Kwanini Mtume Paulo hakumsamehe Marko, pindi walipotaka kwenda wote kazini?

Kwanini Mtume Paulo hakumsamehe Marko, pindi walipotaka kwenda wote kazini?

Matendo 15:37 ″Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao.

38 Bali Paulo HAKUONA VEMA kumchukua huyo aliyewaacha huko pamfilia,asiende nao kazini.

39 Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana….”

JIBU: Ukisoma kitabu cha Matendo 13:13 utaona Yohana, aliwaacha wakina Paulo na Barnaba huko Pamfilia, inaonekana aliogopa dhiki itakayokwenda kuwakuta mbeleni, kwasababu Paulo bado mzigo wa kupeleka injili duniani kote alikuwa nao, hivyo walipomsihi waende pamoja alikataa, lakini sasa baadaye tunakuja kumwona tena akikutana na mtume Paulo na Barnaba na kutaka kujumuika nao katika kwenda kuipeleka injili, na ndio hapo tunaona mtume Paulo hakukubali jambo hilo kwasababu kama alishindwa kuandamana nao wakati wa tabu za awali,

kadhalika hataweza kushikamana nao katika dhiki zinazofuata, hivyo sio kwamba Paulo hakumsamehe, alimsamehe lakini hakutaka kuambatana naye tena ili asiwe kikwazo cha injili kwenda mbele.

Ni mfano tunaopaswa tujifunze na sisi [watumishi wa Mungu], kazi ya Mungu si ya kuifanya kirafiki tu, hapana bali wale watakaoitenda kazi kiuaminifu ndio tuambatane nao na kuwatambua hata kama watakuwa si watu wetu wa karibu sana. Lakini ikiwa ni ndugu halafu anaipuuzia kazi ya Mungu, hapo ni kumweka kando, Biblia ilishasema

Wafilipi 2: 12 “…utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu”

Mungu akubariki.

Mada zinazoendana:

DHAMBI YA MAUTI

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!

KWANINI PALE BWANA ALICHUKUA HATUA YA KUMSAMEHE DHAMBI KWANZA KABLA YA KUMPONYA YULE MTU MWENYE KUPOOZA?.

UTAJI ULIOKUWA JUU YA USO WA MUSA.

JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

AGIZO LA UTUME.

USIPIGE MATEKE MCHOKOO!


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Leave a Reply