Zabarajadi ni nini katika biblia (Ufunuo 21:20)?

Zabarajadi ni nini katika biblia (Ufunuo 21:20)?

Zabarajadi ni nini?


Ni moja ya mawe ya thamani, ambayo yanaonekana yakitajwa sehemu nyingi katika biblia, mawe haya yapo katika rangi mbalimbali, mengine yana rangi kama ya kijani, mengine njano, mengine nyekundu, bluu n.k. tazama picha.

Katika biblia tunaona kile kifuko cha kifuani cha Haruni, kati  ya yale mawe 12 yaliyowekwa pale mojawapo lilikuwa ni hili la zabarajadi(Kutoka 28:20),

hata rangi ya magurudumu katika maono aliyoonyeshwa Ezekieli yalikuwa ya rangi ya  zabarajadi,

Ezekieli 1:16 “Kuonekana kwake magurudumu hayo na kazi yake kulikuwa kama rangi ya zabarajadi; nayo yote manne yalikuwa na mfano mmoja; na kuonekana kwake na kazi yake kulikuwa kana kwamba ni gurudumu ndani ya gurudumu lingine.

 

Ezekieli 10:9 Nami nikaangalia, na tazama, yalikuwako magurudumu manne karibu na makerubi, gurudumu moja karibu na kerubi mmoja, na gurudumu lingine karibu na kerubi mwingine; na kuonekana kwa magurudumu kulikuwa kana kwamba ni zabarajadi.

zabarajadi

Vilevile biblia inaonyesha, msingi wa ukuta wa mji ule wa kimbinguni (Yaani Yerusalemu mpya), nao pia utakuwa umenakshiwa na mawe haya..Japo pia inaweza kuwa ni lugha ya picha kuonyesha uzuri wa makao hayo  jinsi ulivyo na sio mawe halisi, lakini mawe haya ya thamani yametumika katika vifungu hivyo.

Ufunuo 21:18 “Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.

19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;

20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto”.

Soma pia Danieli 10:5-6,

Shalom.

Tazama tafsiri ya mawe mengine, na maneno mengine ya biblia chini;

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Rangi ya kaharabu ni ipi kibiblia(Ezekieli 1:4,27,8:2)?

Rangi ya samawi ni ipi kibiblia(Kutoka 36:37)?

Pomboo ni nini katika biblia?(Kutoka 25:5, Ezekieli 16:10)

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

 

JE! NINYI NANYI MWATAKA KUONDOKA?

MAONO YA NABII AMOSI.

BONDE LA KUKATA MANENO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments