Je! Kiongozi wa dini anaouwezo wa kusamehe dhambi?

Je! Kiongozi wa dini anaouwezo wa kusamehe dhambi?

SWALI: Je! Ni sahihi kwenda kumfuata kiongozi wa dini kwa mfano Padre na kumpigia magoti kumweleza dhambi zako?.kwasababu imeandikwa “Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa;(Yohana 20:23)”

JIBU: Kwa kuongezea hapo Bwana Yesu pia alisema..

Mathayo 16:15 “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?

16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.

17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.

18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

19 NAMI NITAKUPA WEWE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI; NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGWA MBINGUNI, NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGUA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGULIWA MBINGUNI.”

Hapo tunaona Petro alipewa funguo za ufalme wa mbinguni za kufunga na kufungua,(ambazo ni sawasawa tu na kumwondolea na kumfungia mtu dhambi) na vivyo hivyo na mitume wengine wote waliosalia walipewa funguo hizo hizo, lakini haikuwa na maana kuwa “wanao uwezo wa kumwondolea mtu dhambi kwa kumtamkia tu basi” hapana! bali walipewa “FUNGUO” za kumfanya mtu kuondolewa dhambi zake(UELEWA),, na ndio maana Petro na mitume wengine walipowahubiria watu na kuamini moja kwa moja waliwaambia WATUBU na WAKABATIZWE KILA MMOJA WAO KWA JINA LA YESU KRISTO ili dhambi zao ziondolewe (Matendo 2:38) lakini hawakuwaambia..”Njooni sisi tumepewa uwezo wa kuwaondolea dhambi zenu hivyo pokeeni msamaha”….

Unaona hapo huo ufunguo ni UFUNUO/UELEWA wa jinsi ya kufanya dhambi za mtu ziondolewe, Na ndio huo wa kumuhubiria mtu atubu, kisha akishatubu akabatizwe, hapo ndipo dhambi zake zitakuwa zimeondolewa.

Lakini Papa na Mapadre, na baadhi ya viongozi wengine wa kidini hawafanyi kama mitume walivyofanya bali wao wanawatamkia tu watu kwamba wamesamehewa dhambi zao basi, bila kufuata mwongozo sahihi kwa kisingizio cha hayo maandiko ya kwamba wao wamepewa hayo mamlaka….(kutokana na kukosa UFUNUO wa Roho Mtakatifu ndani yao wanayatafsiri maandiko kwa akili zao ili kutimiza matakwa yao wenyewe.) Mungu atusaidie. Kwahiyo kiongozi yeyote wa kidini akikwambia umesamehewa dhambi zako, pasipo toba binafsi na ubatizo sahihi matamshi yake ni batili yakatae.

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

JE KUNA ANDIKO LINALOMRUHUSU MWANAMKE KUWA SISTER?

KATIKA MARKO 2:2-12, KWANINI BWANA YESU ALICHUKUA HATUA YA KUSAMEHE DHAMBI KWANZA KABLA YA KUMPONYA YULE KIWETE?

KWANINI MTUME PAULO HAKUMSAMEHE MARKO, PINDI WALIPOTAKA KWENDA WOTE KAZINI?

CHUKIZO LA UHARIBIFU

 


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Haya ni mafundisho ya kweli kabisa ubarikiwe sana mtumishi

Paul lavvino
Paul lavvino
1 year ago

Ubarikiwe mtumishi wa mungu

Imani Ruzamuka
Imani Ruzamuka
4 years ago

Asante sana