Katika Marko 2:2-12, Kwanini Bwana Yesu alichukua hatua ya KUSAMEHE dhambi kwanza kabla ya kumponya yule kiwete?

Katika Marko 2:2-12, Kwanini Bwana Yesu alichukua hatua ya KUSAMEHE dhambi kwanza kabla ya kumponya yule kiwete?

JIBU:Tukisoma

Marko 2:2 “Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake.

3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.

4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.

5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.

6 Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao,

7 Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?

8 Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu?

9 Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?

10 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza),

11 Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.

12 Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe..”  

Ukichunguza hapo utaona kuwa jambo la kwanza; Bwana aliona Imani yao kwake, aliona ndani yao walikuwa na kitu cha ziada zaidi ya imani ya kuponywa, nayo ni Imani kwa Yesu Kristo…..Na tunajua kitu cha kwanza kilichomleta Bwana Yesu duniani ni kuokoa dhambi za watu, na vitu vingine baadaye… Ukisoma

Yohana 8:24 Bwana aliwaambia makutano ..

“Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu”

Unaona hapo? Ni lazima uwe na imani ya kumwamini mwana wa Mungu kwanza ndipo upate uzima… Inakupasa uamini kwanza. Na ndio maana jambo la kwanza alilolitamka yeye kama mkuu wa uzima wa roho za watu mara baada ya kuona Imani yao kwake, akamwambia sasa yule aliyekuwa amepooza..UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO…..Ni Neno zuri na la neema kiasi gani!!!   Lakini wale wengine waliokuwa pale mawazo yao yalikuwa tofauti, wao walitazamia tu, Bwana amponye yule mtu kisha amwambie nenda zako, halafu yule mtu akaendelee kuishi maisha ya dhambi kisha mwisho wa siku afe aende kuzimu!..na uponyaji wake wa mwili usimfaidie kitu baada ya maisha ya hapa duniani. Sasa Ukiendelea kusoma pale utaona Bwana anawauliza tena wale watu,

Marko 2:9 “VYEPESI NI VIPI, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?

Unaona hapo, …Kwa mtu mwenye akili na anayethamini maisha yake ya rohoni atagundua kuwa ni afadhali usipone ugonjwa wako, lakini usamehewe dhambi zako…kuliko kuponywa halafu dhambi zako ziendeleee kubaki! Na ndio maana Bwana alimchagulia fungu lililo jema la kusamehewa dhambi zake kwanza, kisha baadaye aje amponye…   Na ndivyo tunavyopaswa na sisi kama wakristo kufanya hivyo sasahivi kama Bwana Yesu alivyofanya, tunakimbilia kuwaombea watu magonjwa ,kupokea miujiza, na mafanikio tunasahamu kuwafundisha watu habari za msamaha wa dhambi ambao ndio msingi wa Imani ya kikristo..

VYEPESI NI VIPI??? Ni heri tukamuhubirie mtu habari za msamaha na toba, aokolewe roho yake hata kama hatapokea uponyaji, kuliko kuhubiri kila siku mimbarani pokea miujiza huku bado watu wanakufa katika dhambi zao. Ni vema tufanye vyote ikiwezekana kuliko kusahau habari za uponyaji wa roho za watu na kuegemea sehemu moja tu ya miujiza….VYEPESI NI VIPI? .  

Ubarikiwe sana.


Mada zinazoendana:

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!

KISASI NI JUU YA BWANA.

MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.

HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)


Rudi Nyumbani:

 

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments