Lakini kama leo hii wewe ni mlevi, ni mwasherati, ni mzinzi, ni mtukanaji, mvaaji wa vimini, mtazamaji wa pornography na bado unajiita mkristo, unategemea mtakatifu gani akutokee siku ile?. Ni dhahiri kuwa haitakuhusu hivyo itakujia kama mwivi tu, kama leo hii tu unajitenga na watakatifu kutokana na uvaaji wako, na ulevi wako, na tabia zako,na anasa zako, kama umeshindwa kuungana nao hapa, utawezaje kuungana nao kule,?, utawezaje siku ile kutokewa na mtume Paulo, mtume Petro, Musa, Stephano, utawezaje siku ile kumwona mchungaji wako aliyekuwa akikufundisha na kukuonya uache dhambi na ukawa unakataa?. hatua ndogo tu kama hiyo ya kuwaona watakatifu ni shida, unategemea vipi kumwona BWANA mwenyewe MFALME WA WAFALME atakapokuja pale mawinguni..?.