UTUKUFU NA HESHIMA.

UTUKUFU NA HESHIMA.

Utukufu na Heshima.


Mungu wetu ndiye anayestahili utukufu na heshima yote..biblia inatuambia hivyo katika..

Ufunuo 4:11  “Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea UTUKUFU NA HESHIMA na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa”.

Lakini Pamoja na hayo Mungu wetu sio mchoyo, yupo tayari kumvika utukufu na heshima kila mtu  ambaye atakuwa tayari kumpokea, na kuishi Maisha matakatifu na kuyashinda Maisha ya ulimwengu biblia inatuambia..

Warumi 2:10  “bali utukufu na heshima na amani kwa kila mtu atendaye mema, Myahudi kwanza na Myunani pia; 11  kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu”.

Unaona?. Kuna mambo mazuri sana, Mungu aliyotuandalia mbinguni, mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia, wala hayajawahi kuingia katika moyo wa mwanadamu. Tutavikwa mataji ya utukufu na heshima, tutang’aa kama jua, tutaishi Maisha ya raha na furaha milele, tutasahau yote tuliyopitia nyuma. Tutapewa miili ya utukufu isiyougua milele, isiyozeeka, isiyo chakaa, isiyo minyonge, isiyo na ulemavu. Na Zaidi ya yote Tutatawala la Mungu, tuyafurahia Maisha kwa miaka isiyokuwa na mwisho,.. Ni raha iliyoje? Ni heri tukose kila kitu duniani lakini tusikose, heshima hiyo Mungu aliyotuandalia kule ng’ambo.

Lakini, ni kinyume chake ni kwamba wale ambao leo hii duniani hawataki kuutafuta huu utukufu na heshima idumuo, utokao kwa Mungu, siku ile ya hukumu watapata hasira na ghadhabu ya milele.

Warumi 2:7  wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele;

8  na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu;

9 Utukufu na Heshima ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia.

Tunaishi katika siku ambazo unyakuo, unaweza kutokea siku yoyote. Na watakatifu kunyakuliwa mbinguni. Dalili zote zinathibitisha hilo, na dalili mojawapo kuu ni hilo la kuzuka kwa magonjwa yasiyokuwa na tiba ambayo biblia imeyafananisha na TAUNI..Leo hii duniani tunaona magonjwa kama CORONA, yanatimiliza unabii wazi wazi mbele ya macho yetu…Tuseme nini tena?

Je wewe nawe bado upo nje ya Kristo? Ingia ndugu yake ndugu yangu, Kristo ayabadilishe Maisha yako. Ukiamua leo kwa dhati kutubu dhambi zako Kristo atakupa utukufu na heshima isiyoharibika kwako. Haijalishi ulikuwa mlevi kiasi gani, umetoa mimba nyingi namna gani, umeua watu wengi kiasi gani, umeloga sana watu namna gani, umezini mara nyingi namna gani..Kristo yupo tayari kukusamehe leo hii ikiwa kwa moyo wako wa dhati utakubali..

Kama upo tayari kufanya hivyo..

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako.

Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ubarikiwe sana.

Utukufu na Heshima, zina Mungu wetu daima.

Mada Nyinginezo:

UNYAKUO.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

MAONO YA NABII AMOSI.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments