Naomba kujua watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?

Naomba kujua watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?

JIBU: watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?..Ni swali ambalo halikuulizwa tu na watu wa kipindi cha Bwana Yesu pekee lakini hadi sasa swali hilo linaulizwa na wengi..

Tukisoma

Luka 13:23 ″Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache?   Akawaambia,

24 Jitahidini kuingia katika MLANGO ULIO MWEMBAMBA, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.

25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;

26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.

28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. ”

  Ukisoma tena..Mathayo 7:13 -14 Inasema..

13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Maandiko hayo yanaeleza wazi kabisa kwamba watakaokolewa ni WACHACHE, kwasababu njia imesongwa sana! lakini swali linakuja je hii njia imesongwa na nini? Ni wazi kabisa imesongwa na mambo mengi ya ulimwengu huu ambayo ni, anasa, upendaji fedha kupita kiasi, wivu, chuki,tamaa, uasherati uliokithiri ambao sasa upo mpaka kwenye mitandao mambo ambayo hapo zamani hayakuwepo, mitindo ya wanawake kutembea nusu uchi, burudani na miziki ya kidunia,ufisadi n.k. na zaidi ya yote ni kuongezeka kwa wimbi kubwa la manabii wengi wa uongo na hivyo kuifanya ile njia ya kweli isitambulike kirahisi, kwasababu imechanganyikana na njia nyingine nyingi za uongo mambo ambayo hapo nyuma hayakuwepo, na jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo ile njia ya ukweli inavyozidi kuwa nyembamba zaidi, imefikia hatua ya kwamba ukristo wa leo unapimwa na kiwango cha mafanikio ya kidunia aliyonayo mtu na sio mafanikio ya kiroho (yaani utakatifu), Neno la kweli limetupwa nje!.  

Bwana Yesu Kristo aliweka wazi pale aliposema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa siku za kuja kwake mwana wa Adamu? je! katika siku za Nuhu waliokoka watu wangapi? tunaona waliokoka watu 8 tu kati ya mabilioni ya watu waliokuwepo duniani wakati ule..na tena alisema kama ilivyokuwa katika siku za Lutu ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adama..je! wakati wa Lutu walipona watu wangapi?..Jibu ni dhahiri kuwa ni walipon watu 3 tu kati ya mamilioni waliokuwa wanaishi Sodoma na Gomora wakati ule. Na kumbuka Bwana Yesu hawezi kusema uongo,kizazi cha Nuhu na Lutu kimefananishwa na kizazi chetu.  

NA NI KWELI KABISA! watakaookolewa katika kizazi hiki cha mwisho tunachoishi ni WACHACHE MNO!!! Hivyo ndugu tujitahidi tuwe kati ya hao wachache watakaokolewa kwa kupita hiyo njia nyembamba iliyodharauliwa na kuchekwa na ulimwengu wote nayo ni UKRISTO ULE WA MTINDO WA KALE WA MITUME..ikiwa wewe ni mwanamke tupa nguo za kizinzi uvae kama mwanamke wa kikristo mwanamke wa kikristo havai vimini, suruali wala kaptula, hapaki wanja wala lipsticks, mwanamume wa kikristo hanywi pombe, sio mtukanaji, mkristo yoyote hapaswi kupenda mambo ya ulimwengu? Bwana Yesu alisema itakufaidia nini kuupata ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi yako.? Ni wakati wa kutafuta vitu vya kimbinguni ile siku ile isitujie kama mwivi. Muda umeenda sana tunaishi katika kizazi kibaya kushinda vyote, tuwe macho Bwana yu mlangoni kuja. Amen.  

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

UNYAKUO.

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA

SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!

WAFALME WATOKAO MAWIO YA JUA.


Rudi Nyumbani:

 

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments