SWALI: Naomba kufahamu maana ya Neno hili, maana huwa nalisoma silielewi.. (Zaburi 84:10 “Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu”) .
JIBU: Maana yake ni kuwa ukitumia siku yako moja kikamilifu kudumu uweponi mwa Bwana, tangu jua linapochomoza mpaka pale linapozama, hujatoka katika uwepo wa Bwana, aidha upo ibadani, au kwenye maombi, au katika kuifanya kazi yake..Basi ujue mbinguni siku yako hiyo inahesabika kuwa ni bora Zaidi ya siku elfu moja kama ungekuwa penginepo..
Jaribu kufikiria siku elfu moja ni sawa na miaka karibia miwili na robo tatu…Hivyo kama ukitumia siku 7 kikamilifu uwepo mwa Bwana, basi ujue inathamani zaidi ya mtu anayehangaika huku na huko kwa miaka 19 kutafuta kitu Fulani..
Na ndio maana Daudi anamalizia kusema.. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu..Bawabu ni mfunga na mfungua milango kwenye majumba makubwa ,ni kama mlinzi wa mlangoni..zamani kazi za mabawabu ni kazi ambazo hazikuheshimika, hata sasa ni vivyo hivyo…Kwahiyo Daudi hapo anamaanisha kuwa akipata ka nafasi kidogo tu kama kale cha bawabu katika kumtumikia Mungu..basi ataifurahia na kuishangalia kuliko angepata kazi ya maofisi ya mashirika makubwa makubwa n.k ya watu waovu…kwasababu anajua akiitumia vizuri siku yake moja hapo, inamletea faida mara elfu katika ufalme wa mbinguni kuliko kule kwengine.
Vivyo hivyo na sisi wakristo, tukiupata ufunuo huo, hatutaona shida kudumu katika mikusanyiko yenye ibada ndefu, hatutaona shida kumtumikia Mungu kikamilifu hata kama kazi yake itatugharimu kuchomoza kwa jua hadi kuzama kwake, hata kama itaonekana ni ya kudharaulika, hatutaona uvivu kusoma mahubiri marefu kwasababu tunajua ni kwa faida yetu wenyewe ..hatutajali ni masaa mangapi yamekwenda katika kuomba..Kwasababu tunajua mwisho wake utakuwa ni wenye thamani nyingi Zaidi ya siku 1000.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
Nini tofauti kati ya Amri, sheria na Hukumu?
JE VIBWENGO NI KWELI VIPO?
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
HAKIKISHA UNALIELEWA NENO.
JE UNATAMANI KUMJUA MUNGU, NA HUJUI PA KUANZIA?
KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.
JE ADAMU ALIKUWA NA KITOVU?
Rudi Nyumbani:
Print this post