Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?

Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?

Marijani ni nini?


Ni madini ya thamani, yenye rangi iliyo katikati ya wa waridi/pinki na nyekundu iliyokolea (rangi ya damu). Yamezoeleka kuitwa kwa jina la kiingereza “Ruby”. Tazama picha juu.

Kwenye biblia madini haya yametajwa sehemu nyingi kufunua vitu mbalimbali;

Kwamfano, katika Ayubu, inasema thamani ya hekima, haiwezi kufananishwa na thamani ya kito chochote, sio dhahabu wala marijani wala chochote, thamani ya hekima ipo mbali sana.

Ayubu 28:17 “Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo; Wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi.

18 Havitatajwa fedhaluka wala bilauri; Naam, kima cha hekima chapita marijani”.

 

Maombolezo 4:7 “Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji, Walikuwa weupe kuliko maziwa; Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani, Na umbo lao kama yakuti samawi”.

 

Ezekieli 27:16 “Shamu alikuwa mfanya biashara kwako, kwa sababu ya wingi wa kazi za mkono wako walifanya biashara kwa zumaridi, na urujuani, na kazi ya taraza, na kitani safi, na marijani, na akiki, wapate vitu vyako vilivyouzwa”.

 

Mithali 3:13 “ Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.

14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.

15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye”.

 

Mithali 8:11 “Maana hekima ni bora kuliko marijani; Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo”.

 

Mithali 20:15 “Dhahabu iko, na marijani tele; Lakini midomo ya maarifa ni kito cha thamani”.

Vilevile biblia inataja ukubwa wa thamani wa mwanamke aliye mwema, na kusema thamani yake ni zaidi ya dini la marijani.

Mithali 31:10 “Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani”.

Hivyo na sisi, tukijikita kuitafuta Hekima, basi ni zaidi ya tunavyoitafuta almasi, au dhahabu, au ruby, au dini lingine lolote, kwasababu thamani na utajiri wa hekima na maarifa, ni wa kudumu, lakini mali na vito ni vya kupita tu.

Na hekima ya Mungu ni YESU KRISTO biblia inatuambia hiyo katika 1Wakorintho 1:23-24

Hivyo ukimpata Yesu kweli kweli katika moyo wako, umepata vyote, vya mwilini na rohoni..

Faidi yako ni kuwa hata ukifa unaouhakika wa uzima wa milele.

Swali ni je! Mimi na wewe tumeshamkaribisha Yesu maishani mwetu? Kama sivyo basi huu ndio wakati. Hivyo ikiwa utapenda kufanya leo uamuzi huo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tazama maana ya mawe mengine katika biblia, pamoja na masomo chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Bilauri ni nini kibiblia?(Ufunuo 21:11,22:1)

Zabarajadi ni nini katika biblia (Ufunuo 21:20)?

NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO?

NGUVU YA HEKIMA NA AKILI

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments