Bilauri ni nini kibiblia?(Ufunuo 21:11,22:1)

Bilauri ni nini kibiblia?(Ufunuo 21:11,22:1)

Bilauri ni glasi, Na kama tunavyojua glasi huwa zina mwonekano mzuri wa kung’ara na  wakuvutia, usiositiri uchafu, zimetengenezwa kwa madini yanayoitwa Crystal, tazama picha juu,

Katika biblia sehemu nyingi Neno hili limetumikia, na hiyo ni kufunua uzuri wa kitu, au mtu au Mungu au mahali fulani..Kwa mfano utaona, mstari huu,

Wimbo 7:2 “Kitovu chako ni kama bilauri iliyoviringana, Na isikose divai iliyochanganyika; Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano, Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro”;

Kuonyesha uzuri, aliokuwa nao mpenzi wake anayemzungumzia hapo.

Ukisoma tena;

Mithali 23:31 “Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu”

Pia,

 

 

 

 

Ezekieli 1:22 “Tena juu ya vichwa vya viumbe hai palikuwa na kitu mfano wa anga, kama rangi ya bilauri, lenye kutisha, limetandwa juu ya vichwa vyao”.

Vilevile..

Ufunuo 4:6 “Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma”.

Soma pia; Ufunuo 22:1 na,

Ufunuo 21:10 “Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;

11 wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri”;

Unaona?

Hivyo, kwa ufupi ni kuwa makao tuliyoandaliwa kule mbinguni, hayaelezeki kwa namna ya kibinadamu, na ndio maana utaona hapo biblia inatumia neno “KAMA”, kama Bilauri/glasi, lakini bado bilauri lenyewe halielezea ipasavyo uzuri uliopo kule, hivyo, cha kufanya ni mimi na wewe, tufanye bidii ili tuwe na uhakika kuwa yaliyopo kule hatuyakosi.

Na hiyo inakuja kwanza kwa kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kisha, tukishatubu tunakubali kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi, na kwa jina la Yesu Kristo, kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu, sawasawa na Matendo 2:38, na baada ya hapo Roho Mtakatifu ataletwa ndani yetu, ili kutufundisha na kututia katika kweli yote. Mpaka siku ile ya unyakuo itakapofikia.

Je! na wewe upo tayari kufanya hivyo leo? Kama upo tayari basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba na mambo mengine. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Na Bwana akubariki sana.

Pia angalia maana nyingine za maneno ya biblia chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Zabarajadi ni nini katika biblia (Ufunuo 21:20)?

Neno beramu lina maana gani katika biblia?

JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?

MAJONZI YA MTUME PAULO KWA NDUGU ZAKE.

Kwanini Bwana aliongea na Abramu baada ya kutengeana na Lutu?

MPINGA-KRISTO

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments