Je! Kusoma biblia kwenye simu ukiwa kanisani ni dhambi?

Je! Kusoma biblia kwenye simu ukiwa kanisani ni dhambi?

SWALI: Je! Kusoma biblia kwenye simu ukiwa kanisani, au sehemu yoyote ile ni dhambi? au kutumia Tablet madhabahuni, pia hilo nalo ni dhambi?


JIBU: Ili tupate jibu sahihi la swali hili, hebu tulihamishe na kumwuliza Mwalimu wa shuleni, Je! Ni vizuri yeye kuwafundisha wanafunzi wake kwa kutumia kitabu au tablet au simu?…Au je ni vizuri wanafunzi wake kumfuatilia anachofundisha kwa kutumia simu zao au tablets zao na si vitabu?.

Kwa Mwalimu yoyote ambaye anajua wajibu wake kamwe hataweza kuruhusu mwanafunzi wake aingie na simu pindi anapofundisha, haijalishi hiyo simu itakuwa na material gani anayoyahitaji yeye..wala yeye mwenyewe hawezi kuwafundisha wanafunzi wake kwa kutumia simu. Ataruhusu wanafunzi wake watumie hizo tablet zao, au simu zao, au ipad au computer baada ya kutoka kwenye masomo au endapo somo analotaka kuwafundisha wanafunzi wake linahusiana sana na hizo simu, au computer, au tablets..Lakini katika hali ya kawaida hawezi kamwe kuruhusu simu darasani kwake. Na lengo la kufanya hivyo sio kwamba simu ni mbaya, hapana!..bali ni kwasababu simu zina vitu vingi ambavyo ni rahisi kumtoa mwanafunzi katika umakini wa darasani, kwasababu wakati mwalimu anafundisha mara meseji imeingia, mara simu imeita, mara imezima chaji ghafla, mara imeganda ghafla n.k..

Tofauti na kitabu, Kitabu hakina muingiliano wa vitu vingi ambavyo vinaweza kuhamisha usikivu na umakini wa mtu. Hawezi mtu kusoma kitabu ghafla kikazima chaji, au kikaleta jumbe nyingi nyingi n.k. Ndio maana mpaka leo kusoma kwa kutumia kitabu imebaki kuwa njia bora na ya umakini kwa wanafunzi.

Na kanisani ni hivyo hivyo, Kanisani ni zaidi ya mashule na madarasa ya kidunia. Mtu anayeingia pale anakwenda kujifunza au kufundisha Elimu ya Mbinguni, ambayo ni kubwa kuliko elimu zote, hivyo umakini mkubwa sana unahitajika kwa anayekwenda kufundisha na anayekwenda kujifunza. Hivyo biblia iliyoandikwa kwenye kitabu Ndio njia bora na itabakia kuwa hivyo mpaka mwisho. Mtu anayefundisha kwa kutumia simu au anayeingia kanisani na simu iliyowashwa, bado hajajua anakwenda kumtafuta nani, na wala hajajua thamani ya Neno la Mungu.

Sasa sio kwamba matumizi ya biblia ya kwenye simu na Tablet na Computer ni mabaya! La si mabaya ni mazuri katika eneo husika, lakini si kanisani..Unaweza kuwa kwenye gari unasafiri umbali mfupi kwenye basi na ukatamani kusoma biblia na huna, hapo unaweza kutumia biblia kwenye simu yako, hali kadhalika unaweza ukawa upo kazini au barabarani na ukakutana na mtu ukamshuhudia na mahali hapo huna biblia ya kuweza kunukuu maandiko, hapo unaweza kutumia biblia ya kwenye simu yako au Tablet yako au ipad yako, kushuhudia au kujikumbusha maandiko. Lakini kanisani ni darasani, na si darasa la kidunia bali la kimbinguni, hivyo panahitajika Kitabu cha uzima kinachoitwa BIBLIA TAKATIFU.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

KAMA MMOJA TU NDIO HIVI! SI ZAIDI 153?

USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.

JE UDHAIFU WANGU UNAWEZA KUZUIA INJILI?

WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.

Je! Bwana Yesu alibatiza akiwa hapa duniani?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Nigundwe nily
Nigundwe nily
3 years ago

Kweli kbs