Kwanini Bwana aliongea na Abramu baada ya kutengeana na Lutu?

Kwanini Bwana aliongea na Abramu baada ya kutengeana na Lutu?

Mwanzo 13:14 Bwana aliongea na Abramu Alipotengana na Lutu na kumpa nchi. Sasa ni kwanini aongee naye baada tu ya wao kutengana?. inamana uwepo wa Lutu ulimzuia Mungu kumpa nchi Abramu?.


JIBU: Tatizo halikuwa kwa Mungu, bali kwa Ibrahimu. Yale mazingira aliyokuwa nayo Ibrahimu ndiyo yaliyokuwa kikwazo cha Mungu kuzungumza naye kwa wakati.

Jambo hilo halikuanzia hapo, utaona tangu Mungu alipomwambia atoke kule Uru ya ulkaldayo, Badala atoke yeye peke yake alitoka na baba yake ambaye alikuwa ni mpagani-mwabudu miungu, na hiyo ikamfanya akae sehemu moja iliyoitwa Harani kwa muda mrefu bila Mungu kuzungumza naye.. Na siku tu baba yake alipokufa ndipo Mungu akazungumza naye tena na kumwambia aondoke pale aende katika nchi ya Kaanani..Jambo ambalo lingepaswa liwe ni la safari ya moja kwa moja, lakini lilimfanya awe mtu wa vituo vituo kwa muda mrefu. Ni wazi kuwa baba yake alimpinga vikali sana, kwa mambo mengi.

Matendo 7:3 “akamwambia, Toka katika nchi yako na katika jamaa zako, ukaende hata nchi nitakayokuonyesha.

4 Ndipo alipotoka katika nchi ya Wakaldayo, akakaa Harani, akatoka huko baada ya kufa babaye, Mungu akamhamisha mpaka nchi hii mnayokaa ninyi sasa”.

Lakini hakuondoka peke yake tena kule Harani bali aliondoka na mjomba wake Lutu..Na walipofika huku, Mungu hakujifunua kikamilifu kwake mpaka walipotengana tena, ndipo baadaye Mungu alipoona utulivu wake sasa kazungumza naye tena.

Hiyo ni desturi ya Mungu tangu zamani. Akikuita unapaswa uondoke wewe kama wewe na kumfuata, kwasababu ukienda na mtu mwingine ambaye hana Habari na Mungu, ni wazi kuwa atakuja kuwa kikwazo kikubwa kwako huko mbeleni, unaweza wewe kutamani hivi, yeye atatamani kile, wewe ukiwaza muda huu nikasali, au nikashuhudie yeye akafikiri vile mkafanye biashara, na hiyo inakuwa kikwanzo kikubwa sana cha Mungu kuyatimiliza yale maono aliyoyaweka ndani yako.

Na ndio maana Bwana Yesu alisema, nimekuja kuleta upanga duniani….

Mathayo 10:34 “Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.

35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;

36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.

37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili”.

Hivyo tukitaka tufike mbali, au tukitaka Mungu atutumie ipasavyo hatuna budikuweka mbali vitu au kujitenga na watu ambao tunaona kabisa wanaweza kuathiri mwito wetu kiuwepesi.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Je! Ule mwiba uliokuwa katika mwili wa Paulo ulikuwa ni nini?

JINSI DHAMBI INAVYOMGHARIMU MTU SANA.

Maana ya ‘Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake’

Je! Ule mwiba uliokuwa katika mwili wa Paulo ulikuwa ni nini?

NINI NI KILICHOMFANYA IBRAHIMU AKUBALI KUMTOA MWANAWE SADAKA?

Kwanini Mungu aliikubali sadaka ya Yeftha ya kumtoa binti yake kafara?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments