MAMBO YA KWANZA YAMEKWISHA KUPITA!

MAMBO YA KWANZA YAMEKWISHA KUPITA!

Karibu tujifunze Biblia.

Hizi tabu tunazoziona na kuzipitia sasa upo wakati umewekwa zitakwisha…

Ufunuo 21:3 “Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

 4  Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

5  Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.

6  Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.

7  Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu”

Magonjwa ni mambo ya kwanza..Yatapita yote!…HIV haitakuwepo kule ng’ambo, Kansa haitakuwepo, upofu hautakuwepo, kutokusikia hakutakuwepo, ulemavu wa Ngozi, akili, wala viungo hautakuwepo, vita havitakuwepo, chuki wala kuchukiwa hakutakuwepo, maadui hawatakuwepo, visasi havitakuwepo, kuteswa hakutakuwepo, kupapambana kutafuta Maisha hakutakuwepo, vifungo havitakuwepo, magereza na mahabusu hayatakuwepo kule, maumivu, huzuni, unyonge na uchungu havitakuwepo, kupanda na mwingine kuharibu hakutakuwepo,…

Ni paradiso ya furaha isiyo ya kifani…Kule hakuna vidonda tena…wala kulia, wala kupokea taarifa mbaya za misiba…wala hofu haitakuwepo tena…wala mashindano wala mateso….Hayo ni mambo ya kwanza…Furaha tutakayoipata tutakapoingia huko itaimeza uchungu wote tuliokuwa tunaupitia duniani…

Hutakuwa na muda wa kukumbuka kwamba ulishawahi kupitia tabu…Utahisi uliumbiwa tu raha tangu zamani…Furaha utakayoipata huko hutakumbuka kwamba kuna siku ulishawahi kuteseka sana ukiwa duniani kiasi cha kufa…Hutakumbuka hata kidogo..utasahau kabisa!…Utajiri utakaoupata huko hutakumbuka kwamba ulishawahi kuwa maskini duniani…Utaona kama hukuwahi kuishigi sehemu nyingine Zaidi ya hiyo hapo kabla….Ni furaha isiyoelezeka…

Tujitahidi sana tufike huko kwasababu siku za kwenda huko zimekaribia sana kulinga na unabii wa kibiblia…Siku yoyote isiyotegemewa na wengi..parapanda italia, wafu watafufuliwa kwanza wale waliokufa katika Imani na utakatifu..na sisi tuliomwamini Yesu na kuishi Maisha ya usafi tutawaona na kwa pamoja wakitoka makaburini mwao, kisha tutaungana nao..na kufumba na kufumbua miili yetu itabadilishwa na kung’aa kama ya malaika wa mbinguni..na tutanyakuliwa juu mawinguni kukutana na Bwana wetu Kristo akitungoja mawinguni ili kutupelekwa mbali sana kule juu zaidi ya nyota zote na sayari zote kwenye Mbingu za Baba yetu Mungu mwenyezi..huko tutakwenda kula mema yote Mungu aliyotuandalia…

Ni mbali sana, juu sana, yaani “mbingu, na mbingu-za-mbingu-za-mbingu” Mungu aketipo kama biblia inavyomzungumzia katika 2Nyakati 6:18 .. Huko ndiko kutakuwa makao yako wewe ambaye leo hii umedhamiria kung’ang’ana na Yesu, uliyedhamiria kusema iwe isiwe siuachi wokovu..

Lakini tusipojiandaa leo, kinyume chake tukaendelea kudumu katika mambo ya dunia hii,..tukaendelea kudumu katika uasherati, wizi, ulevi, utukanaji, ibada za sanamu, tukaendelea kuidharau Injili ya msalaba wa Yesu, halafu Unyakuo ukipita leo hatutakwenda popote na hata tukifa kabla ya unyakuo kutokea hatutafufuliwa kwenda mbinguni.

Sasa itatufaidia nini kupata majumba tele leo, kupata viwanja vyote leo, kupata wake/ waume wengi leo, kupata umaarufu wote na kisha kupata hasara ya nafsi zetu?..si ni heri niendelee tu kuwa maskini lakini nisiikose mbingu…Kwasababu kama umaskini wangu utanifanya nimsogelee Mungu Zaidi, kama utanifanya muda wangu mwingi niutumie kwa Bwana, kama utanifanya nisiwe mtu wa kula rushwa au kupokea rushwa ni heri niendelee kuwa maskini lakini niwepo miongoni mwa wale watakaokwenda na Bwana siku ile..Kwa maana najua utajiri nitakaokuwa nao kule hautalinganishwi ni utajiri wa kupita wa hapa duniani.

Kwa kumalizia mstari huo mstari hapo juu unasema..

Ufunuo 21:5  “Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.

6  Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.

7  Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.

8  Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”

Maji ya UZIMA YANAPATIKANA BURE…kama hujaokoka, mlango wa wokovu upo wazi sasahivi..kwasababu bado huijui baadaye yako pengine umebakisha masaa tu ya kuishi, hivyo okoka leo..pale ulipo jitenge dakika chache omba toba kwa Mungu wako kwa yote na Maisha yote ya dhambi uliyokuwa unayaishi huko nyuma..Tubu kwa kumaanisha kabisa na kwa vitendo..dhamiria kuacha kuanzia leo pombe, rushwa, sigara, zinaa, wizi, uvaaji vimini, na suruali na uwekaji wa makeup kwenye uso wako..dhamiria kuacha yote hayo na kisha katafute ubatizo sahihi ukabatizwe..kumbuka ubatizo sahihi sio wa kunyunyiziwa..kama ulinyunyiziwa basi ulifanyiwa hivyo kimakosa..hivyo unapaswa ukabatizwe tena katika ubatizo sahihi wa maji tele (Yohana 3:23) na kwa Jina la Yesu Kristo kwaajili ya ondoleo la dhambi zako (Marko 16:16, Matendo 2:38, Matendo 8:16, Matendo 19:5, na Matendo 10:48). Na Bwana mwenyewe kupitia Roho Mtakatifu atakayeingia ndani yako atakuongoza kufanya yaliyosalia yaliyo mapenzi yake.

Wote tufike mbinguni..AMEN.

Bwana akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

WALE WAZEE ISHIRINI NA WANNE (24), WANA KAZI GANI?

NGUVU YA HEKIMA NA AKILI

NINI MAANA YA UCHAWI?

Inaruhusiwa Kula nyama ya Nguruwe kwa Mkristo wa Kweli?

Petro aliambiwa na Bwana Yesu UKIONGOKA WAIMARISHE NA NDUGU ZAKO. Je! kuongoka maana yake nini?

KWANINI MAISHA MAGUMU?

LULU YA THAMANI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments