Inaruhusiwa Kula nyama ya Nguruwe kwa Mkristo wa Kweli?

Inaruhusiwa Kula nyama ya Nguruwe kwa Mkristo wa Kweli?

1).Inaruhusiwa Kula nyama ya Nguruwe kwa Mkristo wa Kweli? 2).Mkristo wa Kweli Anaruhusiwa Kunywa Pombe/kuvuta sigara? 3).Ubatizo Wa Mkristo Wa Kweli Ni Wa Namna Gani?

JIBU: Kwa ufahamu hakuna tatizo lolote kula nyama ya nguruwe au chakula chochote ambacho mtu anaweza kukipokea kwa shukrani mbele za Mungu…biblia inasema viumbe vyote vimetakaswa na Mungu, Tukisoma

1Timotheo 4:1-5 inasema..

“Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru WAJIEPUSHE NA VYAKULA, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.

4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; 5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.”

Hivyo vyakula vyote ni halali lakini biblia inasema tule tu kwa IMANI, ila tukila kwa mashaka ni dhambi, na pia biblia inasema anayekula asimuhukumu yeye asiyekula, wala asiyekula asimuhukumu anayekula, kwasababu tumetofautiana ujuzi, haupaswi kumkwaza mwenzako(Ndugu yako) kwa ujuzi ulionao, ukimkosea mwenzako kisa hali nguruwe ni sawa na kumkosea Kristo mwenyewe

1wakorintho 8:13 inasema “Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.”…..

8:8 Lakini chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu.    

Hivyo tunafundishwa tuwe na hekima tunapokuwa katikati ya jamii fulani ya watu, iwe ni wakristo au isiwe wakristo, sio tunapofika mahali na kukuta jamii fulani hawali chakula fulani (nguruwe), na sisi tunaanza kula mbele yao na kuwaudhi. Hivyo ni sawa na kumkosea Kristo, ndio maana Paulo anasema ni “heri nisile nyama kabisa kama itakuwa ni kikwazo kwa ndugu yangu.”  

Na pia tukisoma.

Warumi 14:14 “Najua, TENA NIMEHAKIKISHWA SANA KATIKA BWANA YESU, YA KUWA HAKUNA KILICHO NAJISI KWA ASILI YAKE, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.

15 Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.

16 Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.

17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. ” 

Hivyo katika agano la kale Mungu kukataza vyakula fulani visiliwe ni kwa ajili ya kutufundisha sisi wa agano jipya mambo kadha wa kadha, kwamfano, kama vile Bwana alivyotenga vyakula najisi na visafi, ilifunua rohoni kuwa kuna vyakula vilivyo visafi na najisi (mafundisho) hivyo wajitenge na vile vichafu, na kudumu katika vile vilivyo safi, kadhalika pia, ilifunua aina mbili za watu yaani waliowasafi(wayahudi), na walionajisi kwa wakati ule (mataifa) lakini Bwana alipokuja aliwatakasa wanadamu wote,(soma Matendo 10:9) kama aliwatakasa wanadamu je! si zaidi viumbe vyake vyote?..n.k.  

2) Mkristo wa kweli haruhusiwi kunywa pombe wala kuvuta sigara wala kuuharibu mwili wake kwa namna yoyote ikiwemo kuchora alama kwenye miili(Tatoo),uzinzi, mustarbation n.k. kwasababu biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, hivyo hekalu la Mungu lazima liwe ni safi.

 1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, MUNGU ATAMHARIBU MTU HUYO. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.

  3) Kuhusu ubatizo, ubatizo sahihi kulingana na maandiko ni wa kuzamishwa katika maji mengi, na inapaswa iwe ni katika JINA LA YESU KRISTO, kulingana na maandiko na sio kwa jina la BABA na Mwana na Roho Mtakatifu, kama inafanyika kimakosa na makanisa mengi, kwa ufafanuzi mrefu kuhusu UBATIZO SAHIHI fuata link hii  >> https://wingulamashahidi.org/2018/07/19/ubatizo-sahihi/

Ubarikiwe sana.


Mada zinazoendana:

USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.

BWANA YESU ANAMAANISHA NINI KUSEMA MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE?

UMEITIKIA WITO INAVYOPASWA?

BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.

MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

5 comments so far

ProsperPosted on11:58 pm - Apr 6, 2023

Vipi sasa kuhusu Ili andiko mimi sijaielewa vizuri ni fafanulia
Kumbukumbu la torati 14:8 inasema
Na nguruwe,kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui,huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse

Japhet nyangaPosted on8:20 pm - Nov 6, 2022

Ndo kwa imani ya maelezo yako unamaanisha bibilia inaruhusu kula kila kiumbe akiwemo nguruwe?

Erastus oumaPosted on3:22 pm - Mar 22, 2022

Asante sana ndugu zangu watanzania naomba kujua njia ya kumjua Mungu kama mwokozi wa maisha yangu

elifurahaPosted on5:48 pm - Dec 8, 2021

Agizo la Yesu Kristo kwenye Mathayo 28: 18-20 inasemaje kuhusu kubatiza?
“Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, nendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”.
kwa ufupi ni kwamba Mungu Baba, Mwana (Yesu Kristo) pamoja na Roho Mtakatifu wote ni wamoja yaani hunia mamoja, hupatana kwa shauri moja. Hivyo Kubatizwa kwa Jina La Yesu Kristo ni sawa na Kubatizwa kwa majina yote matatu. ubarikiwe sana

Leave a Reply

UTAPENDA KUCHANGIA HUDUMA HII?

Tutamshukuru Mungu kwa ajili yako, kwa mchango wako, ili kuifanya injili hii isonge mbele Tuma sadaka yako kwa namba hizi:
Airtel:+255789001312 -Devis Magembe
Mpesa: +255767992434-Denis Magembe