Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa kuna roho za malaika na roho za mashetani…Malaika walioasi ndio wanaojulikana kama mashetani leo…Na malaika hawa wanafanya kazi katika mamlaka ya giza…Yaani kazi yao ni kwenda kinyume na kila kazi ya Mungu…
Kadhalika malaika hao walioasi (yaani mashetani au kwa jina lingine Mapepo)..wapo wa aina nyingi na wenye tabia tofauti tofauti…Kama vile malaika walivyo wengi na wenye tabia tofauti tofauti…kadhalika na mapepo nao ni hivyo hivyo…Katika biblia tunasoma kuna malaika wa maji..(Ufu.16:5)..kadhalika kuna malaika wanaohusika na nchi, bahari, pia wapo malaika wa kuleta habari kama Gabrieli, ..wapo malaika wa sifa kama maserafi na makerubi, wapo wa vita kama Mikaeli na wengine wengi.
Na katika upande wa pili wa malaika walioasi ni hivyo hivyo wana vipawa tofauti tofauti..yapo mapepo yanayohusika tu na maji, mengine moto, mengine yanahusika kusababisha majanga kama ajali,.. mengine kuleta magonjwa, mengine kuharibu nchi n.k..Lakini yote lengo lao kuu ni kupambana dhidi ya ufalme wa Nuru..
Sasa Vibwengo ni aina ya mashetani/mapepo yanayoangukia katika moja wapo ya hilo kundi…Vibwengo vina kazi ya kuwasumbua wale watu ambao hawajaokoka au hawajasimama vizuri kiimani..Na kwasababu ni roho za mapepo zile zile ambazo zinatenda kazi katika ufalme wa giza..hivyo lengo lao ni kuleta mauti ndani ya Mtu.
Na mtu anaweza kuishi na jamii hiyo ya mapepo aidha kwa kujua au kwa kutokujua…wakati mwingine mapepo hayo (vibwengo) vinaweza kujidhihirisha dhahiri kwa mtu..na mtu kuvishuhudia kabisa kwa macho…
Mara nyingi vinajidhihirisha kwa umbo la mtu mfupi sana aliyejaa..au aina fulani ya wanyama ambao wanaonekana kama watu..mfano wa maumbo yanayoonekana mara nyingi na vibwengo ni maumbo ya mfano wa nyani..Anaonekana mtu kama nyani lakini si nyani n.k…Na mapepo hayo yasipopatiwa ufumbuzi mapema yanaweza kusababisha hata kifo cha kiroho na cha kimwili kwa mtu..au yanaweza kusababisha tatizo fulani lenye madhara makubwa…Hivyo si busara kuzipuuzia roho hizo chafu.
Jambo la kwanza ni dhambi ndani ya maisha ya mtu..Mtu yeyote ambaye anaishi katika maisha ya dhambi anafungua mlango mpana sana wa kusumbuliwa au kuingiliwa na roho zozote za mapepo..Mtu anayetenda dhambi ni kama mtu aliyewasha WIFI data kwenye simu yake ya mkononi.. kiasi kwamba simu yoyote iliyokaribu na yake inaweza kukamata mawimbi yatokayo katika hiyo simu yake…Kadhalika mapepo ni hivyo hivyo, mtu anayefanya dhambi ni kama amewasha WIFI katika ulimwengu wa roho,..kwamba hata mapepo yaliyokuwa yanatembea tembea huko na huko ni rahisi kupata habari za huyo mtu.. na kumwingia au kumletea madhara fulani.
Dhambi zifuatazo ndizo zinazoongoza kukaribisha uwepo wa vibwengo kwa mtu..na si tu vibwengo bali hata jamii nyingine zote za mapepo.
1) IBADA ZA SANAMU : Hii inahusisha aina zote za aubuduji sanamu, aidha za watu au za wanyama…unapoisujudia sanamu ya aina yoyote ile ni mlango mpana sana wa kuingiliwa na mapepo..au kuishi na vibwengo pamoja nawe…
2) UASHERATI : Dhambi hii inashika nafasi ya pili katika kukaribisha uwepo wa mapepo ndani ya mtu na hata kuvutia uwepo wa vibwengo..Asilimia kubwa ya watu wanaoona roho hizo za vibwengo lazima kwa namna moja au nyingine ni waasherati. wa kimwili.
