVU ZAKO, OSHA NYAVU ZAKO.

Shalom, Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno ya Bwana wetu.

Katika mambo ya uvuvi, zipo kanuni za uvuvi za kufuatwa, wengi wetu tunadhani, kazi ya mvuvi ni ya kwenda tu kutupa nyavu baharini, kukusanya samaki, kisha kuwatoa nje, halafu basi analala, anaamka tena kesho na nyavu yake hiyo hiyo, anakwenda kuitupa habarini na kuvua samaki wengine tena.. Ndugu Kama umekuwa ukifikiria hivyo basi umekosea.. Vinginevyo kazi ya uvuvi  ingekuwa ni rahisi sana.

Kwa kawaida, wavuvi ni sharti, kila wamalizapo uvuvi mmoja, wazioshe nyavu zao kama sio kuzitengeneza, Kwasababu wanapokwenda kuvua sio tu samaki peke yake wanajinasa kwenye nyavu, bali pia kunakuwa na takataka nyingine nyingi  zinakwama kwenye neti, sana sana magugu ya baharini, masalia ya magamba ya viumbe , na matope, kiasi kwamba nyavu zile zikiachwa, siku kadhaa bila kuoshwa, vinavundisha nyavu.

Na si hilo tu, kunakuwa na samaki waliokufa, katikati ya neti, nao pia wakaachwa kipindi kifupi sana wanaozesha , na hiyo inapelekea kukaribisha panya kula neti, na kuifanya iwe dhaifu sana, hususani kwenye kamba zake,

Na bado wanasema, ili samaki wawezi kukamatwa kiwepesi, ni sharti ni yenyewe iwe kama vile haionekani itupwapo habarini ,lakini kama inauchafu mwingi, wanasema samaki wakiona, wanaogopa na kukimbia.

Pia nyavu hiyo hiyo inapaswa itengenezwe/au ifanyiwe ukarabati, kwasababu wakati mwingine, kunakuwa ni miamba yenye ncha kali chini inayochana nyavu, au samaki wenye miiba mikali ambao wakipita mara moja tu katikati wanachana nyavu. Hivyo kama mvuvi kila unapoliza kuvua ni sharti ukague neti yako kama inamatundu uizibe.

Hivyo suala la kusafisha na kukarabiti neti ni lazima kwa mvuvi yeyote kila anapomaliza kuvua, haijalishi siku hiyo amepata samaki au hajapata. Haijalishi atakuwa amechoka au hajachoka, Ni lazima aisafishe, kwasababu ni lazima tu itakuwa na uchafu.

Na ndio maana wakati ule Bwana Yesu alipokuwa anapita pwani aliwaona akina Petro, wametoka kuvua samaki, na hawajapata chochote usiku kucha, lakini kanuni ilikuwa ni lazima wazioshe nyavu zao, haijalishi walipata au hawakupata.

Luka 5:1 “Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,

2 akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa, LAKINI WAVUVI WAMETOKA, WANAOSHA NYAVU zao.

3 Akaingia katika chombo kimoja, ndicho chake Simoni, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni.

4 Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.

5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu”.

Umeona, sasa soma tena vifungu hivi, uone kuna wakati pia walizitengeneza nyavu zao, na sio kuosha tu peke yake.

Marko 1:19 “Akaendelea mbele kidogo, akamwona Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, nao pia walikuwa chomboni, WAKIZITENGENEZA NYAVU ZAO.

20 Mara akawaita, wakamwacha baba yao Zebedayo ndani ya chombo pamoja na watu wa mshahara, wakaenda, wakamfuata.

SASA MAMBO HAYO KATIKA ROHO YANAFUNUA NINI?

Sisi kama wahubiri, sisi kama watumishi wa Mungu tunaofanya kazi ya kuwavua watu kwa Kristo, huwa tunajisahau sana na kudhani kuwa kuhubiri tu kunatosha, Au kufundisha tu, au kushuhudia tu. Hatujui kuwa tunapaswa kila siku TUSAFISHE na kutengeneza NYAVU zetu, tunazozitumia kuvulia.

TUNATENGENEZAJE NYAVU ZETU?

Na tunazitengeneza kwa NENO LA MUNGU. Ikiwa na maana tunapaswa Neno la Mungu likae kwa wingi ndani yetu, tusome Neno, tujue misingi na kanuni za uvuvi Kristo anazozitaka, tujue ni nini tunapaswa tufundishe, na nini tusifundishe kwa wakati husika, ujumbe upi tutoe, na upi tusitoe kwa watu fulani. Vinginevyo tukipuuzia, tutajikuta samaki watapenya kwenye nyavu zetu, tukawakosa, kwasababu zina matundu matundu.

TUNAOSHAJE NYAVU ZETU?

Vile vile, Kuosha nyavu zetu. Ni kwa kujitakasa maisha yetu. Maana yake kuishi maisha yanayompendeza Mungu, maisha ya ushuhuda, maisha matakatifu. Ikiwa tuna ushuhuda mbaya katika mazingira yanayotuzunguka, na huku bado tunahubiri injili ni kuonyesha kuwa NYAVU zetu ni chafu. Hivyo Samaki watatukimbia wanapoona uchafu huo kwetu. Na ndio maana pale tunapovua hatuona matunda yoyote, kumbe ushuhuda wetu ndio unaowakimbiza mbali na sisi.

Hivyo ni wajibu wetu, sisi kama wahubiri kuzingatia hayo mambo mawili kila siku. Kwasababu wavuvi nao wanafanya hivyo kila siku. Nasi tuifuate kanuni hiyo rohoni. Na hakika tutamletea Kristo matunda mengi.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

MIUJIZA YA KRISTO, HAITEGEMEI KANUNI ZA KIBINADAMU.

Je ni sahihi kuweka walinzi kulinda mali zetu?

Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko siku elfu”?

MATARAJIO YA KILA MWANADAMU DUNIANI NI YAPI?

APENDAYE FEDHA HASHIBI FEDHA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments