Mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili

Mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili

SWALI: Bwana alikuwa na maana gani kusema mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili?(Mathayo 5:39)


JIBU: Bwana Yesu aliposema mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili na sawasawa na pale aliposema pia “mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.”

Kama tunavyofahamu ukiwa kama mkristo ni lazima ukutane na vikwazo vingi kutoka kwa wasioamini, Hii ikiwa na maana kuwa kwa kufanya hivyo utakuwa umeushinda uovu na utafanikiwa kuiokoa roho ya mtu huyo badala ya kuingamiza. kwasababu kwa kufanya vile Biblia inasema utakuwa umempalia makaa ya moto kichwani pake,atakuwa akijiuliza kila siku ni kwanini sikutendewa kama mimi nilivyomtendea yeye?. hivyo baadaye atajiona yeye ndiye mwenye makosa na kugeuka na kutubu kwasababu yale makaa ya moto yatakuwa yanachoma ndani yake. Biblia inasema katika..

Mithali 25: 21 “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa;

22 Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na Bwana atakupa thawabu”. 

Lakini sasa mfano atakapokupiga na wewe ukamrudishia, au atakapochukua mali yako nawe ukaenda kuchukua ya kwake, atakapokuabisha na wewe ukamwaibisha, atachomwaje dhamira na kujiona kama yeye ni mwenye dhambi?, hivyo atabakia kuwa vilevile tu na kukuona wewe ni mtu wa kawaida tu kama watu wengine walivyo. Na ndio maana Bwana Yesu alisema tuushinde ubaya kwa wema, ili tuwe wakamilifu kama Baba yetu alivyo mkamilifu. Aliendelea kusema..

Mathayo 5:41 “Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.

42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?

47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?

48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”

 Ubarikiwe sana.


Mada zinazoendana:

KISASI NI JUU YA BWANA.

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!

 KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.

SHUKURU KWA KILA JAMBO.

AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?.

KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Emmanuel Kitengule
Emmanuel Kitengule
1 year ago

Barikiwa sana mwalimu umenifungua ufahamu mpaka nafurahi.Mungu na azidi sana kukuinua katika maarifa yaletayo uzima.

Charles
Charles
2 years ago

Mtumishi wa Bwana kazi yako ni kubwa sana Mungu wetu wa mbinguni awazidishie neema yake ili mzidi kuhudumia kundi lake