NINI MAANA YA UCHAWI?

NINI MAANA YA UCHAWI?

JIBU: Katika ukristo kitendo chochote cha kutafuta msaada wa rohoni au mwilini kwa kupitia nguvu nyingine mbali na nguvu za Mungu, biblia inakiita Uchawi,…Na ni wazi kuwa hakuna nguvu nyingine iliyo kinyume na Mungu zaidi ya nguvu za shetani, Na uchawi kwa ujumla umebeba mambo mengi, kuloga, kuagua, kutazama utabiri wa nyota, kubashiri, kusihiri, kuabudu sanamu, hata kuamini baadhi ya movie au magemu ambayo yanatoa maagizo fulani kukuaminisha kuwa unaweza kupata maelekezo ya maisha yako mbali na nguvu za Mungu ni uchawi n.k. vipo vingi, kwa ujumla vyote hivyo vinaitwa uchawi.

Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.’’

Hivyo katika biblia uchawi umekemewa sana, tangu kipindi cha wana wa Israeli kuingia nchi ya Kaanani Mungu aliwaonya sana, mtu yeyote miongoni mwao asionekane anafanya mojawapo ya mambo hayo, Ni jambo ambalo lilikuwa linamuudhi Mungu kiasi kwamba adhabu yake ilikuwa ni kifo tu (Walawi 20:27, Kutoka 22:18)

Vile vile Biblia katika agano jipya inatuaeleza pia mtu yeyote anayejihusisha na uchawi hawezi kuurithi ufalme wa mbinguni..

Ufunuo 22:14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.

15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

Kama tulivyoona hapo juu kujihusisha na uchawi sio tu kupaa na ungo, lakini pia hata kwenda tu kwa mganga tayari wewe ni mchawi, hata tu kuamini kuwa ipo nguvu nyingine mbali na nguvu ya Mungu inayoweza kukuongoza, au kukutabiria mambo yako, au kukusaidia kuamua mambo fulani tayari ni uchawi, kuamini kama mti Fulani au ua Fulani au nguo Fulani au tarehe Fulani, au mwezi au jua vinaweza kukuletea bahati nzuri au mbaya, huo tayari ni uchawi ambao unaangukia katika lile kundi la kutazama nyakati mbaya (Kumb 18:10) sehemu yako siku ile itakuwa ni katika lile ziwa la moto. Wewe na Yule mchawi anayewanga usiku hamna tofauti.

Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”

Hivyo kama wewe upo huko, au ulishawahi kujihusisha na mojawapo ya mambo kama hayo, unachopaswa kufanya ni kuamua kuacha kufanya hivyo tena, na kisha unatubu kwa kudhamiria kuacha kabisa hayo mambo kisha nenda kachome vitu hivyo, au katupe, halafu mfuate mchungaji wako au mtumishi yeyote mwaminifu wa Mungu akuombee, ili Roho wa Mungu aje juu yako, Kisha nawe utakuwa mmojawapo wa wana wa NURU. Lakini ukiendelea na mambo hayo, fahamu kuwa ukifa leo ni moja kwa moja kuzimu. Kwasababu ufalme wa giza ni kinyume na ufalme wa Nuru.

Ubarikiwe.

Kwa Maombezi/Ushauri/Maswali/ Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba 

+25683036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


 

Mada Nyinginezo:

JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?

JE NI KWELI MTU ANAWEZA KUCHUKULIWA MSUKULE?

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

NYOTA ZIPOTEAZO.

JINSI ITAKAVYOKUWA KATIKA SIKU ILE.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Uwezo ni nini?

Jibu hapa
0692667266