Maana ya Mafarisayo Hupanua HIRIZI zao, na kuongeza MATAMVUA yao

Maana ya Mafarisayo Hupanua HIRIZI zao, na kuongeza MATAMVUA yao

SWALI: Naomba kufahamu kwanini Bwana wetu Yesu Kristo kwanini amesema “Waandishi na MAFARISAYO wameketi katika KITI CHA MUSA;” basi YEYOTE watakayo watakayowaambia,MYASHIKE na KUYATENDA;LAKINI KWA MFANO WA MATENDO YAO MSITENDE;maana wao hunena lakini hawatendi.Wao hufunga MIZIGO MIZITO na kuwatwika watu mabegani mwao;WASITAKE WENYEWE KUGUSA KWA KIDOLE CHAO.Kwakuwa hupanua HIRIZI ZAO,huongeza MATAMVUA yao”.(Mathayo23:1-5).?

JIBU: Kwanini alisema hivyo sababu ameshaitoa hapo…“hunena lakini hawatendi” hiyo ndiyo sababu akawaambia wanafunzi wake wasitende matendo kama yao.
Na aliposema mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa anamaana mafarisayo na masadukayo, wameisoma sana torati ya Musa na ni wepesi kuhukumu kwa kupitia hiyo torati, hivyo wanakuwa kama wawakilishi wa Musa, jambo lolote likitokea mfano mwanamke kafumaniwa kwenye uzinzi ni rahisi kutumia torati ya Musa kuhukumu,.na hali wao wenyewe ndani ya mioyo yao wanafanya hayo hayo.

Na aliposema wao WANAPANUA HIRIZI ZAO hakumaanisha wao wana hirizi, kama hizi wanazotumia wachawi, hapana! Neno hirizi zamani lilitumika kuwakilisha “kiboksi” kidogo kilichobeba maandishi Fulani madogo ambacho watu walikuwa wanatembea navyo, kama kumbukumbu kila waendapo wasisahau yale aliyoyakusudia kuyafanya au kuyatunza katika maisha yake. Mfano katika dunia ya sasa wanandoa wanavaa pete na kutembea nazo kila mahali,..zile ni hirizi za wakati huu wa sasa, kwamba mtu akiitazama inamkumbusha agano aliloingia yeye na mke wake mbele za Mungu siku ile walipofunga ndoa.

kwahiyo, wana wa Israeli waliamuriwa na Mungu waandike baadhi ya vifungu vya maneno ya torati katika viboksi Fulani vidogo kisha wawe wanatembea navyo popote waendapo, wavivae kama utepe katikati ya macho yao, au mkononi. sasa huo utepe waliokuwa wanauvaa katikati ya kipaji cha uso ndio unaoitwa hirizi.

Tukisoma

(kumbu 6:4-9) “Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.
5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;
7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.

Kwasasa jambo hili limezoeleka kuonekana likifanywa na wachawi, lakini asili ya neno hirizi sio uchawi. Kama vile neno kafara lisivyokuwa la wachawi, shetani anatabia ya kugeuza mambo na kuyafanya yawe yake. Isipokuwa sisi wakristo hatufungi hirizi mwilini bali hirizi zetu [sheria za Mungu] tunazifunga rohoni.

Sasa hawa mafarisayo, wenyewe badala ya kuweka utepe mdogo tu(mfano wa kiboksi kidogo cha nchi 2) katikati ya macho yao, wao waliongeza ukubwa wa utepe likawa ni li-boksi likubwa ili waonekane na watu kuwa ni watakatifu sana,

kadhalika na MATAMVUA yao waliyaongeza, matamvua ni sehemu ya mwisho wa kanzu za wayahudi katika sehemu za mikono, hizo waliamuriwa wazishone wakichanganya na michirizi ya rangi ya samawi(yaani blue), lakini wao wakawa wanashona makubwa kupita kiasi ili waonekane na watu kuwa ni watakatifu zaidi.

Hivyo badala ya hizo hirizi zao kuwa ni za kiasi tu, wao wakaziongeza na kuwa kubwa ili waonekane na watu ni watakatifu zaidi na wanashika sheria zaidi, kadhalika na matamvua yao badala yawe ya madogo kiasi wao wakayafuma na kuwa mafundo makubwa kupita kiasi ili kila mtu atakapowaona waonekane kuwa wanaijua sheria zaidi, ili kuelewa vizuri tazama picha chini…

Huu ni mfano dhahiri, wa viongozi wa kidini na madhehebu na baadhi ya wakristo wa sasa, wanavaa majoho marefu, na misalaba mikubwa, na kubeba biblia kubwa na kujionyesha mbele za watu, nia yao hasaa sio kumtangaza Kristo, hapana bali waonekana na watu kuwa ni watu wa kuheshimiwa zaidi na kuogopwa katika kanisa, nia yao ni kuonyesha vyeo vyao, lakini ndani yao hawayashiki yale wanayoyaonyesha kwa nje.

Hivyo tunafundishwa na sisi pia tusiwe wanafki, kuigiza mambo ambayo sisi wenyewe hatuyatendi ni unafki mbele za Mungu..na itageuka kuwa OLE!! Katika siku ile.

mfano wa matamvua
mfano wa HIRIZI

Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

CHUJIO HILI NI LA AJABU SANA!.

NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!

ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!

NINAJUA MAWAZO NIKUWAZIAYO:

CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.

MELKIZEDEKI NI NANI?


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
James Mageto
James Mageto
2 years ago

Leave your message.Mungu awabariki watumishi kwa kuwa Mafundisho haya ya injili yamenijenga kiroho na nimefundisha wengi pia.Barikiweni

EDGAR OCTAVIAN TEMU
EDGAR OCTAVIAN TEMU
2 years ago

Mbarikiwe na BWANA wa mabwana.