3) USHIRIKINA/UCHAWI : Ushirikina ni hali ya kujihusisha husisha na masuala ya nguvu za giza,… kama kwenda kwa waganga au kwa watabiri wa nyota, au utambuzi…Mtu anayehudhuria kwa waganga huyo ni mshirikina hata kama sio mchawi kabisa…lakini kitendo tu cha kwenda kwa waganga kutafuta suluhisho fulani..huo tayari ni ushirikina..na ni mlango mpana sana unaoshika namba tatu kukusogeza karibu na uwepo wa roho za mapepo hususani vibwengo.
Ikiwemo uvaaji wa wigi, kujitoboa mwilini na kujiweka vito kama hereni, mabangili, mikufu…pia upakaji wa wanja, upuliziaji wa marashi makali yasiyojulikana hata yametengenezewa wapi,..uchoraji wa hina na uchoraji tattoo..Mambo hayo yanahusika sana katika kuvuta uwepo wa roho za vibwengo na jamii nyingine za mapepo…Ndio maana hata vibwengo vyenyewe vinakuwa kama vimepaka chokaa usoni, au vinatoa harufu ya marashi fulani yasiyojulikana..hiyo yote ni kuonesha vimekutana na mahali ambapo panastahili wao kuwepo..
5) UVAAJI MBAYA:
Mavazi yote yasiyopasa…kama suruali kwa wanawake, magauni kwa wanaume, mavazi ya nusu uchi kama vimini, vitop, nguo za kubana n.k…ni WIFI kwa mapepo….Hata roho hizo za vibwengo viwatokeapo watu zinakuwa kama zimevaa mavazi yasiyoeleweka, kiasi kwamba huwezi kukitambua kama ni jinsia ya kiume au ya kike…Sasa vinakuwa vinatafuta mahali panapowastahili…kwa watu wa jamii zao.
6) ULEVI, UVUTAJI SIGARA na ANASA: Disko ni makao ya mapepo, mtu anayeingia disko tayari anatoka na pepo pasipo hata yeye kujijua…Mapepo ndio makao yao huko, sehemu ambazo watu wapo akili nusu kutokana na ulevi…sehemu ambazo watu wanacheza cheza madansi na kucheka cheka na kuwa na mizaha…Ndio maana hata vibwengo vyenyewe viwatokeapo watu ni lazima viwe nusu-nusu kama vimelewa hivi…vinakuwa nusu vinaakili timamu nusu vitahira…vinachekacheka, mara vinacheza cheza, vinakuwa na mizaha mizaha…yote hiyo ni kwasababu ndiyo asili yao..Hivyo vinatafuta watu wenye asili kama yakwao vikae nao..na hao wapo bar, disko au kwenye vikundi vya kamari.
7) UTAZAMAJI WA PORNOGRAPHY: Pornograph ni picha za ngono..ambazo siku hizi zinatazamwa hata kupitia simu za mkononi…Ufahamu uliojaa zinaa ni lango kubwa la roho hizo…
Suluhisho pekee la kuepukana na roho hizo za vibwengo ni kuokoka!…Kuokoka maana yake ni kutubu kwa kudhamiria na kumaanisha kabisa kuacha dhambi…unaacha dhambi zote ulizokuwa unazifanya hizo zilizoorodheshwa hapo juu na nyingine zote ambazo hazijaorodheshwa…Unatubu na kumwambia Bwana Yesu unahitaji wokovu na unamuhitaji yeye..si tu kwaajili ya kuepukana na vibwengo, bali kwasababu unahitaji kufanyika kuwa kiumbe kipya na kuwa mkamilifu kama Mungu alivyo.
Ukisha tubu hatua inayofuata ni kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kama ulikuwa hujabatizwa,.. na baada ya hapo Roho Mtakatifu aliyeingia ndani yako atafanya mengine yote yaliyosalia.
Ukishaokoka namna hiyo! na kudhamiria kuacha dhambi…basi wewe mlango wa mapepo hautakuwepo ndani yako…Haiwezekani funza kuwepo ndani yako au kwenye mazingira yanayokuzunguka kama umefanya usafi kweli kweli…Dawa ya kuondoa funza ndani kwako ni kuwa msafi sio kuwaambia funza ondokeni kwangu…kadhalika dawa ya kuondoa mapepo na vibwengo karibu na wewe ni kuwa msafi.. (yaani kujiweka katika hali ya utakatifu), ambayo hiyo inakuja kwa kutubu dhambi na kuziacha..(yaani kuokoka) na sio kwenda kutafuta maombezi huku na huko…
Ikiwa umeshawahi kusumbuliwa na roho hizo za vibwengo..basi hiyo ndio dawa pekee tuliyopewa katika biblia takatifu.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789 001 312 jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Wakatoliki wanaabudu sanamu?
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?
PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.
Rudi Nyumbani:
Print this post