NANGA YA ROHO, YENYE SALAMA.

NANGA YA ROHO, YENYE SALAMA.

Shalom, Karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya Bwana wetu.

Ndugu, ukilikosa tumaini ambalo linapatikana kwa YESU tu peke yake, ni ngumu kuimaliza hii safari yako hapa duniani salama, haijalishi utajifanya una furaha kiasi gani, furaha hiyo ni feki ndugu yangu, huwezi kuushinda huu ulimwengu uliojaa vishawishi na shida na taabu, na mitego mingi ya adui, huwezi..Haijalishi utasema nina pesa nyingi kiasi gani, bado utafika mahali utachukuliwa na maji tu, hata ukimtegemea mwanadamu Fulani, bado uzima wa milele hutaweza kuupata.

Na ndio maana kuna wakati Bwana Yesu alisema ili nyumba iwe salama, ni lazima ijengwe kwanza juu ya msingi, vinginevyo ikijengwa bila msingi upo wakati hata upepo wa kasi ukivuma tu, nyumba hiyo itakuwa gofu.. Na msingi huo ni Yesu Kristo. Soma..

Mathayo 7:24 “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba”.

Lakini pia upo wakati utapitia mahali ambapo huwezi kuchimba msingi chini yako, kwasababu chini yapo maji mengi, ipo bahari, lipo ziwa, n.k. kwamfano wanaosafiri kwa meli, wanajua ili kujilinda na hatari ya upepo mkali au dhoruba, inawapasa watembee na kifaa kingine cha kipekee , kinachoitwa NANGA.

Nanga kazi yake ni kwenda chini sana, kuhakikisha inashuka mahali ambapo bahari au ziwa linaishia,  na kukutana na mwamba chini, kisha inajikita pale,, sasa ikishanasa  hapo hata dhoruba ya upepo mkali ikipita kule juu ni ngumu kikipindua chombo..

Sifa ya Nanga ni kuwa inakwenda mbali sana, kutafuta msingi.. Jambo ambalo kitu kingine chochote hakiwezi kufanya..msingi wa nyumba unashuka mita mbili tatu, lakini nanga inashuka hata mita 300 au 500, kutafuta mwamba.

Ndivyo ilivyo kwa mtu aliyempokea Yesu kwa moyo wake wote leo,..Mungu anachofanya kuanzia huo wakati  ni kuwa  anamshushia nanga ya roho , inayoitwa TUMAINI, ambayo hiyo inakwenda moja kwa moja mpaka kwenye  moyo wa Kristo (Mwamba halisi), kukuanganisha wewe na yeye, kiasi kwamba hata mawimbi makali vipi yaje mbele yako, hayawezi kukugharikisha..japokuwa chini yako hakuonekani msingi wowote.

Utapitia misukosuko ya kila namna, utapitia dhiki, utapitia kuumizwa, utapitia kila aina ya taabu kwa ajili ya imani yako, lakini kung’olewa katika mstari wa wokovu ni jambo ambalo halitawezekana daima.. Watu wataangalia msingi wako mbona hatuooni, wataoni ni kikamba tu kidogo kimeshuka majini, lakini huko chini  kuna chuma kizito kinene, kimejikita kwenye mwamba mgumu sana (Yesu Kristo) Kiasi kwamba huwezi kutikiswa, na wimbi lolote la ibilisi.

Waebrania 6:18 “….sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;

19 TULIYO NAYO KAMA NANGA YA ROHO, YENYE SALAMA, YENYE NGUVU, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia,

20 alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki”.

Lakini kama hujampa Kristo maisha yako, au upo vuguvugu tu, yaani mguu mmoja nje, mwingine ndani, haueleweki, basi Tumaini hili Mungu hawezi kuliweka ndani yako..Na ndio hapo utashangaa, mtu dhoruba kidogo tu imemjia kashaurudia ulimwengu, ni kwasababu hakuchagua kumfuata Yesu kwa moyo wake wote..Nanga ile haikushushwa kukutana na mwamba usiotikisa ulionana chini ya bahari.

Ndugu wokovu ni jambo halisi sana, na ni nguvu ya Mungu kwelikweli, mtu yeyote anayedhamiria kumfuata Yesu, nanga hii ni lazima atashushiwa asilimia mia. Usijitumainishe na dini, au dhehebu, au mtu yeyote anayejiita mtume au nabii, au chochote kile, vyote haviwezi kukuokoa hapa duniani ni Kristo tu peke yake.

Na wokovu unakuja kwa kuamini, na kubatizwa, unapooamini moja kwa moja unakuwa tayari na kwenda kubatizwa pia katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO. Na baada ya hapo unaanza kuishi maisha ya mtu kama aliyeokolewa..

Hapo ndipo Mungu analeta tumaini hili ndani yako, ambalo wimbi lolote la adui halitaweza kukuondosha..

Hivyo kama wewe upo nje ya Kristo au ulikuwa vuguvugu na ndio maana ulimwengu ukakushinda, ni wakati wako sasa huu kufanya uamuzi sahihi, dhamiria wewe mwenyewe kwanza kutoka katika moyo wako, kisha piga magoti tubu kuonyesha kwamba unahitaji msaada kutoka kwa Mungu, na kukiri makosa yako, kisha anza hatua za kutafuta ubatizo sahihi wa kuzamishwa kwenye maji mengi (kama utahitaji wasiliana nasi),.Na baada ya hapo anza kuishi maisha yanayoendeana na toba yako..

Na kuanzia huo wakati na kuendelea utaona mabadiliko makubwa maishani mwako kwa Yule Roho Mtakatifu atakapokuwa ameletwa ndani yako.. Kwasababu wokovu una nguvu zaidi ya jambo lingine lolote hapa duniani.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Daawa ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

Naomba kujua nini maana ya kuteguka uvungu wa paja?

JE! KUNA UCHAWI KATIKA KUTENDA WEMA?

JIEPUSHE NA UNAJISI.

WEWE NI BWANA UNIPONYAYE.

Naomba kujua nini maana ya kuteguka uvungu wa paja?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments