KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

Kifo cha Reinhard Bonkey kinaacha ujumbe gani kwetu?


Mwinjilisti wa kimataifa Reinhard Bonkey, raia wa Ujerumani, aliyezaliwa tarehe 19 Aprili 1940.. Anaeleza jinsi alivyompa Kristo Maisha yake akiwa bado kijana mdogo mwenye umri wa miaka 9, baada ya kuhubiriwa na mama yake kuhusu habari za Yesu na dhambi zake.

Alidumu katika Imani mpaka kufika kwenda chuo cha biblia na Mara baada ya kumaliza chuo cha mafunzo ya biblia huko Wales na kusimikwa utumishi wa Uchungaji nchini kwake Ujerumani, ndipo alipoanza kuja Afrika, kwa ziara zake za umishionari na kuweka maskani yake rasmi  katika nchi ndogo ya Lesotho.

Ono la kumtumikia Mungu Afrika.

Akiwa huko Lesotho Reinhard Bonkey anasema kabla hajaanza kazi ya Uinjilisti katika bara la Afrika akiwa na mke wake, usiku mmoja aliota ndoto ambapo aliona bara la Afrika likioshwa kwa damu ya Yesu kuanzia kusini kwenda kaskazini, na kutoka magharibi kwenda mashariki. kwa siku ya kwanza anasema aliipuuzia ndoto hiyo akidhani kuwa labda usiku uliopitia alikula ndizi, lakini ndoto hiyo ikajirudia kwa siku nne mfululizo ndipo alipotambua kuwa ni Mungu ndiye alikuwa anasema naye.

Akaenda kuwaeleza viongozi wake juu ya jambo hilo na nia yake lakini walimkataza na kumwambia afanye kazi kama za wamishionari wengine, lakini sio hiyo ya kuzunguka kuhubiri injili..Lakini Bonkey aliondoka na kwenda kukaa hotelini kwa kipindi kumwomba Mungu ampe ruhusu ya kupata kibali kwa viongozi wake, kama ikiwa ni yeye kweli aliyemuita lakini wakati akiwa anaomba alisikia sauti ya Mungu ikimwambia..“USIPOIFANYA HII KAZI, NITACHAGUA MTU MWINGINE WA KUIFANYA”

Mwanzo ya uinjilisti:

Aliposikia hivyo alishituka kwa hofu, ndipo akamfuata mke wake, na kumweleza kuwa siku hiyo hiyo ataandika barua ya kuacha, kazi yake ya utumishi aliyowekwa na viongozi wake..Na ndipo akaanza safari ya kuhubiri injili katika miji mbalimbali bila kugeuka nyuma.

Kwa kuwa hakuwa na mtu wa kumuuliza jinsi kuandaa mikutano na jinsi ya kufundisha kwenye mikutano ya hadhara, alitumia uzoefu wake ule ule akijua kuwa Roho Mtakatifu atakuwa naye katika kila hatua, japo alipotoka hakufundishwa juu udhihirisho wa nguvu za Mungu, hivyo kila mahali alipokuwa akiandaa mikutano watu walikuwa wakimtazama tu,

Anasema siku moja nguvu za Mungu zilishuka katika mkutanao ule, na yule mtafsiri wake alidondoka chini kwa kuzidiwa na nguvu hizo, na huku akiwa analia alisikia sauti ikimwambia “NENO LANGU LITOKALO KINYWANI MWAKO, LINA NGUVU ILE ILE SAWA NA LINAVYOTOKA KATIKA KINYWA CHANGU”..

Imani ilivyoanza kutenda kazi:

Alivyosikia vile alishangaa, akapata msukumo mkubwa sana ndani yake, ndipo kwa ujasiri akasema “Vipofu wote walio katika huu mkutano wasimame, na leo hii kwa mara ya kwanza watakwenda kuuona uso wa Bonkey”..Alivyosema vile, ndani ya moyo wake alisikia sauti nyingine ikimwambia..Na ikiwa hatawataona utafanyaje…Lakini yeye alisema Ninalisema Neno la Mungu..Na alipotamka tu “KWA JINA LA YESU, MACHO YENU YAFUMBUKE!!” ..Alichosikia tu ni kelele za watu wakisema ninaona…wakirukaruka, na mara mda huo huo alimwona mtoto mdogo aliyekuwa amebebwa na mama yake, akipitishwa juu ya vichwa vya watu, na kurushwa mbele mpaka pale alipo na kujikuta mtoto yule yupo mikononi mwake..

Anasema mtoto huyo alikuwa na viungo vilivyokunjana mfano wa tambi…Lakini saa ile ile alipofika mikononi mwake, nguvu za Mungu zikaanza kumtetemesha mtoto yule, akamwachia akadondoka lakini hakutua vibaya bali alitua kwa miguu yake na kuanza kukimbia na kurukaruka. Na huo ndio ulikuwa mwanzo wa huduma yake iliyoambata na nguvu za Roho Mtakatifu.

Jinsi huduma ilivyokuwa:

Mwanzoni kabisa mwa huduma yake Alianza kwa kuitisha mikutano midogo midogo, japo anasema haikuwa na mwitikio mkubwa kwa siku za mwanzo, kwani mkutano ulio mkubwa sana uliweza kuhudhuriwa na watu mia nane tu (800). Lakini, baadaye alivyozidi kuhubiri idadi ya watu ilizidi kuongezeka kwa kasi, mpaka kufikia hatua kila mkutano anaouitisha haupungui watu laki moja na nusu (150,000). Na kwa jinsi ilivyozidi kuendelea alipoitisha tu mkutano mmoja katika mji mmoja, kuliweza kukusanyika watu Zaidi ya milioni moja na laki sita (1,600,000).

Zaidi ya watu milioni moja kwa siku walikuwa wanarekodiwa kumpa Kristo Maisha yao.

Na Tangu mwaka 1986, huduma ya Reinhard Bonkey inarekodi ya watu Zaidi ya milioni 77 waliokuja kwa Kristo. Hiyo ni Zaidi ya idadi ya watu waliopo katika la Tanzania.

Kifo cha Reinhard Bonkey:

Mnamo tarehe 7 Disemba 2019, safari ya mtumishi huyu mwaminifu wa Mungu ilifikia kikomo..Reinhard Bonkey, bila shaka watu kama hawa ndio wanaostahili waandikiwe kwenye makaburi yao maneno haya:

2Timotheo 4:7  “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda”;

NI FUNZO GANI AMETUACHIA KATIKA UTUMISHI WA MUNGU?

Ukweli ni kwamba Huduma ya mtumishi huyu ilifanikiwa kwa jambo moja linaloitwa utiifu. Alitii pale alipoitwa bila kujali mahali atakapokwenda, na kazi atakayoifanya.. Enzi hizo hakukuwa na miundo mbinu mizuri kama iliyopo sasa, lakini alijitoa kwa hali na mali kwa ajili ya injli ya Kristo..

Waebrania 12:1  Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

2  tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

Watu kama hawa, tutawezaje kwenda kupata thawabu moja na wao kama na sisi hatutapiga mbio kama za kwao?

Unasubiri nini usitubu dhambi zako?

Ikiwa bado upo nje ya Kristo, usisubiri kifo kikukute, tubu leo hii umpe Bwana Maisha yako, Akuokoe..Fanya hivyo kwa kumaanisha hapo ulipo kwa kupiga magoti na kumwambia Mungu, Nisamehe makosa yangu yote, na kuanzia leo ninakiri kukutumikia na kukufuata,. Nisafishe kwa damu ya mwanao mpendwa YESU KRISTO, nifanyike kuwa mwana wako kuanzia wakati huu.

Sasa ikiwa umefanya hivyo, kwa kumaanisha kutoka moyoni, unachopaswa kufanya ni kuithibitisha hiyo Imani yako kwa kuacha yale ambayo ulikuwa unayafanya nyuma, na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kimaandiko wa kuzamishwa katika maji mengi, na kwa jina la YESU KRISTO, sawasawa na Matendo 2:38 ili uukamilishe wokovu wako.

Na Kristo akishaona mwitikio wako atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu, bure, ambaye huo ndio muhuri wa wokovu wako, atakayekaa nawe mpaka mwisho wa safari yako hapa duniani,..ikiwa unyakuo utakuwa haujapita. Fanya hivyo na Bwana akubariki sana.

Maran Atha!

Mbali na histori na Kifo cha Reinhard Bonkey, ungependa kupata habari za mashujaa wengine wa Imani?. Mtazame William Branham chini utajifunza mengi pia.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

HISTORIA YA WILLIAM BRANHAM

USHUHUDA WA RICKY:

MTETEZI WAKO NI NANI?

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Barikiwa san

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Asante kwa fundisho la Neema ya Yesu

Morris sanyano
Morris sanyano
2 years ago

Group hii imekuwa ya baraka sana kwangu