Rangi ya samawi ni ipi kibiblia(Kutoka 36:37)?

by Admin | 24 Septemba 2020 08:46 um09

Rangi ya samawi ni ipi?


Rangi ya samawi ndio rangi ya bluu, Kama unavyoona katika picha, katika biblia rangi hii ilitumika kwa matumizi mbalimbali husasani yale ya madhabahuni pa Mungu (hema ya kukutania na hekaluni),

Kutoka 39:1 “Na zile nyuzi za rangi ya samawi, na nyuzi za rangi ya zambarau, na nyekundu, wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ustadi sana kwa ajili ya kutumika katika mahali patakatifu, na kuyafanya hayo mavazi matakatifu ya Haruni, vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa.

2 Naye akaifanya hiyo naivera, ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa”.

Haruni

Hesabu 15:38 “Nena na wana wa Israeli, na kuwaagiza ya kwamba wajifanyie vishada katika ncha za nguo zao, katika vizazi vyao, tena ya kwamba watie katika kila kishada cha kila ncha nyuzi za rangi ya samawi;

39 nacho kitakuwa kwenu ni kishada, ili mpate kukiangalia, na kuyakumbuka maagizo yote ya Bwana, na kuyafanya; tena kwamba msiende kutanga-tanga kuandama mioyo yenu wenyewe, na macho yenu wenyewe, ambayo mlikuwa mkiyaandama kwa uasherati hapo kwanza”;

vishada vya samawi

Esta 8:15 “Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi ya samawi na nyeupe, mwenye taji kubwa ya dhahabu, na joho ya kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa Shushani wakapaza sauti, wakashangilia”.

Hivyo rangi hii ni rangi ya utukufu wa Mungu, hata katika maisha ya kawaida, utaona vitu vingi vya asili Mungu amevipamba kwa rangi hii, ukitazama anga, utaiona, ukitazama bahari utaiona, ukitazama milima, utaiona,..Hivyo uinapo rangi hii jua umeona utukufu wa Mungu.

Bwana akubariki.

Tazama maana za rangi kikiblia chini na tafsiri nyingi za maneno.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MAANA YA RANGI KIBIBLIA.

Bwana Yesu alimaanisha nini aliposema; Mafarisayo Hupanua HIRIZI zao, na kuongeza MATAMVUA yao?

Pomboo ni nini katika biblia?(Kutoka 25:5, Ezekieli 16:10)

JE KUPOKEA CHANJO NI DHAMBI?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi Nyumbani:

WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/09/24/rangi-ya-samawi-ni-ipi-kibiblia/