Rangi ya samawi ni ipi kibiblia(Kutoka 36:37)?

Rangi ya samawi ni ipi kibiblia(Kutoka 36:37)?

Rangi ya samawi ni ipi?


Rangi ya samawi ndio rangi ya bluu, Kama unavyoona katika picha, katika biblia rangi hii ilitumika kwa matumizi mbalimbali husasani yale ya madhabahuni pa Mungu (hema ya kukutania na hekaluni),

  • Rangi hii ilitumika kupamba mapazia ya hekalu,(Kutoka 38:18, Kutoka 36:37,)
  • Nyuzi za samawi pia zilitumika kufumia nguo za makuhani,:

Kutoka 39:1 “Na zile nyuzi za rangi ya samawi, na nyuzi za rangi ya zambarau, na nyekundu, wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ustadi sana kwa ajili ya kutumika katika mahali patakatifu, na kuyafanya hayo mavazi matakatifu ya Haruni, vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa.

2 Naye akaifanya hiyo naivera, ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa”.

  • Hata kile kifuko cha kifuani cha Haruni sehemu ya kifuko hicho kilifumwa kwa nyuzi za rangi ya samawi/bluu , na vilevile, yale mawe 12 yaliyowekwa pale kwenye kifuniko hicho, mojawapo lilikuwa ni jiwe la samawi, lijulikanalo kama Yakuti samawi, (Kutoka 39:8-13, Ayubu 28:16) ..Tazama picha.

Haruni

  • Ile meza ambayo iliwekewa mikate ya wonyesho, nguo iliyowekwa juu yake, ilikuwa ni lazima iwe ya rangu ya samawi. Hesabu 4:7
  • Hata kinara cha taa, cha hekalu, na ile madhabahu ya dhahabu viilifunikwa kwa nguo za rangi hii ya samawi/bluu, Hesabu 4:9-11
  • Mungu aliwaagiza pia wana wa Israeli, kila wanapotengeneza mavazi yao, wahakikishe mwisho wa ncha wanafuma vishada vya rangi ya nyuzi za samawi, lengo ni kila wavitazamapo wakumbuke sheria za Mungu na maagizo yake.

Hesabu 15:38 “Nena na wana wa Israeli, na kuwaagiza ya kwamba wajifanyie vishada katika ncha za nguo zao, katika vizazi vyao, tena ya kwamba watie katika kila kishada cha kila ncha nyuzi za rangi ya samawi;

39 nacho kitakuwa kwenu ni kishada, ili mpate kukiangalia, na kuyakumbuka maagizo yote ya Bwana, na kuyafanya; tena kwamba msiende kutanga-tanga kuandama mioyo yenu wenyewe, na macho yenu wenyewe, ambayo mlikuwa mkiyaandama kwa uasherati hapo kwanza”;

vishada vya samawi

  • Vilevile mavazi ya kifalme, yalikuwa na mchanganyiko wa rangi ya samawi.

Esta 8:15 “Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi ya samawi na nyeupe, mwenye taji kubwa ya dhahabu, na joho ya kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa Shushani wakapaza sauti, wakashangilia”.

Hivyo rangi hii ni rangi ya utukufu wa Mungu, hata katika maisha ya kawaida, utaona vitu vingi vya asili Mungu amevipamba kwa rangi hii, ukitazama anga, utaiona, ukitazama bahari utaiona, ukitazama milima, utaiona,..Hivyo uinapo rangi hii jua umeona utukufu wa Mungu.

Bwana akubariki.

Tazama maana za rangi kikiblia chini na tafsiri nyingi za maneno.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MAANA YA RANGI KIBIBLIA.

Bwana Yesu alimaanisha nini aliposema; Mafarisayo Hupanua HIRIZI zao, na kuongeza MATAMVUA yao?

Pomboo ni nini katika biblia?(Kutoka 25:5, Ezekieli 16:10)

JE KUPOKEA CHANJO NI DHAMBI?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments